Dar: Fundi Jokofu asakwa na Polisi kwa Kumuua Mke wake

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,137
Inasikitisha..

Wanaume wasiojiamini wanaendelea kuua wake zao

=====

Fundi jokofu asakwa tuhuma za kuua mke

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 396 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu, huku likimsaka fundi wa majokofu, Godbles Sawe (47), anayetuhumiwa kumuua mke wake.

Sawe, mkazi wa Kimara Suka mkoani Dar es Salaam, anatuhumiwa kumuua mke wake, Ester Gadau, kwa kumkata kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia umauti kisha kukimbia baada ya mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro, alibainisha hayo jana jijini humo wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akifafanua kuwa tukio hilo la mauaji lilitokea Jumanne ya wiki hii eneo la Kibamba wilayani Ubungo.

Kuhusu watuhumiwa 396, kamanda huyo alisema walikamatwa kupitia msako uliofanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja kilichoanzia Mei 15, mwaka huu hadi Juni 15, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.

Alisema msako huo ulikuwa na lengo la kuzuia na kukabiliana na vitendo vya kihalifu vikiwamo unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi wa magari na vipuri, wizi wa pikipiki, uvunjaji, dawa za kulevya na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Alisema katika tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, waliokamatwa ni Mohamed Bakari, maarufu Mremi, na wenzake 12 ambao wanatuhumiwa kupanga, kujihusisha na kutekeleza matukio mbalimbali yakiwamo ya kutumia silaha kama mapanga, nondo na visu.

Kamanda Muliro alisema kuwa kupitia falsafa ya ulinzi shirikishi, zimepatikana bastola mbili aina ya TAURUS Silver namba P-22 Cariba FL-22 LR iliyotengenezwa Miami nchini Marekani ikiwa na risasi mbili na ya pili ni aina ya Browning ikiwa na risasi 42.

Alisema kwa matukio ya uvunjaji, wamemkamata Omary Bwilani (34), mkazi wa Buza wilayani Temeke na wenzake 54 wakiwa na runinga nane zinazodaiwa kuwa ni za wizi zenye ukubwa tofauti.

“Watuhumiwa hao wamekutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jozi tatu, buti jozi moja na kofia moja. Vingine ni DVD player moja na fedha Sh. 300,000 zilizoibwa,” alisema.

Kamanda Muliro alisema katika msako huo wamewakamata watuhumiwa 15 wanaodaiwa kujihusisha na wizi wa magari na vipuri vyake.

“Tumewakuta na magari mawili, moja lenye namba za usajili T 617 DRU aina ya Suzuki Carry na lingine Toyota Wish jeusi ambalo limefutwa namba za usajili na kubadilishwa rangi kuwa jeupe, tumewakuta na vipuri mbalimbali vya magari na pikipiki.

“Vifaa walivyokutwa navyo ni mlango wa gari aina ya Toyota Prado, side mirror 38 za magari mbalimbali, namba za magari 47, gear box moja ya Toyota Hilux, taa za mbele 21 za magari mbalimbali na za nyumba zipatazo 14.

“Rim sita size 15 za magari madogo, exhaust pipe moja ya gari, kadi 26 za usajili wa magari na injini tatu za pikipiki wamekutwa na leseni moja ya biashara inayodhaniwa kuwa ni ya kughushi pamoja na mkataba wa mauziano ya gari ambao nao unachunguzwa," alisema.

Pia alisema watuhumiwa hao walihojiwa ili waonyeshe magari ya namba walizokutwa na kwamba mifumo ya kisheria inafuatwa kushughulikia tukio hilo.

Kamanda Muliro alisema wamekamatwa watuhumiwa 206 wakiwa na dawa za kulevya za aina mbalimbali zikiwamo heroine gramu 93, bangi kilo 222 na gramu 109 na mirungi kilo 3.5 ambao tayari wamefikishwa mahakamani.

Pia alisema mtuhumiwa Fatuma Juma, mkazi wa Tumbwi, Kigamboni na wenzake 80 wanatuhumiwa kukamatwa na pombe haramu ya gongo na wameshafikishwa mahakamani.

Kamanda Muliro alisema Jeshi la Polisi limeweka mkazo wa kesi za ukatili wa kijinsia zipelekwe haraka na baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni Joshua Simangwe (66), mkazi wa Kipunguni Ukonga, anayetuhumiwa kuwalawiti wanafunzi watatu wenye umri wa chini ya miaka 18 wanaosoma huko Gongo la Mboto.

Alisema wanamshikilia Frank Barnabas kwa tuhuma za kujifanya askari na kufanya uhalifu wa kutapeli watu na kupita kwenye maduka, akidai anatafuta vipuri vya gari la polisi.

Alisema mtuhumiwa huyo amekuwa akishirikiana na mwenzake ambaye ni John Shija ambaye yeye anadaiwa kujifanya fundi wa magari ya polisi.

Chanzo: Nipashe
 
Hii nchi inamengi sana, Unaanzaje kumuua mpenzi wako? Kama amekuzingua si uachane nae tu, Sasa tizama maisha yake sasa
 
hii vita hatuwezi kuimaliza mpaka hawa kenge waache jeuri zao ndani ya nyumba na watutii sisi Waume zao
 

Attachments

  • 2ABEC313-CEAC-42DB-811F-F50812645C60.jpeg
    2ABEC313-CEAC-42DB-811F-F50812645C60.jpeg
    77.3 KB · Views: 16
Back
Top Bottom