Dar: Gari dogo lateketea kwa moto daraja la Nyerere Kigamboni

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
Gari dogo limeshika moto ghafla, wakati dereva akikata tiketi katika Daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam asubuhi hii.

MY TAKE:

Ile Ofisi ya zimamoto inafanya nini pale? Muda wotenimefungwa. Ipo siku tutakuta daraja letu limeteketea lote.

Mbaya zaidi wale askari wa pale wameacha kufanya kazi za usalama, wanahangaika na watu wa mikoani wanoenda kupiga picha za kumbukumbu darajani.

Wanajificha kichani kunyemelea wanaojipiga selfie na wakikukamata unalipa elfu 50 wala hupewi risiti. Sasa ona gari ilivyoteketea na wao wapo.

IMG_20180702_080651.jpeg
IMG_20180702_080701.jpeg

=======

Moto umewaka na kuteketeza gari aina ya Toyota Ractics maeneno ya daraja la mwalimu julius nyerere lililopo wilaya ya kigamboni ambayo usajili wake haukufahamika mapema na kwa taarifa tulizozipata hakuna majeruhi katika tukio hilo, mwenye gari alifanikiwa kutoka nje ya gari na kukimbilia sehem salama..

Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme wa gari hiyo pindi limefika kwenye kukata ticket hitilafu hiyo imetoka na kuanza kuungua, juhudi za kuliokua gari hilo zilifanyika na kufanikiwa kuuzima moto huo hali likiwa limeshaungua mbele.

Juhudi za kuwapata viongozi wa usalama wa daraja hilo ili kuweza kuliongelea swala hilo ziligonga mwamba baada ya mwanahabari wetu kupenya huku na kule bila mafanikio yoyote.

Jitihada za kupiga picha pia ziligonga mwamba na kisababisha Mwandishi wetu Kuondolewa na askari wa eneo hilo kwa Madai kuwa hakuruhusiwi kipigwa picha eneo hilo

Chanzo: Muungwana
 
Hivi kwa gari namba B spacio old model wanakubali kukata bima kwa comprehensive?
 
Ile Ofisi ya zimamoto inafanya nini pale? Muda wotenimefungwa. Ipo siku tutakuta daraja letu limeteketea lote.

Mbaya zaidi wale askari wa pale wameacha kufanya kazi za usalama

Hizi kazi za moto wangeachiwa SUMA JKT maana hilo jeshi husika ni kama lipolipo tu, rejea uokozi wa mtoto aliyefia kwenye dimbwi mlimani city, hicho kikosi kilishindwa kazi, aliyefanya uopoaji wa mwili alikuwa raia na wao wakiwepo wameshika magongo
 
Ofisi za Jamaa wa Zimamoto si wako kama mita 10 tu na hapo???.
Hatujajipanga kweli.
 
Hizi kazi za moto wangeachiwa SUMA JKT maana hilo jeshi husika ni kama lipolipo tu, rejea uokozi wa mtoto aliyefia kwenye dimbwi mlimani city, hicho kikosi kilishindwa kazi, aliyefanya uopoaji wa mwili alikuwa raia na wao wakiwepo wameshika magongo

Nadhani wengi wao watakuwa ni watoto wamezaliwa na kukulia Maghorofani kwa hiyo maisha halisi hawayajui.
 
Hizi kazi za moto wangeachiwa SUMA JKT maana hilo jeshi husika ni kama lipolipo tu, rejea uokozi wa mtoto aliyefia kwenye dimbwi mlimani city, hicho kikosi kilishindwa kazi, aliyefanya uopoaji wa mwili alikuwa raia na wao wakiwepo wameshika magongo
Mkuu hilo jeshi la zimamoto halina vifaa vya kisasa kabisa, magari yote yale ya zimamoto ni tia maji tia maji tena niya msaada toka nchi za ujerumani na Japan

Jamaa kalipia tozo ya kuvuka gari iliyoungua
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom