Dar: Mapokezi ya ndege ya pili ya ATCL aina ya AirBus A220-300(Ngorongoro) katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere


Roving Journalist

Roving Journalist

Senior Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
198
Likes
1,622
Points
180
Roving Journalist

Roving Journalist

Senior Member
Joined Apr 18, 2017
198 1,622 180
Rais Magufuli leo anatarajia kuongoza watanzania kupokea ndege nyingine ya sita aina ya Airbus A220-300, inayowasili hapa nchini ikitokea nchini Canada, na kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa katika kipindi cha awamu ya tano kufikia 6.

UPDATES; 1520hrs

=> Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 iliyonunuliwa na serikali yatua uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar muda huu. Rais John Magufuli, viongozi waandamizi, viongozi wa dini na wananchi wajitokeza kuipokea.

=> Askofu Kakobe: "Hata ungefanya kitu gani huwezi kusifiwa na Watu wote na MUNGU anasema kama utasifiwa na Watu wote basi ni ole wako, tumekusanyika kwa ajili ya ndege za ATCL ni jambo zito na kubwa lakini usitarajie Watu wote watakusifu, wengine watakusifu ukifa"
fb_img_1547218887609-jpg.991910

“Mheshimiwa mimi huwa ni mbishi kidogo…na ukiona nimekuja mahali kama hapa…ujue umenikosha,” – kauli ya Mchungaji wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe akikiri kukoshwa na Rais

Kakobe amsihi Rais Magufuli alale. “…Umewahi kutuambia unashindwa kulala kwa sababu kitanda kimejaa mafaili…lakini leo tunakusihi…hebu jipongeze ulale…” – kauli ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe.

Paul Makonda: Mh. Rais naomba niruhusu kwa leo nikupe salamu tu kwa kuwa furaha yangu imezidi

> Pokea salamu kutoka kwa Mwl. Christopher Mwakasege. Anakupongeza kwa jambo kubwa unalolifanya ila ameshindwa kuja yupo Tukuyu kwa jambo la kifamilia.

Paul Makonda: Nilipotoa tangazo la kuja hapa nilisema waje wale waliowahi kutoa ahadi na wakatekeleza.

> Tumekuja kukuunga mkono kwa kuwa ulitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na unatekeleza ikiwemo elimu bure

Paul Makonda: Hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama baba wa familia. Nikikua nataka niwe kama wewe

Akizungumza katika mapokezi ya ndege aina Airbus A220-300 hapa uwanja wa ndege, RC Paul Makonda amewataka viongozi wa Dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Dkt Magufuli.

Serikali imesema Ndege mpya iliyopokelewa leo aina ya AIRBUS A220-300 NGORONGORO itakuwa na safari za kila siku kwenda Dodoma kuanzia January 16 mwaka huu tofauti na ilivyo sasa ambapo ATCL hufanya safari 4 tu kwa wiki kwenda Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji ATCL Ladislaus Matindi: Ujazo wa ndege hizi 2 za Airbus unatuwezesha kutoa huduma kwa Mkoa wa Mtwara na mikoa yenye viwanja vidogo

> Ndege hizi zote zina uwezo wa kubeba tani 19 na tayari tumefanikiwa kuingia kwenye makubaliano ya kusafirisha nyama ya mbuzi

Matindi: Tayari tunashirikiana na ubalozi wa Uingereza ili kuwakutanisha wadau wa usafiri wa ndege kuweza kujadiliana na kukubaliana kuhusu fursa zilizopo kwenye shirika la ndege
fb_img_1547214211302-jpg.991911

Matindi: Baada ya kurudisha kwenye mfumo wa tiketi duniani kazi ya kuunganisha ATCL kwenyw mfumo huo inategemewa kuwa imekamilika Januari hii.

