DAR: Mahakama Kuu yatupilia mbali maombi ya wabunge Viti Maalum 8 wa CUF

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
wabunge+cuf.jpg





Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya waliokuwa wabunge wa viti maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), waliokuwa wakipinga kuapishwa kwa wabunge wateule.

Wabunge hao walifungua maombi hayo wakiiomba mahakama itoe amri ya zuio kwa Bunge, lisiwaapishe wabunge hao wateule, hadi pale kesi yao ya msingi kupinga kufutwa uanachama wa CUF itakapotolewa hukumu.

Hata hivyo, Mahakama Kuu imeyatupilia mbali maombi hayo, baada ya kukubaliana na hoja za mapingamizi zilizowasilishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia jopo la mawakili wanane wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata, na wakili wa Bodi ya Wadhamini CUF pamoja na wabunge wateule, Mashaka Ngole.

Malata anawawakilisha Katibu wa Bunge na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
 
Kwa tafsiri yangu kwa hili lina ashiria kabisa ya kuwa Pro Lipumba yupo madarakani kihalali....

Ina maana kipindi wakati Lipumba anajiudhuru nafasi yake ya mwenyekiti Cuf hawakupeleka taarifa kwa msajiri wa vyama vya siasa. Na ndiyo mana Lipumba ana anajulikana kama bado nibmwenyekiti halali wa CUF.....


Ngoja tuone Jipya litakalo Kuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom