Dar: Mahakama ya Kisutu imewafunga maisha, watu nane waliochoma kituo cha Polisi Bunju A mwaka 2015

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,399
2,000
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu nane kutumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi Bunju A, jijini Dar es Salaam.

Kati ya washtakiwa nane wamo wanafunzi wawili.

Habari zaidi, soma=>Ajali ya gari Bunju, wananchi wachoma Kituo cha Polisi - JamiiForums

======

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha maisha jela washitakiwa wanane baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A jijini Dar es Salaam huku wengine 10 wakiachiwa huru.

Jumla ya washitakiwa katika kesi hiyo walikuwa 35, awali Mahakama ilikwishawaachia huru 17 na kubaki 18 ambapo wanane ndio wametiwa hatiani leo Ijumaa Februari 23, 2019 huku 10 wakiachiwa huru.

Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa sita ikiwemo kuchoma kituo hicho moto Julai 10 mwaka 2015.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema kitendo walichofanya washitakiwa ni unyama kwa kuchoma moto kituo hicho.

"Kitendo hiki ni cha kinyama, hakiwezi kuvumilika na sioni sababu ya kuwaonea huruma kwa kuwa walihatarisha usalama wa nchi," amesema Simba.

Chanzo: Mwananchi
 

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,571
2,000
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hukumu hiyo baada ya kuwakuta na hatia ya kuchoma Kituo cha Polisi Bunju A Jijini Dar es Salaam

Kati ya Waliohukumiwa wamo Wanafunzi wawili ambapo mmoja amefahamika kwa jina la Halifani Mshengeli mwenye umri wa miaka 19
 

zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
6,614
2,000
upumbavu tu, yule malkia kahujumu nchi tangu miaka ya 90 hajafungwa maisha hawa wa kuchoma kituo ukawafunge maisha kam si upunguani ni nini?

hakimu wa namna hii ni wa kulogwa tu pumbavu sana hawa wangepigwa faini milioni moja moja kituo kijengwe upya kwisha kazi.
 

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Feb 19, 2018
3,734
2,000
Kituo ni nyumba na wanakaa watu mule. Ukichoma moto maana yake ni kuhatarisha maisha ya hao watu wakiwemo mahabusu ambao kama jitihada za kuwatoa zinachelewa wangefia humo humo.
Wamepata walichostahili
upumbavu tu, yule malkia kahujumu nchi tangu miaka ya 90 hajafungwa maisha hawa wa kuchoma kituo ukawafunge maisha kam si upunguani ni nini?

hakimu wa namna hii ni wa kulogwa tu pumbavu sana hawa wangepigwa faini milioni moja moja kituo kijengwe upya kwisha kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Feb 19, 2018
3,734
2,000
Baada ya hukumu kusomwa...
Kweli jela isikie kwa jirani tu.
IMG-20190222-WA0023.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom