Dar: Hii mvua mbona siielewi, tangu asubuhi inanyesha tu

kuna muda hata wao wanashindwa watabiri vipi, wakisema mvua itanyesha kwa siku 3 siku hiyo hiyo inakata kunyesha, wakisema mwezi wa 5 hakutakuwa na mvua basi mwezi wote huo mvua zitanyesha mfululizo.
 
Nipo kwa bedi na mtoto mbichi.tunapumzika mpaka sasa tatu mbil
 
Kuanzia majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo may 5, mvua inanyesha bila kukoma na ikisimama basi si zaid ya masaa mawili inamwagika tena, yaan dar es salaam sasa hivi joto linatafutwa lilipo. Yaani imekuwa ni mwendo wa manyunyu na mvua kwa kwenda mbele, nimekatiza maeneo kadhaa ya biashara hasa kwa wale wenzetu akina machinga ni wameghafirika vibaya juu ya usheshaji wa hii mvua unaopelekea kukosa vipato vyao vya kila siku.

Baadhi ya sehem nikasikia minong'ono kuwa hii mvua ni majibu ya ile dua ilofanyika pale mnazi mmoja juu ya kuomba mvua inyeshe, na sasa inanyesha jiji zima bila shaka hata baadhi ya mikoa mingine itakuwa inanyesha.

Tahadhari kwa waishio mabondeni wawe makini na wasicheze mbali na makazi yao kwani lolote laweza kutokea
aisee msalimie sana paul kinyozi hapo kidamali na geoge flyiakus waambie bwn,kura mayii a.ka mzee wa povu nawapa hi!
 
Toka asubuhi mpaka mida hii huku Mbezi luis hakuna kutoka ndani ni maji tu yanamwagika,sijui ni hapa tu au na kwingine nako inanyesha .
Ya kutoa mwezi. Ni kawaida mwezi unapobadilika hali ya hewa lazima I change. Fanya utafiti
 
Nashangaa hizi mvua zinazonyesha mfululizo Dar tangua jana saa mbili usiku na maeneo mengine kuanzia saa nane usku, mamlaka ya hali ya hewa Tz haikutoa tahadhari youote.

TMA lazima waelewe kwamba kwa daslam mvua za kunyesha mfulilizo zinapelek a ardhi kujaa maji na hivyo mafuriko yanayoweza kuleta maafa makubwa.

Kimbunga Cha Kenneth mlipiga kelele Sana au ilikuwa pest and copy kutoka luninga za ulaya?

Dizaini TMA hamna uhakika na tabiri zenu. Mvua hizi ilipaswa zitolewe tahadhari hususani usiku wa Leo endapo zitaendelea kunyesha
Ndiyo maana xa utabiri mkuu
 
Yaani hatukosi maneno
Kwani mwaka jana iliponyesha waliomba pia?
Hapa naona mpambane na kuzibua mifereji ya vinyesi tu maana drainage systems za huko ni mbaya sana kwa ajili ya uchafu
 
Back
Top Bottom