Dar: Mapokezi ya ndege ya pili ya ATCL aina ya AirBus A220-300(Ngorongoro) katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere


Roving Journalist

Roving Journalist

Senior Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
198
Likes
1,622
Points
180
Roving Journalist

Roving Journalist

Senior Member
Joined Apr 18, 2017
198 1,622 180
Rais Magufuli leo anatarajia kuongoza watanzania kupokea ndege nyingine ya sita aina ya Airbus A220-300, inayowasili hapa nchini ikitokea nchini Canada, na kufanya idadi ya ndege zilizonunuliwa katika kipindi cha awamu ya tano kufikia 6.

UPDATES; 1520hrs

=> Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 iliyonunuliwa na serikali yatua uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar muda huu. Rais John Magufuli, viongozi waandamizi, viongozi wa dini na wananchi wajitokeza kuipokea.

=> Askofu Kakobe: "Hata ungefanya kitu gani huwezi kusifiwa na Watu wote na MUNGU anasema kama utasifiwa na Watu wote basi ni ole wako, tumekusanyika kwa ajili ya ndege za ATCL ni jambo zito na kubwa lakini usitarajie Watu wote watakusifu, wengine watakusifu ukifa"
fb_img_1547218887609-jpg.991910

“Mheshimiwa mimi huwa ni mbishi kidogo…na ukiona nimekuja mahali kama hapa…ujue umenikosha,” – kauli ya Mchungaji wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe akikiri kukoshwa na Rais

Kakobe amsihi Rais Magufuli alale. “…Umewahi kutuambia unashindwa kulala kwa sababu kitanda kimejaa mafaili…lakini leo tunakusihi…hebu jipongeze ulale…” – kauli ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe.

Paul Makonda: Mh. Rais naomba niruhusu kwa leo nikupe salamu tu kwa kuwa furaha yangu imezidi

> Pokea salamu kutoka kwa Mwl. Christopher Mwakasege. Anakupongeza kwa jambo kubwa unalolifanya ila ameshindwa kuja yupo Tukuyu kwa jambo la kifamilia.

Paul Makonda: Nilipotoa tangazo la kuja hapa nilisema waje wale waliowahi kutoa ahadi na wakatekeleza.

> Tumekuja kukuunga mkono kwa kuwa ulitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na unatekeleza ikiwemo elimu bure

Paul Makonda: Hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama baba wa familia. Nikikua nataka niwe kama wewe

Akizungumza katika mapokezi ya ndege aina Airbus A220-300 hapa uwanja wa ndege, RC Paul Makonda amewataka viongozi wa Dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Dkt Magufuli.

Serikali imesema Ndege mpya iliyopokelewa leo aina ya AIRBUS A220-300 NGORONGORO itakuwa na safari za kila siku kwenda Dodoma kuanzia January 16 mwaka huu tofauti na ilivyo sasa ambapo ATCL hufanya safari 4 tu kwa wiki kwenda Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji ATCL Ladislaus Matindi: Ujazo wa ndege hizi 2 za Airbus unatuwezesha kutoa huduma kwa Mkoa wa Mtwara na mikoa yenye viwanja vidogo

> Ndege hizi zote zina uwezo wa kubeba tani 19 na tayari tumefanikiwa kuingia kwenye makubaliano ya kusafirisha nyama ya mbuzi

Matindi: Tayari tunashirikiana na ubalozi wa Uingereza ili kuwakutanisha wadau wa usafiri wa ndege kuweza kujadiliana na kukubaliana kuhusu fursa zilizopo kwenye shirika la ndege
fb_img_1547214211302-jpg.991911

Matindi: Baada ya kurudisha kwenye mfumo wa tiketi duniani kazi ya kuunganisha ATCL kwenyw mfumo huo inategemewa kuwa imekamilika Januari hii.

