Dar: Jamaa adaiwa kumuua mpenzi wake kisha naye kujiua kwa kunywa sumu, vidonge na pombe

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Bunaza Doto Manyanda (34) anadaiwa kumuua mpenzi wake, Happiness Mzalile Zakaria (23) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni kisha naye kujiua, marehemu wote wakiwa ni Wakazi wa Charambe kwa Mbiku Wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Juni 8, 2022 ambapo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Muliro Jumanne amesema baada ya mauaji, ndipo Bunaza akaamua kujiua kwa kunywa dawa ya kuulia wadudu wa mazao ya DUDU CRON, vidonge vya flagyl na kuchanganya na pombe.

“Bado tunachunguza chanzo, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” - anasema Muliro.
 
Hakuna kosa lolote LA kimapenzi linakuhalalisha kuua,japo inauma sana ila usimuue sababu hakuna jipya la kimapenzi ambalo kalifanya yote yashafanyika.

Sometimes watu tunaogopa kuface insecurities za kimapenzi unajiona huna thamani kama unayempenda hakupendi Tena,inawaza utapata wapi kama huyu,unawaza mbona kabadilika na mwanzoni mapenzi yalikua motomoto,na kama umefulia unawaza au sababu Sina pesa?

Kila unavoendelea kuwaza ndio unazidi kupata sababu na hasira ya kumfanyia kitu kibaya, relationships are not meant to be forever wadau.
 
Bunaza Doto Manyanda (34) anadaiwa kumuua mpenzi wake, Happiness Mzalile Zakaria (23) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni kisha naye kujiua, marehemu wote wakiwa ni Wakazi wa Charambe kwa Mbiku Wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Juni 8, 2022 ambapo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Muliro Jumanne amesema baada ya mauaji, ndipo Bunaza akaamua kujiua kwa kunywa dawa ya kuulia wadudu wa mazao ya DUDU CRON, vidonge vya flagyl na kuchanganya na pombe.

“Bado tunachunguza chanzo, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” - anasema Muliro.
BUNAZA DOTO MANYANDA.
"The same shit but with different toilet pit"
 
Back
Top Bottom