Dar es salaam: Wanaume na supu ya pweza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar es salaam: Wanaume na supu ya pweza!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by vukani, Mar 20, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Hivi karibuni nilitoka kwenda kumtembelea rafiki yangu mmoja anayeishi maeneo ya Msasani. Eneo la Msasani ni eneo ambalo sijui nisemeje, lakini ni eneo ambalo linaishi watu wenye vipato tofauti tofauti, kuanzia wale wenye vipato vikubwa na wale wenye hali duni kabisa na maisha yanasonga mbele kama kawaida.

  Nilifika kwa rafiki yangu majira ya saa kumi jioni, kwani anaishi eneo ambalo lina pilikapilika nyingi sana. Nilipofika nilimkuta amekaa kibarazani kwao akijisiomea novel zake. Alinikaribisha kwa bashasha na tukaanza kukumbushana stori zetu za zamani na vituko tulivyokuwa tukivifanya enzi zetu za shule.

  Mnajua maisha ya shule huwa yana mambo mengi ya kukumbukwa maana ndipo mahali ambapo kuna kila aina ya ujinga, na werevu kidogo. Wakati tukiendelea kupiga soga, nilishangaa kuona kundi la wanaume wakiwemo wazee na vijana wakiwa wameizunguka meza upande wa pili wa barabara huku kila mmoja akiwa na kibakuli chake. Kulikuwa na vitu Fulani wanaokota juu ya meza na vijiti yaani tooth picks na kula huku wakiteremshia na kinywaji kilichopo ndani ya vibakuli vyao.

  Nilijishikwa na udadisi, ikabidi nimuulize shoga yangu, kuwa ni kitu gani kinaendelea pale, shoga yangu linijuza kuwa mahali pale ni maarufu kwa uuzwaji wa supu ya pweza. Shoga yangu hakuishia hapo aliendelea kubainisha kuwa supu ya pweza imeibuka na kuwa maarufu siku za hivi karibuni hususana kwa vijana kwa kuwa inasemekana kuwa inaongeza nguvu za kiume.

  Kwangu mimi hiyo ilikuwa ni habari mpya, nafahamu kuwa hapa jijini hasa maeneo ya Kariokoo ni kawaida kukuta vijana wakiwa wamebeba masinia yakiwa yamesheheni vipande vya pweza, ngisi na chachandu, wakitembeza mtaani, lakini hili la supu ya pweza sikulifahamu.

  Nilimuuliza shoga yangu kama ninaweza kwenda mahali pale ili kupata habari zaidi, shoga yangu huyu kwa bahati nzuri anajua kuwa mimi ni mdadisi, na hakusita kunitania, "He nawe, najua hapo ushapata umbeya wa kuweka mtandaoni"
  "Habari ndiyo hiyo shoga yangu hivi hapa nimeshapata udaku" nilimjibu.


  Tulivuka barabara na kufika mahali pale, "Shifeya, ( Sio jina lake halisi) tunaona umetuletea mgeni hapa, karibu dada" alitudaka yule kaka muuzaji wa supu. Tulipofika pale tulikuta anazo chupa za chai kubwa maarufu kama thermos chini ya meza yake, ambazo nilijulishwa na mwenyeji wangu kuwa ndizo anazotumia kuhifadhia supu hiyo ya pweza.

  Wale vijana na baadhi ya wazee tuliowakuta pale walionekana kufurahiya uwepo wetu pale na nilikaribishwa nijipatie vipande vya pweza na supu. Niliwashukuru kwa ukarimu wao na kuwaambia kuwa kwa bahati mbaya situmii pweza kwa kuwa nina mzio {Allergy} nao.


  Kama kawaida nilifanya udadisi wangu, kwa yule kijana muzaji wa supu, kutaka kujua sababu supu ile ya pweza kupata umaarufu siku hizi tofauti na zamani,

  "Unajua dada, supu ya pweza inafaida nyingi sana, kwanza ni kiburudisho, pili inaondoa uchovu, inachangamsha na pia…….si unajua yale mambo yetu yaleeee,"
  "Mambo gani sasa, mbona humalizii" nilifanya udadisi,
  "Weweee sasa unamficha nini kwani ni mtoto mdogo huyo?" alidakia kijana mwingine pembeni aliyekuwa na bakuli lake la supu. "Unajua sister supu ya pweza, pamoja na hizo faida alizokueleza, lakini faida kubwa kabisa ni kwamba inaongeza nguvu za kiume, yaani kama mwanaume anapata supu hii ya pweza halafu akutane na mwanamke, weee inakuwa ni shughuli pevu." Watu waliokuwa pale wote waliangua vicheko.

  "Mweleze huyo akamjulishe shemeji, maana kama hayajua mambo haya, basi akiyajua itakuwa kazi kweli kweli"
  "Tokeni zenu kule kwanza ninyi watu wa bara ndio mliosababisha mpaka pweza wamepanda bei siku hizi, kwani zamani pweza hakuwa ghali kiasi hiki lakini tangu mufahamu kuwa inafaa kwa majamboz, imekuwa taabu mpaka wamepanda bei" alisema mzee mmoja.

  Mara akadakia kijana mwingine, "Huo sasa ni uongo, pweza wamepanda bei kutokana na kuenea kwa mahoteli na mighahawa ya kitalii hapa jijini, na ndio maana wakapanda bei"
  Basi yalizuka malumbano mpaka nikashindwa nimsikilize nani na nimuache nani. Nilitoa ofa ya kuwanunulia chupa nzima ya chai iliyojaa supu ya pweza na kujiondokea zangu.

  Hata hivyo kupitia malumbano yao nilikuja kufahamu kuwa mpaka miaka ya tisini supu ya pweza haikuwa maarufu kiasi hiki, lakini kutokana na hiyo sifa ya kuongeza nguvu za kiume, imetokea kuwa maarufu miaka ya 2000 na kuwafanya pweza kuwa ghali.

  Yule kijana muuuza pweza alinijuza kuwa inamlazimu kwenda hadi Bagamoyo kuwafuatilia pweza kule, kwani hapa Ferry jijini Dar Pweza wamekuwa ni ghali mno kutokana na kupata umaarufu na pia kutokana na watu wa mahoteli na mighahawa ya kitalii kuwanunua kwa bei ya ghali.

  Kule Bgamoyo napo hawakuwa ghali sana, lakini siku za karibuni wamekuwa ghali sana kutokana na wafanyabiashara wengi wa supu ya pweza jijini Dar kukimbilia kule kuwatafuta.


  Sijafanya utafiti wa kina juu ya madai haya, hivyo msije mkaniuliza kama nina ushahidi na madai hayo.

  Kama yupo mwenye changamoto juu ya mada hii anakaribishwa kwani mimi ni msimuliwaji tu.

   
 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hadithi tamu sana, hongera mdada
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hahb yaelekea siku hizi wanaume wengi kitu kwenda angani bila msaada ni shida, kwa hiyo mpaka wapate vitu vya msaada ndo waweze ku perfom
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mmmh.! sasa mnatukashif
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hiyo ni kweli kwa baadhi ya watu ila wengine kitu kinaweza kwenda angani laini baada ya mzunguko mmoja tu kinakuwa hoi hadi kesho yake au wiki ijayo......... it is so terrrible...........

  wanawake nao pia wana sababu katika hili............ tangu wameanza kujilinganisha na wanaume, wamepunguza ego za wanaume na haya ni moja ya matokeo yake...........
   
 6. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hivi unajua nyie wanawake ndo mnatusababishia haya matatizo. Kwanini nyie kufika kileleni wakati wa shughuli inawachukua muda hivyo. Yaani mpaka mdada ubahatike kua na mkaka mjanja wa ma-foreplay na kujizungusha murua akiwa shughulini of which wanaume wachache sana siku hizi wanaweza hivyo bila influence ya vigra za kienyeji kama hiyo supu ya pweza, pombe nk.

  Yaani haya yote sijui ya supu ya pweza sijui valuu ni kwa ajili yenu nyie.

  Hebu kinadada mji-tune bwana. Mkiwa ktk mchezo wekeni mawazo yenu pale na si kwingineko. Naamini kufanya hivi kilele cha mlima mrefu tuupandao tutafika pamoja. Sio mnawatia hasara wanaume bwana. Yaani mwanaume wa siku hizi haingii gemuni mpaka ashtue na pombe?! Matokeo yake wakati wa mambo anakua kama analima badala ya ku-enjoy.

  Supu ya pweza bwana huenda kwa kua watu tushajenga imani hiyo basi ndo maana inatusaidia. Vinginevyo naweza kusema life style ya siku hizi including menu tunazokula zimekua ziki-degrade performance za wanaume tendoni.

  Imefikia wakati sasa kina dada nanyi mgundue chakula au kinywaji kitakacho shusha muda wa kufikia vilele vyenu. Au mnavyo mi sijui? hebu tujuzeni!
   
 7. M

  Mzee wa Kale Member

  #7
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi mamlaka ya chakula na dawa Zanzibar, yalifanya msako katika maeneyo mbali mbali ya mjini Unguja waligundua wauzaji wa supu ya pweza huongeza ndani yalke dawa aina ya viagra, inawezekana tukaona supu ya pweza inaongeza nguvu za kiume kumbe kuna vitu vimeongezwa ndani yake,

  Haya mambo sio ya kushabikia yanaweza yakawa na madhara makubwa sana mbeleni.
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Pweza ni maarufu kwa wanaoishi maeneo ya pwani ya Afrika ya Mashariki na hata pwani ya Mediterranean (Wataliana, Spanish, Wagiriki, Eastern Europe..). Mimi kwanza kusikia hadithi ya supu ya pweza ni miaka mingi nyuma na hata wanaoishi Mediterranean wana imani inayokaribiana na hiyo.

