Dar es Salaam na Pwani, kwanini usiwe mkoa mmoja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar es Salaam na Pwani, kwanini usiwe mkoa mmoja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Columbus, Oct 20, 2012.

 1. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mtakubaliana nami kwamba wafanyakazi na wafanyabiashara wengine hapa Dar wanatokea mkoa wa pwani na kurudi kila siku kiasi kwamba imekuwa vigumu kutofautisha mikoa hii miwili.

  Wakati mwingine unalazimika kupata huduma fulani fulani mkoa wa Pwani ingawa unaishi pembezoni mwa Dar.

  Imefika wakati tungependa kujua ni sababu zipi zilizofanya mkoa wa Dar utenganishwe na mkoa wa Pwani. Kutenganishwa huko kumepelekea kuongezeka kwa watumishi wa serikali isivyo lazima, mkoa wa Dar umesongamanishwa na ofisi kibao na makazi ya watu, vile vile makambi ya jeshi zaidi ya 20 yamezunguka mkoa wa Dar kwa sababu zipi?

  Ukiangalia kwa makini mikoa hii miwili ni midogo midogo na huu mkoa wa pwani umeuzunguka mkoa wa Dar kwa pande zote. Nchi yetu ni masikini, imefika wakati tupunguze gharama za uendeshaji serikali zisizo za lazima.
   
 2. d

  diwan JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kwel mkuu.Huwa sijui walifikiria nin kuweka mkoa ndani ya mkoa. Ukitoka kibaha unaenda mkuranga unapta dar, ukitoka bagamoyo unaenda mkuranga,mafia etc unapta dar.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,261
  Likes Received: 19,389
  Trophy Points: 280
  kisarawe je?
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,740
  Likes Received: 6,016
  Trophy Points: 280
  Una haki kabisa ya kutoa maoni na mawazo yako kama ulivyofanya. Tena zamani ilikuwa hivyo unavyofikiria. LAKINI usidhani waliofanya iwe kama ilivyo walikuwa wajinga kuliko sisi. Wakati mwingine tatizo tulilo nalo vijana wa leo ni kudhani tuna akili kuliko waliopita; la hasha. Kwa kadiri ya uwezo wa kufikiria wa mwanadamu hakuna jipya chini ya jua.

  Ndio yale yale ya waziri mmoja wa elimu kipindi cha awamu ya tatu kuvuruga kabisa mfumo wa elimu uliokuwa umewekwa kipindi cha awamu ya kwanza na ya pili pengine kwa kuwaona waliotangulia walikuwa wajinga baada ya muda tukarudi kule kule.
   
 5. jason

  jason JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 295
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  wakati serikali inafikiria hata hizi wilaya za dar ziwe mikoa we unataka waunganishe dara na pwani hilo sahau, mkuu maana wenzetu hawana time na kubana matumizi
   
 6. y

  yaya JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, wazo lako ni zuri. Lakini walioamua kuitenganisha hii mikoa miwili japo awali ulikuwa ni mkoa mmoja yaani, Pwani, walifanya kwa sababu za kurahisisha utawala na maendeleo ya mkoa wa Pwani.

  Unachokiongelea wewe ni kwa kuangalia miji iliyoko Pwani, lakini karibu na DSM tu. Huangalii maeneo kama Kilwa, Rufiji, utete, Bagamoyo, Chalinze n.k. Unayaonaje hayo maeneo? Yapo karibu na DSM? Unaweza kuishi Kilwa na kufanyakazi DSM? Maendeleo yake nayo unayaonaje? Unadhani yanaweza kupata maendeleo ya haraka kwa kutegemea mtawala wa mkoa anayeishi DSM.

  Ukipata majibu ya maswali haya machache kati ya mengi ambayo hayakuorodheshwa hapo juu, ndipo utapata jawabu la kwa nini ilitenganishwa.
   
 7. G

  Gangi Longa Senior Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  na pia Mafia
   
 8. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Pwani ibaki hivyo hivyo kwa sababu ni eneo la kitalii ambalo limewahi kutoa kiongozi dhaifu ambaye hajawahi tokea popote duniani,baadaye tz itapata watalii wengi sana wa nje na wa ndani.ni mtazamo tu wakuu.
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Nyerere alimpa Kighoma Malima ili aiendeleze kama Msuya aivyopewa Jangwa la Mwanga
   
 10. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo unataka kutuambia nini?
   
 11. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi kuwa na serikali ndogo au kubana matumizi kwa serikali ndio inamaanisha maisha bora ya wananchi kila wakati? kwa ufaham wangu mdogo wa misingi ya uchumi jibu ni HAPANA. hivyo kuongeza mikoa pia kunaongeza ajira lakini pia kunarahisisha utendaji kazi wa serikali.
   
 12. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Eleza basi hiyo maana waliyokusudia, na kama walikushurikisha.
   
 13. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndio maana wazanzibar wanataka nchi yao sasa, unakumbuka Nahodha alihoji rasilimali za Zanzibar akafumbwa mdomo kwa madaraka ya uwaziri?
   
 14. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  acheni ibaki ilivyo,kwahyo ikitokea pia moro wakafanya kazi dar na kurudi itabidi mikoa hii iungane uwe 1 .. ni mitizamo
   
 15. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapo umenena. Mimi naishi mbele ya GongolaMboto-mabomu lakini huduma zangu nyingi nazifuata Kisarawe ikiwa ni pamoja na umeme tanesco, huduma ya benki, kulipa kodi mbalimbali TRA, huduma za kilimo bwana shamba, hospitali, shule nk nk.
   
 16. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hoja ya wakazi wanaishi na kufanya kazi mikoa tofauti haina mashiko vipi Arusha na kilimanjaro? vipi Mtwara na Lindi? ok tuiache kama ilivyo kumbuka mkoa wa pwani ni mkubwa sana na dar ina wakazi wengi sana so ukiichanganya huduma za jamii zitazorota sana mkuu
   
 17. m

  mdunya JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tehe tehe tehe!
   
 18. m

  mdunya JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni upuuzi wa akina Magufuli, Mwakyembe na Tibaijuka kuwaza kuijenga Dar na si Tanzania! Wangepunguza viwanda, vyuo vikuu na maofisi ya serikali Dar ingeshikika! Tumbaku Tabora na Kigoma kiwanda Dar (upuuzi)! Tibaijuka anawaza sattelite city & Kigamboni (upuuzi) wakati kuna maeneo mengi ya wazi. Magufuli anawaza barabara za juu (upuuzi) badala ya kushauri kuondoa vyuo vikuu Dar! Nchi ina vyuo vikuu kama 60 na takribani 30 viko Dar (upuuzi). Mwakyembe anawaza treni ndani ya jiji (upuuzi) badala ya kufikiri nini vinajaza watu mjini!! Upuuzi
   
Loading...