DAR: Mbunge Esther Bulaya(CHADEMA) aitwa Polisi kwa Mahojiano, amepata dhamana

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (ZCO), imemuita kwa ajili ya mahojiano Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa Bunda mjini, Mhe Ester Bulaya.
FB_IMG_1522939553942.jpg

ameambatana na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee(CHADEMA) kwenda huko Polisi.

Bulaya alifika Mahakamani hapa Kisutu kuhudhuria kesi ya Mbunge Mwenzake wa Tarime Vijijini John Heche

Haijafahamika wazi anaenda kuhojiwa juu ya nini hasa, ila inadaiwa anaenda kuhojiwa kuhusu maandamano yaliyofanyika Februari 16, 2018 katika eneo la Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

====

Amehojiwa kuhusu uchochezi. Amepata dhamana Polisi kwa kudhaminiwa na Wadhamini wawili. Anatakiwa kurepoti tena 13/04/2018.
 
Alitaka na yeye awekwe ndani ili mwenyekiti aitishe press.
 
Hii Wizara chini ya Madaru aka Mwigulu Nchemba sasa imegeuka kuwa tawi la chama flani cha siasa na kazi yao imebaki kuharass watu. Mbunge wa Bunda, aliyepo Dodoma kutimiza wajibu wake anaitwa na polisi wa Mambosasa aende Darisalama. Sijui huwa wanawawekea mafuta kwenye magari yao?
 
Wakuu,

Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya(CHADEMA) ameitwa Kituo kikuu cha polisi kuhojiwa na ameondoka na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee(CHADEMA) kwenda huko.

More to follow...
Sasa viwanda vitakuwa vingi sana
 
Hii Wizara chini ya Madaru aka Mwigulu Nchemba sasa imegeuka kuwa tawi la chama flani cha siasa na kazi yao imebaki kuharass watu. Mbunge wa Bunda, aliyepo Dodoma kutimiza wajibu wake anaitwa na polisi wa Mambosasa aende Darisalama. Sijui huwa wanawawekea mafuta kwenye magari yao?
Ndiyo hali halisi mkuu, ukizingatia wizara yenyewe ipo chini ya naibu rais.
 
Back
Top Bottom