> Tunatazamia pia kutoa huduma kwa wateja kwa saa 24 kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo kwenye matengenezo

Matindi: Kufika kwa ndege hii kunahitimisha mkataba wa ununuzi wa ndege mbili za Airbus A220-300, ndege hizi zinatuwezesha kuwa na upanuzi wa mtandao wa safari zetu na kutoa huduma za kimkakati katika soko la Kusini mwa Afrika

Ladslaus Matindi: Katika safari ya ndege hii tulikuwa na Kapteni Khamisi, Kapteni Msingi na aliyeiteremsha ndege hapa nchini ni Kampteni Budodi na kiongozi wa safari alikuwa ni Kapteni Patric anayetoka kwenye kampuni iliyotuuzia ndege na atakuwa hapa kwa miezi 3 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana wetu

Waziri Mkuu Majaliwa: Jambo hili ni kubwa sana na tunaamini wafanyakazi mtafanya kazi kwa weledi na kuendelea kuliinua shirika letu na ukitaka usafiri mzuri safiri na Air Tanzania

Mhandisi Isack Kamwelwe: Nakupongeza Rais wangu kwamba uliweka nia na ukaagiza tununue ndege 7 na zimenunuliwa ambapo Oktoba mwaka huu inaingia ndege nyingine na juzi umeniambia tununue ndege nyingine tena

Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson: Sisi kama Bunge tunakupongeza Rais kwa kazi kubwa unayoendelea kuifanya, sote ni mashahidi kwa kinachoendelea, ulipokuja bungeni kusema utanunua ndege hatukuamini lakini kama matani tunazo ndege Sita

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa na ninawashukuru sana viongozi wa dini, wamemaliza maneno mazuri ambayo tulitakiwa kuyazungumza hapa. Endeleni kuliombea taifa hili

Mafanikio ya ndege hizi 6 ni shuhuda tosha wa nguvu za watanzania hivyo watanzania hongereni sana.

Ndege hizi ni zenu, hakuna hata senti 5 iliyotoka kwa mfadhili kununua ndege hizi. Mfadhili ni mtanzania.

Ukangalia nchi zingine utakuta ndege zina "percent" kubwa inayomilikiwa na watu wengine hata kama zina majina ya nchi hizo lakini Tanzania Air Tanzania inamilikiwa na watanzania 100%.

Napenda kutoa wito kama pesa imepangwa ikanunue ndege basi ikanunue ndege

Kwa taarifa yenu kitendo cha ndege hii kuchelewa hiyo kampuni imetulipa hela dola milioni 1.3 na wameandika "cheque" na wanairudisha pesa Wizara ya fedha.

Hiyo ndiyo Tanzania ninayoitaka mimi, Tanzania ya ukweli na uwazi

Na walipokuwa huko niliwaambia hakuna kuacha cheque huko waje nayo ingekuwa miaka mingine hizo pesa zingebaki huko na kuliwa hukohuko

Tunafanya kazi kwa mapenzi makubwa kwenu watanzania na ni kwa watanzania wote, vyama vyote, makabila yote na dini zote maana maendeleo hayana vyama

Nimesikia wito wa Kakobe kwamba wao wanavyokutana na sisi wanasiasa tuwe tunakutana lakini shida kubwa huwezi ukawa unakutana na mtu anakutakana tukana hovyo kwamba uchinjwe ufie huko

Hakuna nchi duniani iliyofanikiwa kwa kupewa misaada. Ninawaambia watanzania wenzangu, itafuteni hamtaipata

Ili nchi ifanikiwe lazima ijitegemee na saa nyingine ukipewa misaada sana inakulemaza.

Tunahitaji misaada sana lakini iwe ya kutufanya tuweze kusimama na tunahitaji ushirikiano kutoka nchi zingine lakini lazima iwe ya kumuwezesha mtanzania kujitegemea

Pia tunahitaji wawekezaji kutoka nchi zingine

Katika kipindi ambacho ndege zimeanza kununuliwa tayari wafanyakazi 380 wameshaajiriwa, hivyo ununuzi wa ndege hizi umegusa maisha ya Watanzania

Ndege hii tuliyoipokea leo sio ya mwisho, mwishoni mwa mwaka huu tunategemea kuleta ndege nyingine aina ya Dreamliner itakayobeba abiria 262

