Dar, Kilimanjaro zatajwa kuongoza kwa utapiamlo

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
10,303
8,251
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetaja mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro kuwa vinara wa utapiamlo wa lishe iliyozidi nchini.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TFNC, Geofrey Chiduo amesema hayo leo Jumanne Machi 19, 2019 jijini Dodoma wakati akizungumzia namna huduma za lishe zinavyoendelea nchini.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, baadhi ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wadau wa lishe.

Chiduo amesema kwa sasa wanapambana na maadui wawili ambao ni utapiamlo wa hali duni ya ukosefu wa virutubisho lakini kuna utapiamlo wa lishe uliopitiliza.

“Naomba nilitamke rasmi hapa kwa kuwa viongozi hapa mpo kwenye mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro, suala la utapiamlo wa lishe iliyozidi wao ndio vinara,” amesema.

Amesema hata katika mikoa ambayo uzalishaji uko juu bado hali ya utapiamlo ipo juu na viwango katika mikoa vinatofautiana.

“Hata katika mikoa ambayo uzalishaji wa chakula ni mkubwa utapiamlo upo kiwango cha juu sana, hakuna aliyesalama,” amesema.
=======

#NB* Wana Kilimanjaro tupunguze lishe maana imezidi hii ni kutokana na neema ya vyakula na Hali nzuri ya kiuchumi mkoani Kilimanjaro ikizingatiwa kuwa 86% ya Wana Kilimanjaro wanaishi maisha Bora kwa mujibu wa nbs
Cc
FisadiKuu
fazili
Frank Wanjiru
Sky Eclat
The only

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi taarifa zinapingana na zile za hapo awali ambapo tuliambiwa Kilimanjaro inaongoza kwa utapiamlo. Sababu zilizotolewa ni kwamba wazazi hushinda kwenye baa wakila nyamachoma na kitimoto wakiwaacha watoto wao wakishinda njaa na kuishia kuwa na unyafuzi na utapiamlo. Nyakati hizo miradi ya lishe ilipelekwa huko Kilimanjaro. Sasa tunauliza haya mambo yakoje?
 
Wakuu salaam
kwA mujibu wa utafiti wa shirika la chakula na lishe ,mikoa ya Kilimanjaro na dar inaongoza watu wake kula lishe kupita kiasi (obesity)
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa mkurugenzi wa shirika Hilo bw chiduo
Chanzo: Mwananchi
#NB* Wana Kilimanjaro tupunguze lishe maana imezidi hii ni kutokana na neema ya vyakula na Hali nzuri ya kiuchumi mkoani Kilimanjaro ikizingatiwa kuwa 86% ya Wana Kilimanjaro wanaishi maisha Bora kwa mujibu wa nbs
Cc
FisadiKuu
fazili
Frank Wanjiru
Sky Eclat
The onlyView attachment 1049157

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu weka hii habari yote. Niliisoma nikashangaa sana. Ina maana Kilimanjaro na Dsm kuna shida ya obesity. Watu wanakula mno. Aisee mangi pigeni kitimoto ila na mazoezi mkumbuke hata muwe mnaenda Kilimarathon😀😀
 
Hizi taarifa zinapingana na zile za hapo awali ambapo tuliambiwa Kilimanjaro inaongoza kwa utapiamlo. Sababu zilizotolewa ni kwamba wazazi hushinda kwenye baa wakila nyamachoma na kitimoto wakiwaacha watoto wao wakishinda njaa na kuishia kuwa na unyafuzi na utapiamlo. Nyakati hizo miradi ya lishe ilipelekwa huko Kilimanjaro. Sasa tunauliza haya mambo yakoje?
Yap Kilimanjaro inaongoza Kwa utapiamulo mtoa mada ndo kaelewa vibaya
Screenshot_20190319-211110.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetaja mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro kuwa vinara wa utapiamlo wa lishe iliyozidi nchini.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TFNC, Geofrey Chiduo amesema hayo leo Jumanne Machi 19, 2019 jijini Dodoma wakati akizungumzia namna huduma za lishe zinavyoendelea nchini.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, baadhi ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wadau wa lishe.

Chiduo amesema kwa sasa wanapambana na maadui wawili ambao ni utapiamlo wa hali duni ya ukosefu wa virutubisho lakini kuna utapiamlo wa lishe uliopitiliza.

“Naomba nilitamke rasmi hapa kwa kuwa viongozi hapa mpo kwenye mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro, suala la utapiamlo wa lishe iliyozidi wao ndio vinara,” amesema.

Amesema hata katika mikoa ambayo uzalishaji uko juu bado hali ya utapiamlo ipo juu na viwango katika mikoa vinatofautiana.

“Hata katika mikoa ambayo uzalishaji wa chakula ni mkubwa utapiamlo upo kiwango cha juu sana, hakuna aliyesalama,” amesema.
=======

#NB* Wana Kilimanjaro tupunguze lishe maana imezidi hii ni kutokana na neema ya vyakula na Hali nzuri ya kiuchumi mkoani Kilimanjaro ikizingatiwa kuwa 86% ya Wana Kilimanjaro wanaishi maisha Bora kwa mujibu wa nbs
Cc
FisadiKuu
fazili
Frank Wanjiru
Sky Eclat
The only

Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi zilizoendelea huwa zinakuwa na magonjwa yake mfano kansa ipo kwa wingi Ulaya kuliko Afrika. Ni magonjwa ya matajiri. Ukiona Kilimanjaro na Dar basi kuna namna fulani inahusiana na hali ya juu ya uchumi. Ingetajwa Kilimanjaro na Mtwara, Kigoma au Kilimanjaro na mkoa mwingine maskini kama Kagera basi ingekuwa tatizo ni umaskini.
 
Kwa hiyo mnaona fahari kuwa na utapiamulo?

Aiseee sijui Rweye na Britannica kama watakuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom