Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 51,985
- 69,375
Hili joto limeanza kuchangamkaWana Dar wenzangu, mji wetu msimu wa joto kali umeanza rasmi.
Tujiandae kisaikolojia maana joto linaanza kushika hatamu hapa ni mpaka mwezi wa sita mwaka 2021 ndo tutaanza kupumua tena kwa kaubaridi.
Joto limeanza rasmi tujiandae kuungua kwa joto; najionea huruma
Ambao mliuza feni na viyoyozi shughuli mnayo.
Wale wa nyumba za kupanga na Luku za kushindana mjiandae.
Tanesco mtuonee huruma msikate umeme maana bila umeme hizi feni na AC ndo tegemeo letu tutakwisha.