Dar Es Salaam tunapoteza utamaduni na mila tulizoachiwa na wahenga

Kwa Dar wilaya ya Temeke bado haya mambo yanaendelea kwa kasi ila Kinondoni si sana
Wazaramu wengi wameswagwa katikati ya jiji wamehamishiwa katika pori la mkuranga, ndio maana Ilala na kinondoni hayo mambo siku hizi hayapo.
Maeneo ya magomeni pamoja na kinondoni Wadigo nao walikua wameshaanza kuwateka watu na ngoma zao za baikoko ila kwa sasa hivi naona wameshadhibitiwa hatusikii tena vile vigoma mitaani.
 
Sheria na amri za Mungu zinampa nani favour? Hivi hujui sheria za Mungu zina mfumo dume kupitiliza?
Hapana hazina mfumo dume kupitiliza bali ni binadamu ndo wanashindwa kutafsiri maandiko vizuri na kuyaelewa wanaishia kuelewa vile ambavyo wanataka wao iwe

Lakini tamaduni za kiafrika ni kandamamizi sana kwa wanawake yaani kuna jamii (hasa wanaume) zilihakikisha zinafanya kila namna hii dunia iwe ni jehanam kwa wanawake
 
hiyo au hizo mila zinatoweka na ndiyo sababu unaona sasa au sikuhizi maadili katika ndoa hakuna na ndoa zinavunjika hovyo zamani kuvunjika ndoa ilikuwaga hakuna kabisa labda moja kwa elfu hicho walichokuwa wanakipata unyagoni hakuna gumu ambalo anaweza akaliona kwa mwanaume akashindwa kuvumilia hakuna sasa siku hizi hujampiga kibao wala nini ukamtukana tu mwanamke anadai talaka
Kwahiyo mnataka wanawake wafundishwe jinsi ya kuvumilia uonevu wa waume zao kwenye ndoa si ndiyo? Kwani wanaume wanashindwa kubadilika na kuacha uonevu? Badala ya wanaume kubadilika na kuacha kuonea wake zao wanataka kulazimisha wanawake wakubaliane tu na huo uonevu wao

Na kwanini umtukane au umpige mkeo eti kwa sababu kakosea kwanini yeye ni malaika kwamba hatakiwi kukosea au hata wewe pia hukoseagi? Na wewe ukikosea nani anakutukana au anakupiga? Yaani waafrika siku tutakapotambua kwamba na wanawake nao ni binadamu ndo tutaacha kuamini huo upumbavu ndo maana wazungu wanatudharau
 
na ukimpata mwanamke aliyepitia hizo mila ndugu utafaidi ni wat***mu balaa wanajituma balaa sikuhizi mtu anakupangia mpaka siku za kuduuuaisee shida tupu siku hizi
Tatizo hamtaki kujitathmini wanaume mnakosea wapi mnawaza kutupa lawama kwa wanawake tu tamaduni zilikuwa enzi hizo ambazo mwanamke anakaa nyumbani anafanya kazi za nyumbani na kulea watoto na mume na mwanaume anaenda nje anatafuta pesa na kuhudumia watoto na mke

Siyo siku hizi wote wanaume na wanawake wanapambana na maisha na wote wanahudumia familia halafu mume akitoka kazini kazi yake imekwisha lakini mke akitoka kazini kazi za ndani zinamsubiri na kulea watoto kunamsubiri na bado akitoka hapo mume anataka mkewe akampe manjonjo chumbani

Mke akishindwa mume anachepuka anasema mkewe hamtimizii mahitaji yake yote tena anachepuka na vibinti ambavyo havina hata kazi yeye ndo anavihonga kwa mtindo huu acha tu ndoa ziendelee kuvunjika hakuna anayependa kubebeshwa majukumu mengi peke yake kama punda wakati mwenza wake anaweza kumsaidia

Maana wanaume hawataki kutimiza majukumu yao kwenye ndoa ila wanataka wanawake watimize majukumu yao kikamilifu na pia wanaume wanataka wake zao wawasaidie majukumu yao ila wao hawataki kusaidia majukumu ya wake zao wanatoa visingizio lakini bado anayelaumiwa ni mwanamke
 
Kwa nini hukuchezwa na unapenda unaweza ukachezwa ukubwani haina tatizo,Mimi sikuchezwa kupigwa bila sababu ya msingi nani anataka 😀😀
sasa nipo kwenye 40's inawezekana? haki napenda nifundishwe mambo ya wakubwa hahaha maana nayajua kijuujuu sana.
 
Back
Top Bottom