> Tunatazamia pia kutoa huduma kwa wateja kwa saa 24 kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo kwenye matengenezo

Matindi: Kufika kwa ndege hii kunahitimisha mkataba wa ununuzi wa ndege mbili za Airbus A220-300, ndege hizi zinatuwezesha kuwa na upanuzi wa mtandao wa safari zetu na kutoa huduma za kimkakati katika soko la Kusini mwa Afrika

Ladslaus Matindi: Katika safari ya ndege hii tulikuwa na Kapteni Khamisi, Kapteni Msingi na aliyeiteremsha ndege hapa nchini ni Kampteni Budodi na kiongozi wa safari alikuwa ni Kapteni Patric anayetoka kwenye kampuni iliyotuuzia ndege na atakuwa hapa kwa miezi 3 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana wetu

Waziri Mkuu Majaliwa: Jambo hili ni kubwa sana na tunaamini wafanyakazi mtafanya kazi kwa weledi na kuendelea kuliinua shirika letu na ukitaka usafiri mzuri safiri na Air Tanzania

Mhandisi Isack Kamwelwe: Nakupongeza Rais wangu kwamba uliweka nia na ukaagiza tununue ndege 7 na zimenunuliwa ambapo Oktoba mwaka huu inaingia ndege nyingine na juzi umeniambia tununue ndege nyingine tena

Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson: Sisi kama Bunge tunakupongeza Rais kwa kazi kubwa unayoendelea kuifanya, sote ni mashahidi kwa kinachoendelea, ulipokuja bungeni kusema utanunua ndege hatukuamini lakini kama matani tunazo ndege Sita

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa na ninawashukuru sana viongozi wa dini, wamemaliza maneno mazuri ambayo tulitakiwa kuyazungumza hapa. Endeleni kuliombea taifa hili

Mafanikio ya ndege hizi 6 ni shuhuda tosha wa nguvu za watanzania hivyo watanzania hongereni sana.

Ndege hizi ni zenu, hakuna hata senti 5 iliyotoka kwa mfadhili kununua ndege hizi. Mfadhili ni mtanzania.

Ukangalia nchi zingine utakuta ndege zina "percent" kubwa inayomilikiwa na watu wengine hata kama zina majina ya nchi hizo lakini Tanzania Air Tanzania inamilikiwa na watanzania 100%.

Napenda kutoa wito kama pesa imepangwa ikanunue ndege basi ikanunue ndege

Kwa taarifa yenu kitendo cha ndege hii kuchelewa hiyo kampuni imetulipa hela dola milioni 1.3 na wameandika "cheque" na wanairudisha pesa Wizara ya fedha.

Hiyo ndiyo Tanzania ninayoitaka mimi, Tanzania ya ukweli na uwazi

Na walipokuwa huko niliwaambia hakuna kuacha cheque huko waje nayo ingekuwa miaka mingine hizo pesa zingebaki huko na kuliwa hukohuko

Tunafanya kazi kwa mapenzi makubwa kwenu watanzania na ni kwa watanzania wote, vyama vyote, makabila yote na dini zote maana maendeleo hayana vyama

Nimesikia wito wa Kakobe kwamba wao wanavyokutana na sisi wanasiasa tuwe tunakutana lakini shida kubwa huwezi ukawa unakutana na mtu anakutakana tukana hovyo kwamba uchinjwe ufie huko

Hakuna nchi duniani iliyofanikiwa kwa kupewa misaada. Ninawaambia watanzania wenzangu, itafuteni hamtaipata

Ili nchi ifanikiwe lazima ijitegemee na saa nyingine ukipewa misaada sana inakulemaza.

Tunahitaji misaada sana lakini iwe ya kutufanya tuweze kusimama na tunahitaji ushirikiano kutoka nchi zingine lakini lazima iwe ya kumuwezesha mtanzania kujitegemea

Pia tunahitaji wawekezaji kutoka nchi zingine

Katika kipindi ambacho ndege zimeanza kununuliwa tayari wafanyakazi 380 wameshaajiriwa, hivyo ununuzi wa ndege hizi umegusa maisha ya Watanzania

Ndege hii tuliyoipokea leo sio ya mwisho, mwishoni mwa mwaka huu tunategemea kuleta ndege nyingine aina ya Dreamliner itakayobeba abiria 262

Tunataka baada ya miaka 10 au 20 Tanzania tuwe na ndege hata 100, tushindane na mashirika mengine makubwa duniani,Tanzania tunaweza

Na nyie ATCL punguzeni matumizi mabaya. Kuna wakati ndege ilikuwa inaenda Dubai kuchukua nguo kwa ajili ya maduka ya watu Fulani Fulani

Hizi ndege mmeazimwa. Ni sawa na koti, wameazimwa. Wakifanya ovyo, tunawanyang'anya. Tunaweza hata kuwapa Precision

