KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,156
Kwa umri wangu nimeshuhudia utekelezaji wa llani za vyama kwa miaka ipatayo 15 lakini sijapata kuona ufanisi wa utekelezaji wake kama miaka mitatu ya JPM madarakani.
Kwa kasi hii, naamini huyu mzee atatekeleza ahadi zote na kutekeleza za nyongeza ambazo haxikuwepo kwenye llani ya 2015 - 2020.
Mm sina Chama lakini kwa kasi ninayoyaiona huyu mzee nnayo kura yake 2020 bila hata kampeni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umeangalia upande mmoja au jambo moja tu ambalo pengine wengi wetu tunaweza kuungana nawe.
Kwa bahati mbaya sana unasahau pande nyingine ambazo pia ni muhimu na za msingi zaidi hata kuuzidi upande huo mmoja tunaokubaliana na wewe kuhusu haya mazuri tunayoyataka sote yatokee kwenye nchi yetu.
Wengine tutamnyima kura zetu kwa kuyaangalia hayo ya msingi zaidi anayoyaharibu kama kutakuwepo na chaguo mbadala litakaloweka matumaini juu ya hayo anayoyaharibu.