Tunataka baada ya miaka 10 au 20 Tanzania tuwe na ndege hata 100, tushindane na mashirika mengine makubwa duniani,Tanzania tunaweza

Na nyie ATCL punguzeni matumizi mabaya. Kuna wakati ndege ilikuwa inaenda Dubai kuchukua nguo kwa ajili ya maduka ya watu Fulani Fulani

Hizi ndege mmeazimwa. Ni sawa na koti, wameazimwa. Wakifanya ovyo, tunawanyang'anya. Tunaweza hata kuwapa Precision

Nashukuru sana Bunge. Mheshimiwa Spika, Naibu, wenyeviti wa kamati na wabunge kwa kupitisha manunuzi ya ndege hizi. Nawapongeza sana wabunge wa CCM

Napenda sana kukipongeza chama changu hasa Katibu Mkuu Dkt.Bashiru Ally amekuwa muwazi sana

Ndege hizi za Rais ambazo ziko tatu, mbili zitapakwa rangi ya Air Tanzania zikabebe abiria siku ambapo hazibebi huku kwetu zikabebe abiria, Rais kwanza sitembei sana

Kwa miaka 8 tulikuwa hatujapa gawio kutoka Airtel.

Leo amekuja Chairman wa Airtel na kakubali hisa zao zishuke. Wakipiga hesabu vizuri wataanza kutoa gawio

Tanzania itakuwa Ulaya. Niamini. Nawaomba Watanzania kila mmoja aamini hivyo.

Haya yaliyopatikana ndani ya miaka mitatu ni rasharasha. Mvua zinakuja

Nimpongeze kijana huyu Mwenyekiti wa ATCL alikuwa anafanya kazi nchini Senegal alikokuwa analipwa mshahara mkubwa lakini tulipomuambia tunataka kurudisha shirika letu alikubali kurudi kufanya kazi hapa na kuacha mshahara mkubwa huko

Mkuu wa mkoa Paul Makonda ameomba awe kama mimi, na mimi namuombea awe zaidi yangu

Niwapongeze sana Bendi ya TOT mmebadilika sana na leo mmepiga Mziki mzuri mpaka nikatamani kucheza na Mama Majaliwa hapa lakini nikaogopa sababu Majaliwa ana wivu sana

Pia nakupongeza Balozi kwa kuzungumza Kiswahili, sisi Watanzania tumekuwa watu wa 'How are you', 'How are you my son', sasa umewafundisha.

Balozi huyu ana miezi mitatu tuu hapa lakini ameonesha mfano na kuwafundisha wale ambao wanaona aibu

Rais Magufuli: Nimpongeze kijana huyu Mwenyekiti wa ATCL alikuwa anafanya kazi nchini Senegal alikokuwa analipwa mshahara mkubwa lakini tulipomuambia tunataka kurudisha shirika letu alikubali kurudi kufanya kazi hapa na kuacha mshahara mkubwa huko
 
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
2,726
Likes
689
Points
280
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
2,726 689 280
[QUOTE="Roving Journalist,]

Tanzania itakuwa Ulaya. Niamini. Nawaomba Watanzania kila mmoja aamini hivyo.
Tukisikia kauli kama hizi ndo watu hujikuta tunaporomosha matusi...hivi hili jitu liko sawa kweli kichwani?[/QUOTE]
Kwa nini matusi? Mbona yeye hajatukana au kusema itakua ulaya ndo tusi? Punguza jazba kwani siku ikiwa ulaya kweli utatahayari buree
 
truth'spassword

truth'spassword

Member
Joined
Dec 4, 2013
Messages
43
Likes
65
Points
25
truth'spassword

truth'spassword

Member
Joined Dec 4, 2013
43 65 25
Askofu Kakobe amenukuliwa akiyasema hayo siku ya leo pale alipoalikwa kwenye uzinduzi wa Air Tanzania, na kupewa nafasi ya kufungua warsha kwa maombi.