Nashukuru sana Bunge. Mheshimiwa Spika, Naibu, wenyeviti wa kamati na wabunge kwa kupitisha manunuzi ya ndege hizi. Nawapongeza sana wabunge wa CCM

Napenda sana kukipongeza chama changu hasa Katibu Mkuu Dkt.Bashiru Ally amekuwa muwazi sana

Ndege hizi za Rais ambazo ziko tatu, mbili zitapakwa rangi ya Air Tanzania zikabebe abiria siku ambapo hazibebi huku kwetu zikabebe abiria, Rais kwanza sitembei sana

Kwa miaka 8 tulikuwa hatujapa gawio kutoka Airtel.

Leo amekuja Chairman wa Airtel na kakubali hisa zao zishuke. Wakipiga hesabu vizuri wataanza kutoa gawio

Tanzania itakuwa Ulaya. Niamini. Nawaomba Watanzania kila mmoja aamini hivyo.

Haya yaliyopatikana ndani ya miaka mitatu ni rasharasha. Mvua zinakuja

Nimpongeze kijana huyu Mwenyekiti wa ATCL alikuwa anafanya kazi nchini Senegal alikokuwa analipwa mshahara mkubwa lakini tulipomuambia tunataka kurudisha shirika letu alikubali kurudi kufanya kazi hapa na kuacha mshahara mkubwa huko

Mkuu wa mkoa Paul Makonda ameomba awe kama mimi, na mimi namuombea awe zaidi yangu

Niwapongeze sana Bendi ya TOT mmebadilika sana na leo mmepiga Mziki mzuri mpaka nikatamani kucheza na Mama Majaliwa hapa lakini nikaogopa sababu Majaliwa ana wivu sana

Pia nakupongeza Balozi kwa kuzungumza Kiswahili, sisi Watanzania tumekuwa watu wa 'How are you', 'How are you my son', sasa umewafundisha.

Balozi huyu ana miezi mitatu tuu hapa lakini ameonesha mfano na kuwafundisha wale ambao wanaona aibu

Rais Magufuli: Nimpongeze kijana huyu Mwenyekiti wa ATCL alikuwa anafanya kazi nchini Senegal alikokuwa analipwa mshahara mkubwa lakini tulipomuambia tunataka kurudisha shirika letu alikubali kurudi kufanya kazi hapa na kuacha mshahara mkubwa huko
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
32,930
Likes
20,380
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
32,930 20,380 280
ndugu, unanikumbusha wakati fulani watu walivyokuwa wanawahi kurudi majumbani mwao ili tu kuwahi kipindi cha ze comedy cha akina Joti.

hata baa nazo zilikuwa zinafurika kwelikweli kwa ajili ya kutizama ze comedy.

wasanii huwa wana mvuto wao usipime bana!!
Teh teh
msabillah

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mzee74

mzee74

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2011
Messages
7,481
Likes
5,590
Points
280
mzee74

mzee74

JF-Expert Member
Joined Sep 17, 2011
7,481 5,590 280
Mabaaa karibu yote yanasikiliza kinachoendelea uwanja wa ndege. Huyu jamaa ni charismatic leader. Jk watu walikuwa hawako interested hivi kusikia speech zake wala hazikuwa na mvuto.
Jpm anavutia wengi mno ndo mana watu wanasubilia speech zake wako radhi hata wasile.

Ikitokea leo akatoka bila kuongea watu hawataridhika kabisa wanamsubili yeye tu wengine ni mbwembwe tu
Upo bar gani kwa sasa kiongozi?
 
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
15,685
Likes
8,156
Points
280
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
15,685 8,156 280
Mabaaa karibu yote yanasikiliza kinachoendelea uwanja wa ndege. Huyu jamaa ni charismatic leader. Jk watu walikuwa hawako interested hivi kusikia speech zake wala hazikuwa na mvuto.
Jpm anavutia wengi mno ndo mana watu wanasubilia speech zake wako radhi hata wasile.

