Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 724
- 245
Wengi tunakubaliana kuwa Dar inakabiliwa na changamoto nyingi za mji. Ukosefu wa huduma na miundombinu muhimu ya taka ngumu na maji taka; usafiri; bustani na viwanja vya michezo; ujenzi holela; ukosefu wa maeneo ya makaburi na changamoto nyingine kadha wa kadha.
Baadhi yetu tunaunga mkono jitihada za serikali na hasa za hivi karibuni za RC Paul Makonda kutaka kuwa na jiji lenye mpangilio na ustaarabu. Hata hivyo, ndoto ya Makonda ya "Dar Mpya" inahitaji kujengwa au kusimikwa kwenye Mpango Kabambe (Master Plan).
Itapendeza kama Ukawa kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa na sisi wadau wengine sote tutahakikisha tunakuwa na Mpango Kabambe wa jiji. Vinginevyo hatutafanikiwa kuwa na Dar inayovutia na yenye ustaarabu.