"Kabla ya kuomba ni vyema tungeanza na neno kidogo ili hata maombi yenyewe yanoge kidogo".. Alinukuliwa Askofu.
Alianza kwa maandiko, Luka 6:26 '..mheshimiwa Rais Ole wenu watu wote watakapowasifu, Mungu anasema ukiona watu wote wanakusifu basi Ole wako..' Aliongeza

Askofu aliongeza tena kusema, mheshimiwa rais haya unayoyafanya usitegemee kila mtu atakusifu, hata kama ungegawa gunia moja moja kwa kila kaya wapo ambao wangesema umetuwekea sumu.
"Mimi ni mbishi sana, hivyo unapoona nimekuja mahali kama hapa, ujue kweli nimekoshwa." Alisema Askofu Kakobe. Watu wanasema ni kodi zetu zimenunua ndege hizi, sawa kwani hata abiria wanaposafiri safari ndefu hata kama wamelioa nauli, Je hawampongezi rubani aliyewasafirisha salama ? Sisi tunaye rubani mzuri, rais john magufuli... Aliongeza Askofu Kakobe.Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alexander The Great

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
2,053
Likes
5,531
Points
280
Alexander The Great

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2018
2,053 5,531 280
Askofu Kakobe anathubutu hata kumpiga "FIX" mungu sasa, achilia mbali sisi raia.

Kuna wazee kila umri ukizidi kwenda mbele wanazidi kua na BUSARA, ila kuna wengine kila wakizeeka wanazidi kuwa WEHU.
 
K

kakolaki

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2017
Messages
449
Likes
361
Points
80
K

kakolaki

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2017
449 361 80
Uamuzi sahihi kabisa nakumbuka kuna siku tulikwama Kigoma ATCL walikodi hiyo Fokker ni ndege ya abiria kabisa ndani haina tofauti kwamba ni special plane hapana, na infact kwa logic hizo mbili zina umri mkubwa hivyo baada ya muda mfupi zaweza kuwa outdated kwa matumizi ya viongozi hivyo bora zizalishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
C

Ctr

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Messages
436
Likes
102
Points
60
C

Ctr

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2013
436 102 60
Uamuzi sahihi kabisa nakumbuka kuna siku tulikwama Kigoma ATCL walikodi hiyo Fokker ni ndege ya abiria kabisa ndani haina tofauti kwamba ni special plane hapana, na infact kwa logic hizo mbili zina umri mkubwa hivyo baada ya muda mfupi zaweza kuwa outdated kwa matumizi ya viongozi hivyo bora zizalishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu anapofanya kizuri hana budi kusifiwa ki ukweli mheshimiwa rais nampa hongera kwa hili suala la ununuzi wa ndege maana utalii wa ndani utaongezeka kwa kiwango kikubwa,chamsingi ni kuangalia uendeshaji wake wa shirika la ndege isije ikatokea kama yale ya nyuma, kwa kifupi nawapa hongera CCM kwa kumpata mtu sahihi kwa wakati sahihi kama huu
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,923
Likes
8,919
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,923 8,919 280
"JokaKuu, post: 29983814, member: 221"]..nadhani ilitosha kupokea ile kubwa ya kwanza.
.hizi nyingine angemuachia Dr.Mbarawa au Mh.Kamwelwe wazipokee.
Sikumbuki kuona Mwl akiwa amewakusanya watu kila mara. Hata Uwanja wa ndege terminal II Mwl alikwenda kufungua na kuondoka. Ndege za ATC zilipowasili baada ya EAC hatukuona haya. Kuna wakati muda wa viongozi uzingatiwe na matukio yapewe kipaumbele
..pia angesitisha kuwakusanya Spika, Jaji Mkuu, CDF, IGP, na viongozi wengine wakuu ktk hafla za kuapisha wateule wapya.
Hili ni tukio la kiofisi.
Sikuona siku za nyuma watu wakipewa nafasi ya kuhutubia baada ya kuapishwa au wakijazana na familia zao. Ni tukio la kisheria baasi, Kuwakusanya viongozi hao haipendezi.
Kila kiongozi atakuwepo eneo lake likihusika wengine sidhani kama wanahitajika
Kuna uhusiano gani, kwa mfano kumwapisha Mkurugenzi au katibu mkuu wa wizara na uwepo wa viongozi wakuu wa mihimili na maeneo mengine?
..Zoezi la kuapishwa inafaa lihudhuriwe na wasaidizi muhimu wa Ofisi ya Raisi, watendaji wa mamlaka ya nidhamu ya aliyeteuliwa, pamoja na wanafamilia wachache.
exactly
..Kinachoendelea sasa hivi kinanikumbusha kipindi cha Raisi Kikwete ambapo kulikuwa na utaratibu wa serekali nzima na vyombo vyake kwenda kumuaga na kumpokea kila anaposafiri
Kuna wakati Mwl alikataa hayo. Alikuwa akisubiriwa na wanafunzi akauliza, wanasoma saa ngapi?

Kuna mambo ya siasa, ya kiofisi, taratibu na protokali. Sidhani kama wasaidizi wanamsaidia Mheshimiwa kuyaratibu kwa ukubwa na hadhi ya ofisi
 
Magonjwa Mtambuka

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Messages
16,831
Likes
9,958
Points
280
Magonjwa Mtambuka

Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2016
16,831 9,958 280
Sikumbuki kuona Mwl akiwa amewakusanya watu kila mara. Hata Uwanja wa ndege terminal II Mwl alikwenda kufungua na kuondoka. Ndege za ATC zilipowasili baada ya EAC hatukuona haya. Kuna wakati muda wa viongozi uzingatiwe na matukio yapewe kipaumbele Hili ni tukio la kiofisi.
Sikuona siku za nyuma watu wakipewa nafasi ya kuhutubia baada ya kuapishwa au wakijazana na familia zao. Ni tukio la kisheria baasi, Kuwakusanya viongozi hao haipendezi.
Kila kiongozi atakuwepo eneo lake likihusika wengine sidhani kama wanahitajika
Kuna uhusiano gani, kwa mfano kumwapisha Mkurugenzi au katibu mkuu wa wizara na uwepo wa viongozi wakuu wa mihimili na maeneo mengine? exactly
Kuna wakati Mwl alikataa hayo. Alikuwa akisubiriwa na wanafunzi akauliza, wanasoma saa ngapi?

Kuna mambo ya siasa, ya kiofisi, taratibu na protokali. Sidhani kama wasaidizi wanamsaidia Mheshimiwa kuyaratibu kwa ukubwa na hadhi ya ofisi
Sasa unataka kila mtu afanye kama alivyofanya Mwalimu?
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
12,923
Likes
8,919
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
12,923 8,919 280
Sasa unataka kila mtu afanye kama alivyofanya Mwalimu?
At least kwa standard inayokaribiana.
Kuna sababu gani za kuwa na hotuba za kupokea ndege kila siku?
Je,yale majukumu tuliyoambiwa yanamzuia mh kuhudhuria hata majanga, yamekwisha?
Kakobe si tuliambiwa si raia, leo anapozungumza kunatoa picha gani hasa idara ya uhamiaji?

JokaKuu
 
K

Kahinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2009
Messages
869
Likes
152
Points
60
K

Kahinda

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2009
869 152 60
Mkuu Loth
Je? Ni vibaya kumpongeza mtu anapofanya jambo jema?.
Rais Magufuli akifanya vyema tumpongeze kama tunavyo msema ovyo asipofanya vyema.
Ndege hizi, barabara na madaraja kwenye njia panda hivyo vinastahili pongezi kwake. Kwani pamoja na kodi zetu bado amezitumia vizuri na zimeonyesha matunda kuliko kishia kwenye matumbo ya wajuaji wachache.
2. Kama binadamu lazima kuna mahali atakosea, lakini kwa watu wastaarabu lazima tuweke mzani wa mema na mabaya.
3. Watanzania tujifunze kutumia akili zetu wenyewe tuache kulishwa mawazo ya watu.
Hayo ni mawazo yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M

muchetz

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2010
Messages
811
Likes
465
Points
80
M

muchetz

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2010
811 465 80
Ukweli ni kuwa hizi ndege A220-300 ni Bombadier CS300 iliyobadilishwa jina baada ya kuchukuliwa na Airbus. Kwanini hatuambiwi hii kweli sehemu yoyote?
 
sekindunda

sekindunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2017
Messages
281
Likes
167
Points
60
sekindunda

sekindunda

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2017
281 167 60
Watu wanapiga kelele, ooh Mhe anavunja Katiba, anatumia fedha bila idhini ya Bunge, yaani mradi basi watu wanacheza ngoma wasiyoijua.

Kwa wajuvi wa Katiba yetu wanaelewa, kuna vifungu vinampa mamlaka Mhe Rais kufanya matumizi ya fedha za Umma ndo atoe taarifa Bungeni.

Hata hvyo, kama ingekuwa kweli kwamba anatumia fedha bila idhini ya Bunge tujiulize,

Je Serikali zilizokuwa zinatumia fedha kwa idhini ya Bunge zilikuwa na ufanisi kiasi gani!?

Je, fedha hizi zinazotumiwa bila idhini ya Bunge zinatumiwa kwa maslahi ya umma!?

Je, Watanzania mahitaji yetu ni kuwa na Kiongozi anayezingatia Katiba pekee au anayelinda maslahi ya Taifa!?

Tukijiuliza maswali haya kizalendo kabisa bila mihemko ya Kisiasa naamini tutapata majawabu mujarabu yatakayotupa picha pana na kumuunga mkono Kiongozi wetu mpendwa.

Kwa imani yangu, Mhe Rais anao upungufu wake kama binadamu, lakini wakele walisema "Mngonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!
Mkuu Loth
Je? Ni vibaya kumpongeza mtu anapofanya jambo jema?.
Rais Magufuli akifanya vyema tumpongeze kama tunavyo msema ovyo asipofanya vyema.
Ndege hizi, barabara na madaraja kwenye njia panda hivyo vinastahili pongezi kwake. Kwani pamoja na kodi zetu bado amezitumia vizuri na zimeonyesha matunda kuliko kishia kwenye matumbo ya wajuaji wachache.
2. Kama binadamu lazima kuna mahali atakosea, lakini kwa watu wastaarabu lazima tuweke mzani wa mema na mabaya.
3. Watanzania tujifunze kutumia akili zetu wenyewe tuache kulishwa mawazo ya watu.
Hayo ni mawazo yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
7,800
Likes
9,291
Points
280
Age
27
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
7,800 9,291 280
Ukweli ni kuwa hizi ndege A220-300 ni Bombadier CS300 iliyobadilishwa jina baada ya kuchukuliwa na Airbus. Kwanini hatuambiwi hii kweli sehemu yoyote?
Mbona walishasema toka ndege ya kwanza ilipowasili kwanza.
Ukitembelea website ya bomberdier wameeleza vizur, sambamba na airbus wenyewe pia wameelezea vizur tu.
Ni vizur ukajisome mwenyewe kuliko kusubiri kuambiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
7,800
Likes
9,291
Points
280
Age
27
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
7,800 9,291 280
Hahahaha! Kumbe DAB ndiye anayefanya kazi ya kuwashawishi Viongozi wa dini wawepo kwenye matamasha ya mfalme! Naona walikuwa wanajaribu kumshawishi na Mwl. Mwakasege awepo, DAB utasubiri sana. Huyo haendi kokote kama sio Roho Mtakatifu kamtuma. Si rahisi sana kumtumia kisihasa kama unavyoweza wazoa wengine!
Mwakasege ni true mtumishi wa Mungu. Huwa anaomba kibali kwanza kwa Mungu. Haendi hiv hiv

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,250,085
Members 481,224
Posts 29,720,455