Dar: Mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHADEMA), afikishwa Mahakamani Kisutu, ashitakiwa kwa makosa 2 apata dhamana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
aja1.jpg

Mbunge wa Kawe Halima Mdee afikishwa Mahakamani Kisutu na Kupandishwa Kizimbani.

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar, katika Uwanja wa Ndege wa Dar-es-Salaam Julius Nyerere International Airport(JNIA) alipowasili majira ya saa 9 alfajiri siku ya Jumapili ya Tarehe 01/ 03/2018, akitokea nchini Afrika Kusini, ilikoelezwa kuwa alikuwa akipatiwa matibabu.

Alinyimwa dhamana ya Polisi hadi leo alipofikishwa Kisutu.

Ameunganishwa kwenye Kesi ya Wakina Mbowe. Mabishano yanaendelea Mahakamani ya kupewe dhamana au la.

=>Halima Mdee, amesomewa mashtaka mawili baada ya kufikishwa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam ambayo ni;

1) Kufanya mkusanyiko usio halali.

2) Kuendelea na mkusanyiko huo licha ya kuamriwa kutawanyika na hivyo kusababisha kifo cha Mwanafunzi Akwilina Akwilin.

=> Halima Mdee amepata dhamana.

Habari zaidi, Soma=>DAR: Jeshi la Polisi lamkamata Halima Mdee akiwa Uwanja wa ndege(JNIA) akitokea Afrika Kusini kwenye matibabu

====

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri baada ya kusikiliza hoja za pande zote ametupilia mbali pingamizi la dhamana dhidi ya mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, badala yake ameamuru apewe dhamana kwa masharti kama ya washtakiwa wengine wa chama hicho.

Akizungumza leo katika Mahakama hiyo katika kesi inayomkabili mbunge huyo na viongozi wengine wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mashauri amesema hakuna sheria inayoeleza kuwa mshtakiwa akiruka dhamana ya polisi na mahakamani, anyimwe dhamana kwa kuwa hizo ni taasisi mbili tofauti.

Mdee ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambayo ni kusaini bondi ya dhamana ya Sh20 milioni, kuwa na wadhamini wawili na kuripoti kituo kikuu cha Polisi kila Ijumaa.
 
Hatimaye Mbunge Halima Mdee apata dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20 na kuripoti mara moja kila wiki..
 
hivi wale polisi 6 waliokamatwa.
kuhusika na hilo tukio.
wamekula chakula leo
 
Back
Top Bottom