Dar: Mbunge wa jimbo la Liwale(CUF) Zuberi Kuchauka atangaza kujiuzulu na kuhamia CCM

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,703
2,000
DkeHfOHWwAAYIdV.jpg

Dkt. Bashiru Ali amempokea Zuberi Mohamed aliyekuwa Mbunge wa CUF Liwale Mkoani Lindi.

Anasema anarejea CCM imebadilika. CCM aliyoiacha mwaka 2005 sio hii ya leo. Hii CCM ya awamu ya tano nmekubali kwamba imerejea kwenye Misingi ya TANU. Misingi ya TANU imerejea, hivyo sikuona kigugumizi cha kurejea.

Mimi nlikuwa CUF, Sasa hivi mtu ukimuuliza nipo CUF unaulizwa CUF gani? Hii inanipunguzia uwezo wa kufanya kazi. Migogoro ni Mingi.

Wananchi wa Liwale wanajua nimewafanyia mambo makubwa sana. CCM imewafanyia mambo makubwa sana

Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana, na sisi inabidi tumshike mkono umsaidia.

Migogoro mingi ya Liwale imeanza kuisha. Sasa hivi Mawaziri wanatembelea Liwale tofauti na Zamani,

Naomba Wanachama wa CCM mnipokee, nlipotea nimerejea tufanye kazi. amesema Zuberi Mohammed Kuchauka aliyekuwa Mbunge wa CUF.

Mwaka 2017, kulikuwepo mjadala mkubwa hapa JamiiForums, kuhusiana na huyu Mbunge kuhamia CCM.

Habari zaidi, soma=>Mbunge wa Jimbo la Liwale CUF Zuberi Kuchauka, muda wowote atahamia CCM - JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom