Dar: Grace Mushi ambaye alimchomea ndani Mpenzi wake, akamatwa na Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,745
11,869
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA ALIYEMCHOMA MOTO MPENZI WAKE NDANI YA NYUMBA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Grace Janes Mushi (25) kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Khamis Abdallah (25).

Tukio hilo limetokea tarehe 16.07.2021 majira ya saa nane na nusu usiku huko maeneo ya Mbezi Makabe kwa Mzungu Wilaya ya Ubungo.

Mtuhumiwa Grace majira hayo ya saa nane usiku aliamka na kumfungia mlango kwa nje Khamis Abdallah kisha kumwagia mafuta ya petroli nyumba hiyo, kitendo kilichopelekea Khamisi kuungua na kufariki dunia akiwa ndani.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kimapenzi.

Imetolewa na :-
MULIRO J.MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI,
KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM

Pia soma > Dar: Amchoma mumewe na Petroli kisa wivu wa mapenzi
 
Kuna jamaa alimchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa.

Tukiambiwa kisasi cha mwanamke ni funga kazi tuelewe.

A sane person will commit a crime huku ana plan ya kutojulikana just like anko wa magunia mawili but this lady? She just burnt the whole house with zero fvcks on getting caught.
 
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA ALIYEMCHOMA MOTO MPENZI WAKE NDANI YA NYUMBA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Grace Janes Mushi (25) kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Khamis Abdallah (25)...
Huyo mwanamke mpumbavu kweli yaani unaua kisa wivu utafkiri aliolewa akiwa bikra kumbe mzigo ndaza
 
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA ALIYEMCHOMA MOTO MPENZI WAKE NDANI YA NYUMBA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Grace Janes Mushi (25) kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Khamis Abdallah (25)...

Wote wana miaka 25, watoto, Hakuna wa kuongoza mwenzake, haya ndo matokeo!
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom