DAR: Mahujaji 100 waachwa solemba Airport, Sheikh Mkuu aiwakia kampuni iliyowatapeli

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum amesema taasisi iliyokusanya fedha kwa waumini wapatao 100 na kushindwa kuwasafirisha kwenda hija, isakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tangu Agosti 23, waumini hao wamekwama Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya taasisi hiyo (jina linahifadhiwa kwa sasa) kuchukua hadi Sh10 milioni kutoka kwa kila hujaji, lakini ikashindwa kufanikisha safari hiyo.

Sheikh Salum alisema jana kuwa kuna haja kwa wahusika wa taasisi hiyo kusakwa, kukamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa kuwa licha ya kuwatapeli mahujaji hao, imesababisha washindwe kutimiza azma yao ya kufanya ibada hiyo.

“Zipo taasisi zenye tabia ya kuwatapeli waumini na hii si mara ya kwanza. Niwape faraja mahujaji waliokwama kwamba kama mwaka huu hawajasafiri labda Mwenyezi Mungu alipanga wasafiri mwaka ujao. Cha msingi ni kuwa makini na kampuni za aina hii,” alisema.

“Kuna waumini wengine wamezuiwa kuingia Saudi Arabia kwa sababu taasisi zilizowasafirisha nazo hazina vibali vya kuingia huko. Sasa ni kwa nini wasafirishe watu wakati wanajua wazi kwamba hawajatimiza vigezo?”

Baadhi ya waumini waliokwama kusafiri wameiomba Serikali kuingilia kati ili warejeshewe fedha zao. Walisema mpaka jana jioni hawakuwa na taarifa zozote kuhusu safari yao, wakati fedha zote walishailipa taasisi hiyo yenye ofisi zake Kariakoo jijini hapa.

Mmoja wa watu waliokuwa wasafiri, Ummy Sekibo alisema licha ya jitihada za kutoa taarifa kwenye taasisi za kidini, vyombo vya habari na Jeshi la Polisi bado wameshindwa kuondoka.

“Hakuna matumaini tena kama taasisi hii inaweza kutusafirisha, maana tangu Agosti 23 tumeganda hapa na hatujui tufanye nini,” alisema Sekibo.
Ummy alisema kwa sababu lengo lake lilikuwa ni ibada, ameanza mchakato wa kutafuta fedha nyingine haraka ili aweze kusafiri huku akiendelea kushughulikia fedha zake ‘alizotapeliwa.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Rajab Tendwa, alisema kila muumini amelipa fedha kulingana na makubaliano na taasisi hiyo. Walilipa kati ya Sh8.5 milioni hadi Sh10 milioni.

FullSizeRender_10.jpg
FullSizeRender_6.jpg
FullSizeRender_2.jpg
FullSizeRender_4.jpg
 
Sio Mara ya kwanza kwa mahujaji kutapeliwa, na hao bakwata hawana la maana wanalolifanya kwani haiwezekani haya mambo yanajiridia rudia na wameshindwa kutumia akili na kutafuta njia nzuri ya kuwapatia usafiri wa uhakika.
Au nao wamo
Bakwata wapo kisiasa zaidi,
Pale kwao wana vitengo vya kutosha tu ila vimekaa kii upigaji upigaji tu.
 
Bakwata wapo kisiasa zaidi,
Pale kwao wana vitengo vya kutosha tu ila vimekaa kii upigaji upigaji tu.
Ndio nikasema wamo nao katika utapeli huo.
Watu siku hizi hawataki kufuata maadili wanaona uongo dhulma na utapeli ndio way of life
 
Wakulaumiwa ni BAKWATA, kwanini wasiratibu wao safari ya waumini wao?

Taasisi za kusafirisha mahujaji zipo nyingi na kila taasisi ina sifa yake jinsi ya kuhudumia mahujaji wake ikiwemo na hiyo BAKWATA pia, sasa huduma za BAKWATA ndizo zinafanya watu watafute taasisi nyingine ambazo zitajali wateja. Kuna taasisi moja ipo mkabala na msikiti wamanyema inaitwa huduma,(nimetafsiri jina lake hapo ili kukwepa kuitaja nisipigwe ban) kwa kweli hautajuta.
 
Taasisi za kusafirisha mahujaji zipo nyingi na kila taasisi ina sifa yake jinsi ya kuhudumia mahujaji wake ikiwemo na hiyo BAKWATA pia, sasa huduma za BAKWATA ndizo zinafanya watu watafute taasisi nyingine ambazo zitajali wateja. Kuna taasisi moja ipo mkabala na msikiti wamanyema inaitwa huduma,(nimetafsiri jina lake hapo ili kukwepa kuitaja nisipigwe ban) kwa kweli hautajuta.
BAKWATA inatakiwa ivunjwe
 
Back
Top Bottom