Dar: Maduka ya kubadilishia fedha za kigeni(Forex) jana yalivamiwa Polisi, mengine yafungwa

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
Tukiwa na msiba mkubwa wa kitaifa kwa ndugu yetu Ruge jana kulitokea tukio kubwa sana ila halijaonekana kwa vile Ruge alikua mkubwa zaid. naam nalo ni bunduki kujaribu kuokoa shiling yetu izidi kuwa imara.

Katika harakati za kuokoa shiling yetu izidi kuwa imara dhidi ya pesa za kigeni, jana serikali iliendelea na kale ka utaratibu kake ka kuvamia maduka ya kubadilishia pesa za kigeni ili kuhakikisha pesa yetu inazidi kuwa juu.

Jana maduka hayo ya kubadilishia dollars yalivaniwa na wale wazee wasiotaka mjadala walihakikisha wanaondoka na kila kitu dukani kwako kuanzia camera za ulinzi mpaka na pesa zako. Wanajua wao wanaoenda kuziweka wapi hizo dollar ili shiling izidi kuwa imara.

IMG-20190228-WA0011.jpg

IMG-20190228-WA0012.jpg

1D905793-3C50-454C-BA03-2FCFA8A4ED3E.jpeg


Bado hatujaridhika au hatuoni sababu za kuhakikisha dollar moja japo iwe 1,000. Na nawaambia soon tutafika 3,000 kwa kasi hii ya kuvamia maduka lazima sh iwe juu.

Wale wazee wa kusifu na kuabudu utawala huu tuzidi kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kuvamia maduka kwa kudhani ndio mwarobain ili shiling yetu izid kuwa imara. Huenda mwezi wa tatu ikawa 2,500. Safi sana serikali.

Kwa wale wanaolipwa dollar watafurahia sana awamu hii maana wanalipwa vikaratasi vichache ila baadaye wanaondoka na fuko la shilingi.

Habari zaidi, soma=>Arusha: Maduka yote ya kubadilishia fedha za kigeni(Forex) yasimamiwa na JWTZ, wananchi watakiwa kwenda Benki Kuu - JamiiForums


==========
TAARIFA YA BENKI KUU (BOT)


IMG_20190228_161717.jpg
 
Back
Top Bottom