Dar es Salaam: Rais Magufuli amemsimamisha kazi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao na mkuu wa upelelezi mkoani humo, John Rwamulema kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Novemba 23, 2019 na msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime inaeleza kuwa wawili hao wamesimamishwa kazi wakidaiwa kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha Canon cha mkoani Shinyanga kukwepa kodi.

“Sababu ya pili ni utovu wa nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack,” inaeleza taarifa hiyo.
 
Haya matamko ya usiku kucha nayo ni shida...mkuu atakuwa yupo ndotoni aisee.
 
Wawakamate wawanyonge, tuna jeshi LA Polisi katili sana sijawahi kuona maisha yangu yote. Vile viaskari pale Njombe vichukuliwe hatua pia, vina lugha chafu sana sana na vinajifanya vijuaji sana sana
 
Njombe sehemu gani??
 
Hao waliotolewa lazima watakuwa walisita pahala kuishighulikia chadema. Hoja zilizotolewa ni kifunika komba,.....
.
 
Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao na mkuu wa upelelezi mkoani humo, John Rwamulema kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Novemba 23, 2019 na msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime inaeleza kuwa wawili hao wamesimamishwa kazi wakidaiwa kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha Canon cha mkoani Shinyanga kukwepa kodi.

“Sababu ya pili ni utovu wa nidhamu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack,” inaeleza taarifa hiyo.

Dar es Salaam: Rais Magufuli amemsimamisha kazi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Amesharudi Dar?

Si alikuwa Dodoma?
 
Back
Top Bottom