Ikitokea leo akatoka bila kuongea watu hawataridhika kabisa wanamsubili yeye tu wengine ni mbwembwe tu
Kumbe wewe ni mzururaji kutwa kucha unapita kwenye mabaa kupiga mizinga ya vinywaji,shauri yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
P

Pilim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
218
Likes
124
Points
60
P

Pilim

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2016
218 124 60
  • Taashira -Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa. Symbolism
  • Taswira -
  • Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
  • Tashihisi -Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Uhuishaji. Personification.
  • Chuku -Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu. Kutilia Chumvi. Hyperbole
Matumizi ya lugha!
 
jogoo_dume

jogoo_dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Messages
1,490
Likes
993
Points
280
jogoo_dume

jogoo_dume

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2014
1,490 993 280
Mafisiem yanapata tabu sana kuchezeshwa singeli kila uchao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona pipa lingine limekuvuruga kabisa. Tunasubiri na tamko la lissu kulaani manunuzi ya ndege siku atakapokuwa anahutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa.
 
sekindunda

sekindunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2017
Messages
281
Likes
167
Points
60
sekindunda

sekindunda

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2017
281 167 60
Kwa umri wangu nimeshuhudia utekelezaji wa llani za vyama kwa miaka ipatayo 15 lakini sijapata kuona ufanisi wa utekelezaji wake kama miaka mitatu ya JPM madarakani.

Kwa kasi hii, naamini huyu mzee atatekeleza ahadi zote na kutekeleza za nyongeza ambazo haxikuwepo kwenye llani ya 2015 - 2020.

Mm sina Chama lakini kwa kasi ninayoyaiona huyu mzee nnayo kura yake 2020 bila hata kampeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2007
Messages
10,608
Likes
3,991
Points
280
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2007
10,608 3,991 280
Ndege ni mali ya serikali chini ya Government Flight Agency, hao ndio wanaikodisha ATCL ndio maana kama umeona pale kuna tukio la Balozi Eng. Kijazi kutiliana saini na watu wa wizara ya mawasiliano ili kuwakabidhi hizo ndege.
Huoni ni kama vile anasukumiziwa lile zigo la 1.5 T taratibu ..............!!?
 
P

phunter

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Messages
378
Likes
100
Points
60
P

phunter

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2013
378 100 60
Mabaaa karibu yote yanasikiliza kinachoendelea uwanja wa ndege. Huyu jamaa ni charismatic leader. Jk watu walikuwa hawako interested hivi kusikia speech zake wala hazikuwa na mvuto.
Jpm anavutia wengi mno ndo mana watu wanasubilia speech zake wako radhi hata wasile.

Ikitokea leo akatoka bila kuongea watu hawataridhika kabisa wanamsubili yeye tu wengine ni mbwembwe tu
Hata tamthilia na katuni zinatazamwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
32,930
Likes
20,380
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
32,930 20,380 280
Kwa umri wangu nimeshuhudia utekelezaji wa llani za vyama kwa miaka ipatayo 15 lakini sijapata kuona ufanisi wa utekelezaji wake kama miaka mitatu ya JPM madarakani.

Kwa kasi hii, naamini huyu mzee atatekeleza ahadi zote na kutekeleza za nyongeza ambazo haxikuwepo kwenye llani ya 2015 - 2020.

Mm sina Chama lakini kwa kasi ninayoyaiona huyu mzee nnayo kura yake 2020 bila hata kampeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunapokea mzigo kutoka kwa mabeberu!

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S

SAIDWE

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
296
Likes
169
Points
60
S

SAIDWE

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
296 169 60
Hahahaha! Kumbe DAB ndiye anayefanya kazi ya kuwashawishi Viongozi wa dini wawepo kwenye matamasha ya mfalme! Naona walikuwa wanajaribu kumshawishi na Mwl. Mwakasege awepo, DAB utasubiri sana. Huyo haendi kokote kama sio Roho Mtakatifu kamtuma. Si rahisi sana kumtumia kisihasa kama unavyoweza wazoa wengine!
 
S

SAIDWE

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
296
Likes
169
Points
60
S

SAIDWE

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
296 169 60
Hahahaha! Kumbe DAB ndiye anayefanya kazi ya kuwashawishi Viongozi wa dini wawepo kwenye matamasha ya mfalme! Naona walikuwa wanajaribu kumshawishi na Mwl. Mwakasege awepo, DAB utasubiri sana. Huyo haendi kokote kama sio Roho Mtakatifu kamtuma. Si rahisi sana kumtumia kisihasa kama unavyoweza wazoa wengine
 

Forum statistics

Threads 1,250,085
Members 481,224
Posts 29,720,455