DAR: Kiwanda chafungiwa na NEMC

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Baraza la Taifa la usimamizi na hifadhi ya mazingira NEMC limefunga kiwanda cha Unga na nafaka cha Twenty 21 First Centuary kilichopo Sinza Dar es Salaam sambamba na kutozwa faini ya shilingi milioni 35.

Baraza hilo limefikia maamuzi hayo sababu kiwanda hicho kimejiendesha kwa zaidi ya miaka kumi bila cheti cha tathimini ya athari ya mazingira kinyume cha sheria huku kikimwaga vumbi kali kwenye makazi ya watu.
 
Viwanda vya sampuli hiyo viwe mbali na makazi ya watu.Sinza yasemekana ni eneo lilopimwa na serikali kama makazi ya binadamu,sasa inakuwaje kijengwe kiwanda kipewe leseni na kufanya kazi miaka 10?Kumbe Tanzania kutunga sheria sio kusimamia sheria.Porojo nyingi
 
Iko kiwanda kidogo,sasa serikali haijatenga maeneo kwa viwanda vidogo vidogo,nahisi ata iyo faini aliyoambiwa alipe milioni 35 ndio mtaji+machine
 
TATIZO NCHI HAINA MPANGILUO WA VUWANDA MBONA CHINA KILA JIMBO LINA VIWANDA VYA HAINA FULANI HATA NASI TWAWEZA ILA LUSHWA ILITAWALA MAISHA
 
Sera ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda na yenye Uchumi wa Kati ifikiaka 2020 ni jambo jema sana. Lakini mchakato huo unatakiwa ufanywe kwa umakini mkubwa ila usikizane na Sera na mikakati mingine ambayo nayo ni ya manufaa kwa Watanzania kwa ujumla wao. Wawekezaji kwenye sekta ya Viwanda wasegeuke miungu watu ambao wako juu ya sheria na kuwa wasiogusika na sheria za nchi.
Kuna Viwanda vingi havifuati wala kutii mashart kama yq baraza la Taifa la Mazingira- NEMC wala hawafanyi ukaguzi wa EIA na kupata vyeti. Uchafuzi wa mazingira upo juu sana na kwa ujumla hakuna public economic benefits zaidi ya maslahi binafsi kwani madhara kwa umma ni mkubwa kuliko faida. Hivyo kila jambo lifanywe kwa maslahi mapana ya nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom