Dar es Salaam ni tofauti kabisa na maeneo mengine Tanzania, ni kama ipo nchi nyingine

Wakihamia Dodoma,hi Dodoma nayo itakua kimaendeleo kama Dar? Vipi Mtwara kwenye gesi? Huko kaskazini kuna Arusha na Moshi zinaelekea kuungana muda si mrefu.Mwanza nayo inakuja juu ikiifukuzia Dar
 
Kuhusu gharama ya maisha utakuwa umeamua mwrnyewe, mfano.
WALI- Mwananyamala 1500 Posta 3000
KADETI - Kinondoni 30,000 Mchikichini 7000
Nauli from Kimara-Posta labda=650 lakini kuna watu wanatumia zaidi ya 10,000
Suti 350,000 lakini kuna mtu ananunua koti 2000 suruali 2000,shati 3000, tai 3000, na viatu 5000 amemaliza hapo.
Bia ni sh 2500 lakini kuna watu wanainunua kwa sh 8000 bia hiyo hiyo na mwingine akiwa na 8000 analewa gongo chakari siku tatu
Nimewahi kwenda Lindi nikahisi maisha ghali kuliko huku. Nyuma ya stendi pale Supu 3500 wakati sisi nyuma tu ya Mahakama ya Kinondoni ukiwa na buku unakunywa supu na chapati 2 safi. Huku maisha ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom