Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,492
- 92,983
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amezuia utekelezaji wa zuio la Bodaboda na Bajaji kuingia mjini hadi atakapotoa tamko jipya baada ya kikao chake na Uongozi wa Bodaboda, Jeshi la Usalama Barabarani na Uongozi wa Jiji la Dar es salaam.
Mapema leo Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdi Issango alizungumza kupitia Power Breakfast ya Clouds FM na kusema ifikapo November 01, 2021 bodaboda na bajaji zote itakuwa ni marufuku kuingia mjini na kuwataka wale waliokua mjini watoke wote isipokua bajaji za walemavu.
RC Makalla amesema amezipata taarifa hizo na ameelekeza kabla ya utekelezaji wa tamko hilo yeye RC ameitisha kikao hicho Jumatatu November 01 kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ambao hautoathiri upande wowote. #MillardAyoUPDATES