  Ila vile vile kwa akina mama ambao wamejifungua karibuni supu ya mweza inasaidia katika kumuwezesha mama kutoa maziwa kwa wingi. Na hii inaeleweka sana kwa wakazi wa pwani yetu. Inasemekana inatokana na pweza kuwa na kiwango kikubwa cha Calcium.

  Kwa hivyo akina mama na nyinyi musibaki nyuma nyuma supu ya pweza ina faida kwenu vile vile.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kamanda bwabwa hata mie ni mwanaume halisi lkn tukiwa kwenye maongezi yetu mara nyingi utasikia jana nilikuwa na gemu, kabla yake nikabwia valuu au ngisi au supu ya pweza basi kitu hakilali mpaka mwisho, huyo ana maanisha bila msaada hapandi mtungi
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Peleka hii hadithi yako kwenye magazeti ya shigongo!
  Supu supu tu hata ikiwa ya kitimoto!
   
 11. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kisaikologia imani yako itakuponya. Hata ukiamini nikila mavi ya kuku yatanisaidia basi yatakuwa dawa.

  Imani yako ita-tune akili yako na mwili wako kupata kile unachotala
   
 12. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii ni dalili mbaya kwa wanaume wengi wenye mawazo na tabia ya kutumia vitu kama hivyo kwa kujiongezea nguvu za kiume huko mbeleni..!

  Inapofikia mahala mwanaume akafikiria kuji boost kwa supu ya pweza au Konyagi na wengine husema dawa za kimasai basi jua kwamba uwezo wake wa nguvu za kiume ni dhaifu. Ikija tokea akavikosa vitu vya jinsi hiyo wakati wakufanya tendo la ndoa huenda asiweze kuenjoy au hata kutokuweza kusimamisha tena kwani atakuwa kesha jiharibu kisaikologia.
  Kula pweza kama kitoweo na tumia Konyagi kama kinjwaji na si kwa madhumuni mengi.!
   
 13. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mbona kazi jamani.mhhh!
   
 14. N

  Ngala Senior Member

  #14
  Mar 20, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tendo la ndoa linaanzia pale tu ubongo unapoamrisha mwili kuwa tayari kwa tendo hilo.ukiwa umebanwa na mkojo waweza stahimili ukajizuia lakini stahimili huisha ghafla pale unapoona choo na mawazo yakakutuma kwenda kujisaidia na ukichelewa kidogo tu jua litamwagika nguoni.tatizo la nguvu za kiume linasababishwa na kinamama wenyewe kwa kuweka wazi mno maumbile yao kiasi cha kuwa mazoea machoni mwa wanaume.tatizo hili lipo kwa wenzetu wazungu miaka mingi iliyopita kiasi kinamama wenye nazo hufunga safari kwemda thailand na kwingineko ili akatoshelezwa.hapa kwetu yapo njiani yaja pweza na valuu ni ishara tosha ya huko tuendako.vijana wengi wanapokuwa hawajalewa ukimuuliza habari ya madem hakuelewi hata kidogo haoni kipya cha kumshawishi maana mchana kutwa anayaona mapaja viuno makalio ya kila aina so lazima nguvu za kiume zifikie tamati KWISHNEEE
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mbona mazoezi yanasaidia sana sio mpaka misupu hio wakuu.tujenge tabia ya kufanya mazoezi na inasaidia kwenye mambo mengine ya afya pia.tukimbie asubuhi au jioni mara tano kwa wiki inatosha.
   
 16. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #16
  Mar 20, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yenu mtakunywa sana hizo booster kama hamtabadilisha tabia. unategemea nini kama unataka mechi wakati mdada hayupo tayari kwa mechi? na sometimes maandalizi basi yawe mazuri kama unaona mdada hayupo kwenye mood ya mechi. wamama wengi siku hizi wanalalamika kubakwa na wapenzi wao, sasa kama mtu unabakwa unaweza kujitune na kupanda mlima kwa kasi ya anayekubaka? unaishia kumsindikiza tu huyo anayetaka kupanda mlima, akifika basi unakuwa umetimiza wajibu.
   
 17. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Well said!
   
 18. Z

  Zeddie Member

  #18
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha ha ha ah
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Da kweli JF kiboko. Leo ndio nimegundua jinsia ya chimunguru.
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahahaha ndo maana dawa nyingi zinaongezeka mala supa shaft ,mala Ngetwa 11 mradi tu wapate starter ya kuwashia gari
   
Loading...