You nail it!! Ulichokiongea Nathan kama wanatusikiliza na kutusoma ndio iwe ajenda yao kesho!! Mipango yoyote inatakiwa kusimamiwa na utaratibu na sheria, huwezi kuruhusu vitu kiholela ukategemea ndio kugawa riziki!! Na katika taifa lolote huwezi kuweka kila MTU akajiajiri mwenyewe... ajabu sana mkuu! Unakataza Hiace (abiria 15) na Coaster (abiria 28) kufika maeneo kama Feri ila unaruhusu utitiri wa bajaji (abiria 3) na bodaboda (abiria 1) kuhanikiza mjini! Hawa wapuuzi mahali popote wanasimama na wanageuza; abiria yuko upande wa pili wa barabara wanageuza wanamfuata kisha wanageuza tena hapo hapo katikati ya barabara wanaendelea na safari!
Kuruhusu hivi vyombo mjini na highway kama Nyerere Rd; Morogoro Rd; A. Mwinyi Rd; Kawawa Rd; Mandela Rd; Sam Nujoma Rd; Shekilango Rd; etc. ni ukosefu wa busara na maarifa. Sio kila chombo kiruhusiwe kupita kila mahali kwa kisingizio cha "riziki" au eti "watanzania ni maskini". Riziki kwako isiwe kero kwa wengine.