DAR: Makamu Mwenyekiti NCCR-Mageuzi(Bara) aondoka chama hicho na kujiunga na CCM

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Makamu Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara), Leticia Mosore leo Ijumaa Julai 13, 2018 ametangaza kujiunga na CCM

Amejiunga pamoja na wanachama wengine watano, akiwemo aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho, Mchata Mchata

Amesema "Kinachonikera kwenye upinzani ni kupinga kila kitu hadi mazuri wakati hayo ndio tulikua tunayasema, mpaka mwisho hatueleweki tunataka nini, Hivyo mtu mzima kama mimi nimeona bora nirud CCM"

"Niliamua kuhama CCM sababu utekelezaji wa ilani haukuwa wa kuridhisha, rushwa na ukosefu wa maadili vilikithiri. Upinzani wa wakati huo walisimamia hoja hizi, zilinigusa nikashawishika kuungana nao ili tunusuru nchi".

IMG_20180713_114550.jpg
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa chadema.
Walimwingiza chaka Mbatia kwa kuuza chama chake kwa Lowasa.
 
Tanzania hamna UPINZANI na Umma umeshalitambua hilo. Kwahiyo siku wananchi wakitaka Mabadiliko yatafanywa bila msaada wa Mpinzani yeyote na hamtaamini. Hili taifa ni la Mungu. sio genge/familia ya mtu.
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa chadema baada ya kumshawishi Mbatia auze chama kwa Lowasa.
 
Njaa tu usijikoshe hapa, wanasimamia ilani gani kama si kujipendekeza tu, watu wana njaa, wana shida, hawana hela halafu huyu mwanamke huyu anakuja na ulopofu huu
 
Back
Top Bottom