DAR-ES-SALAAM ndio TANZANIA tuuuu basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DAR-ES-SALAAM ndio TANZANIA tuuuu basi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jethro, Oct 29, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Katika mahojiano ya JK na PowerBreakFast-FM, JK ameelezea swala la miundombinu Dar na ukiangalia kweli serikali itaimarisha miundombinu kataka hilo Jiji, which Means DAR-ES-SALAAM ndio TANZANIA tuuuu basi, Kwahiyo Mikoa mingine yote haiitaji Miundombinu kuboreshwaa?

  Katika Ilani ya CCM serikali ilipaswa kuhamia DODOMA mpaka leo hakuna dalili na hata kwa miaka 10 ijayo serikali haito hamia DODOMA na hiyo kutokana na Kusikiliza maelezo yake ya hiyo miundombinu itakayo tekelezeka DAR pekeyake.

  Machinga Copmlex utazijenda wilaya zote za DAR je Mikoa mingine watasubili kwanza mpaka za DAR ziishe ndio wahamie Mwanza au zote zitakuwa zikijengwa kwa wakati huo huo katka baadhi ya mikoa mikubwa kwanza?

  Kwa hali hiyo sidhani kama watu wataendelea kukaa huko Lindi/Kigoma/Tabora/ Sumbawanga kwani mikoa mingine itabaki nyuma sana kimaendeleo ni bora Nchi igawanywe kwenye Majimbo
   
 2. u

  udongo Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo Machinga Complex za Dar zimeshaanza kutumika? Nimeamini huyu ndugu yetu uwezo wake ni mdogo kupindukia
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nini kingine alichosema.
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Nyiii zilikuwa ni stories tuuuuuuu

   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ziko kwenye Mikakati ya kujengwa na kipaumbele kimepewa DAR, Kwa ukaribu tuu ukiangalia ni kuwa serikali yetu haiko makini kufanya research na kujua wapi pa kuanzia kwa mfano wingi wa watu kuhami DAR ni nini? na ni Jinsi gani kupunguza Ongezeko la watu kuhamia Dar kukimbia kijijini sasa sijui kama hiyo kilimo kwanza itawarudisha watu huko vijijini?

   
 6. J

  Jackob Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuh! jamani Jethro, Ina maana wewe hujui kila jiji/mji/kijiji vinakuwa na mahitaji tofauti kwa nyakati tofauti. Moja ya mahitaji muhimu ya jiji la Dar kwa sasa ni miundombinu hususan barabara ambapo kila mkaazi wa jiji anaonja joto ya jiwe kwa staili yake. si kipindi cha mvua wala kiangazi. Wakati wa mvua maji hujaa kila kona na madimbwi kedekede na wakati wa kiangazi wasafiri wa magari binafsi na public wanakoma kwa joto kwenye magari yao na pamoja na vumbi, si kwa waenda kwa miguu wala wenye magari hata wenye maguta na mikokoteni pia.
  huwezi ukaja kutangaza kilimo cha umuagiliaji kwa wakazi wa dar. huwezi kuja kutangaza majosho ya mifugo kwa wakazi wa dar na huwezi kuja kutangaza maghala ya chakula kwa wakazi wa Dar, hizo sio kero za wakazi wa dar. Piga ua, ni wendawazimu uliopindukia kuponda mikakati ya kuboresha miundombinu ya barabara dar. nadhani hujui hata maumivu ya gharama za uendeshaji wa vyombo vya moto kwenye barabara zetu ndio maana unakimbilia kulaumu. Kama ni ahadi zingine si alizitoa kwenye maeneo au miji aliyoipitia wakati wa kampeni?
  Ukibeza mpango wa miundombinu bora Dar utakuwa mchawi kwelikweli.
  Pia lazima ujue kuwa Dar ni Gateway kuu ya nchi. Pia dar ndio inaongoza kwa kuingiza mapato ya Serikali na hivyo wakaazi wake wana haki ya kunufaika na kuboreshewa miundombinu kama ilivyo kwa majiji na miji mingine nchini.
   
 7. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa, kwani si anaomba kura kwa watanzania wote? Labda useme ataongea na sisi wengine wa mikoani siku nyingine na aseme nini atatufanyia!!!!!!!!!!!!

  NN
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  anayo ongea jk yalikuwa si ya raisi bali halmashauli za manispaa zipange hayo mambo, huyu ni raisi wa tz na si dar tu! Tena alitakiwa aongeelee watu kwenda kulima mikoani badala ya kuwavutia hata wale wanaolima kutamani kuja dar kwenye biashara. Namuunga mkono jethro! Mikoa yoote inahitaji kuendelezwa kwa usawa ili kuleta maendelea nchi nzima!
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ndugu fikilia zaidi kuhusu hili!
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kILIMO KWANZA KIWALUDISHE WATU KIJIJINI??? HAIWEZEKANI KWA MWENDO HUU LABDA KIWATOE WATU KIJIJINI KUJA MJINI, ASILIMIA KUBWA YA WATU DAR WANAISHI KISANII TUUU KIHUNIHUNI, JITU ZIMA MIRABA MINNE LINAUZA SIMU ZA DILI CM YENYEWE ANAYO MOJA SI UTAPELI HUU! TUNAPOTEZA NGUVU KAZI KUBWA HAPA.
   
 11. M

  MJM JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono. Kwa kuongezea siyo tu simu ya mkononi ya dili bali pia vifuko vitatu vya korosho. Omba omba kibao mitaa yote ya Dar. Something has to be done. Kuna vitu yeye kama rais alitakiwa kukemea halmashauri na kuwahimiza wafanye ambazo ni weak points za serikali yake amegeuza kuwa sababu ya kuombea kura.

  Kitu kama daraja la Kigamboni ni story tu zinaendelea. Ukiangalia idadi ya watu kwenye feri na foleni pale unaona kama watendaji na rais mwenyewe wangekuwa makini wasingemwita rais kufungua kivuko badala ya kuzindua daraja (karne ya 21) tena katikati ya jiji (only 800 mitres. Wangeangalia jinsi ya kushirikiana na wananchi na potential investors (Public Private Partnership - PPP) kila kitu kingekuwa sehemu yake. Ni weak point ambayo yeye anaona sababu ya kuombea kura
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Bado tuna matatizo katika kujua vipaumbele katika nchi yetu,mambo emngi ambayo rais Kikwete amekuwa akiahidi ni miradi ambayo afisa mipango yeyote katika wilaya au sehemu yoyote anaweza kuipanga na ikafanikiwa.

  Tunachotaka wananchi toka kwa JK ni mipango mipya ya kujiletea maendeleo yetu ya sasa na ya vizazi vijavyo,kwa mwendo huu wa nguvu za zima moto hatutafika popote.
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Duuuuuh!!!!!

  Thankx Bro!!

  Nadhani unaelewa Fika nini maana ya usawa kwa wote na maendeleo kwa wote maana JK alikuwa anatoa reference za Dar na huko kwa upande wa pili ndiko Fund kila zikija lazima iwe Dar kwa nini.

  Basi nasi huku Mikoani Dodoma si tuna Uranium sasa basi iwe ya wana dodoma ,Tanzanite iwe ya wana Manyara/Arusha na mbuga zao na huko Musoma nao Serengeti iwe yao, Mwanza na Bukoba Gold/Diamonds Minings Na Lake victoria zote hizi ziwafaidishe basi wale wote walioko hayo maendeo kama Funds zitolewazo zina ubaguzi wa kukuza maendeleo ya kila miji/jiji/vijiji pia??

  Aliye kudanganya Dar inaongoza kwa kuingiza mapato huko ni nani na lazima ujue ni mapato ya aina gani Dar inaongoza kuingiza TRA?

  Ndg Jackob wewe ukiwekwa kuwa Mkurugenzi au mayor wa JIJI nadhani ndio utavuruga kabisa kwani marengo yako ni ya kujionea wewe naomba kabisa utoke huko kwenye fikra za umimi kwani hizo dalili ni sawa na Udini+Ukabila ndivyo wewe utakavyo ongoza JIJI au kitengo chochote. Sie twaongelea maendeleo ya kwa pamoja nchi nzima wewe wa tetea Dar tuu??? kama wewe ni kijana nadhani unatakiwa uwe na vision ya haraka sana mkuu.

   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hayo uliyo yasema ndio mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na yawe kwenye MUSTAKABALI wa nchi kwani sasa ukiwauliza hao watu wa IKULU nini au ni hupi ndio MUSTAKABLI WA NCHI hawajui wao ni kujifanyia mambo kihole hole na kumpiga Rais changa la macho kila kukicha

  Nini namaanisha eg NASA wanafikilia kuwa by 2030 wanataka watu wafike sayari ya Mars na wakae kwa muda fulani kwahiyo sisi hapa Turipaswa kumsikia Rais akisema japo kuwepo kiwanda cha Ku assemble hata Ma tractor,Mabasi, viwanda vyakuzarisha malighafi nyingi au Tanzanaite/Diamonds/Gold Hazito kuwa zinafanyiwa Processing tena Nje ya nchi means viwanda vitakuwepo hapa 2015 na kuendelea hayo ndio twayataka kusikiliza kwani more than 40yrs after Independence yet twategemea meza za kichina jamani na huku magogo twayasafirisha sie wenye kwa serikali makini haiwezi kufanya upuuzi kama huo kabisa ndio hayo ya JK.
   
Loading...