Dar kuwa ngome ya upinzani baada ya uchaguzi mkuu 2015

tufe

JF-Expert Member
Apr 24, 2015
750
290
Habari kwenu wanajukwaa,

Katika nchi nyingi hususani katika bara la Africa ambazo zimebadilisha utawala kutoka chama tawala kwenda chama cha upinzani basi vuguvugu la mabadiliko hayo huwa yameanzia katika miji mikuu ya nchi hizo kuelekea vijijini mfano Zambia yalianzia Lusaka kuelekea vijijini,Malawi yalianzia Blantyre kuelekea vijijini,Kenya yalianzia Nairobi kuelekea vijijini. Lakini hali ni tofauti kwa Tanzania.

Nchini Tanzania vuguvugu la mabadiliko limejikita zaidi katika miji ya kati kama vile ARUSHA CITY,MBEYA CITY,MWANZA CITY,MOSHI CITY,IRINGA URBAN pamoja na miji midogo midogo kama vile Tunduma,kilwa,shirati,kyela,geita na semi urban nyingi tu.

Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hali ni tofauti kwa Dar kwani Dar nayo sasa imeamka tena ina kiu ya mabadiliko.

Kiu hii ya mabadiliko imesababishwa sana na UFANISI na WELEDI mkubwa wa kazi za kibunge ulioneshwa na wabunge wawili tu kutoka upinzani Ndugu JOHN JOHN MNYIKA WA UBUNGI na Ndugu HALIM JAMES MDEE WA KAWE kwani wao hawakuwa wawakilishi wa majimbo yao tuu,Bali walikuwa wawakilishi wa mkoa mzima wa Dar es salaam.

Kitendo cha wabunge hawa kuisimamia na kuinyoosha serikali vizuri kumewaamsha watu wa Dar na wameona na kufahamu faida ya kuchagua wabunge wa upinzani. Kwa hivyo katika utafiti wangu nimegundua kati ya majimbo 11 yaliyopo Dar,majimbo yafuatayo yatangukia katika kapu la upinzani kama Muungano wa UKAWA UTADUMU:

1) KIBAMBA(CHADEMA) jimbo hili ni jeupe kabisa na upinzani kushinda ni 90%.

2) UBUNGO(CHADEMA) jimbo hili pia ni jeupe kwa upinzani na wana 80%

3) KAWE(CHADEMA) Jimbo lipo wazi kwa upinzani chini ya mwanamama jasiri HALIMA MDEE na wana 90%.

4)SEGEREA(UKAWA) jimbo lipo salama kwa upinzani chini ya UKAWA na wana 70%.

5) MBAGALA(CUF/UKAWA) jimbo lipo salama kwa upinzani chini ya UKAWA wana 60%.

6)UKONGA(CHADEMA/UKAWA) jimbo lipo salama kabisa chini ya ukawa na wako na 60%

7) KIGAMBONI(CUF/UKAWA) 57%

8) TEMEKE(UKAWA)55%

9) KINONDONI(UKAWA)55%

Ahsanteni sana.
 
Faustin Ndungulile angejitafakari akajiunga na CHADEMA

Pale CCM lazima atapigwa mizengwe...Watampitisha Dotto Diwani wa Feri
 
Mbona thread moja mnaigeuza kwa kujifanya wajuaji! mmesha toa kama hii sasa mnatakaje tuchangie vp huku na kule!!
 
Kutokana na ugumu wa maisha unavyowapiga wanadarsalama ninasema tena kwa kujiamini kabisa yakwamba pamoja na hila zote wanazofanya ccm hivi sasa lakini 2020 hawatapata jimbo hata moja ndani ya Dar,hata moja!! TUOMBENI UHAI TU!!
 
tatizo nyie vijana wa ufipa mnaongea sana ili hali mnajua haiwezekani jifunzeni kuwa na akiba ya maneno si ata 2015 Dj. wenu alihubili kuwa wanachukua nchi saa 4 ili hali akijua haiwezekani by the way jifarijini tu make hamna namuna
 
Back
Top Bottom