May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Leo nimesikia kwenye habari ya kuwa Mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani watarajie upungufu wa maji kutokana na kina cha maji ya Mto Ruvu kupungua.
Mwanamuziki Bob Marley kwenye wimbo wake wa 'Rat race' kuna mstari anasema "in the abudance of water the fool is thirsty"...na maandiko yanasema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".
Nimekuwa najiuliza hili kwa miaka mingi kuhusu yale maji ya baharini, ni maji mengi sana yasiyotarajiwa kuisha milele...Miaka ya nyuma niliwahi kumsikia Mwanasayansi au Mwanasiasa sikumbuki vizuri wa hapa kwetu akisema teknolojia ya kusafisha maji yale ni ghali sana, nikajisemea 'ala' sasa ikiwa ghali ndio tupande vitandani tuchape usingizi tusubiri miujiza?.
Mambo duniani hufanywa kwa mikakati, kama tuna Wanasayansi nchini basi tuwawezeshe washinde maabara usiku na mchana mpaka wapate jibu, waje na teknolojia rahisi ya kuwezesha kutumia maji ya baharini kwa matumizi ya kila siku ya kibinaadamu na kilimo.
Marekani waliweka tu mikakati kuhakikisha Binaadamu anafika kwenye mwezi na ikawa...Hata chanjo ya corona ni mikakati tu baada ya Binaadamu kuwa cornered.
Tusisubiri kila jibu litoke kwa Binaadamu wengine ili hali hata sisi ni Binaadamu.