Dar es Salaam Mpya: NSSF kuanzisha miradi mikubwa jijini; Mwisho wa malori kuingia jijini wawadia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Imeandikwa na Waandishi Wetu, Zanzibar

Jumanne, Desemba 04, 2012 12:21

*NSSF kuanzisha miradi mikubwa jijini
*Mizigo bandarini kuondolewa kwa treni tano
*Mwisho wa malori kuingia jijini wawadia
*Nyumba zote Manzese, Vingungu kuvunjwa

Sura ya Jiji la Dar es Salaam itabadilishwa na kugeuka jiji la kisasa ndani ya miaka minne ijayo kutokana na mpango mzito ulioandaliwa na Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF).

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau, ameliambia Jamhuri mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki kuwa Mfuko huo umenunua ekari 1,000 za ardhi huko Kisarawe ambazo watajenga Bandari Kavu.

Kutokana na hatua hiyo, mizigo yote bandarini itatolewa moja kwa moja kutoka melini na kupelekwa Kisarawe.


Dk. Dau anasema katika kusafirisha mizigo hiyo watatumia treni tano zenye behewa 20 kila moja, kwa maana ya behewa 100, na hivyo mizigo itatolewa kwa kasi bandarini kuliko wakati wowote katika historia ya nchi hii.


"Nisingependa kuwa msemaji wa bandari, lakini najua kwa sababu nimefanya kazi pale, bandari ya Dar es imepitwa na wakati.

Bandari ya Dar es Salaam ipo kwenye daraja la pili, Mombasa wameboresha wapo daraja la tatu, lakini bandari nyingine duniani zipo kwenye 7th generation (daraja la saba).


"Bandari makini inapaswa kuwa sehemu ya uzalishaji mali. Inapaswa kuwa imezungukwa na viwanda vidogo vidogo. Dubai bandari yao imezungukwa na viwanda vya kutengeneza washing machines, tv na vitu vingine ambavyo baada ya kutengenezwa tu vinasafirishwa," amesema Dk. Dau.


Ameliambia Jamhuri kuwa chini ya mpango ulioandaliwa na NSSF, meli ikiingia bandarini inapakua mzigo na kuweka kwenye treni na mzigo huo unasafirishwa moja kwa moja kwenda Kisarawe.

Kufanikisha mpango huu NSSF watajenga hoteli, vituo vya mafuta na maduka huko Kisarawe ambapo malori karibu 3,000 yanayokwenda bandarini sasa yote hayataingia jijini Dar es Salaam.


"Hii itapunguza msongamano kwa kiwango kikubwa. Clearance ya mizigo yote haitafanyika tena hapa bandarini, bali itafanyika huko Kisarawe," anasema Dk. Dau.


Anasema mbali na kwamba NSSF watapata fedha kutokana na mradi huu, anaamini kuwa Mfuko utakuwa umetimiza jukumu la msingi la huduma kwa jamii ambayo inapaswa kupunguziwa matatizo kwa njia kama hizo. Mradi huu unaanza mwaka huu wa fedha. Dk. Dau hakutaja kiasi kitakachotumika kugharamia mradi huu kwa maelezo kuwa bado wataalam wanaendelea na uchambuzi wa gharama.

NSSF kuboresha makazi
Mkurugenzi wa Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula, aliwambia wahariri mjini hapa kuwa Mfuko unaanzisha mradi wa kujenga nyumba za kisasa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambapo nyumba zilizojengwa bila mpangilio zitavunjwa na kujenga nyumba zenye viwango.

Utaratibu ulioandaliwa na NSSF chini ya mradi huu ni wa kujenga nyumba za dharura kwa watu wote watakaohamishwa katika makazi yao na kuwaweka katika nyumba hizo, kisha kutumia miezi 24 kujenga nyumba katika eneo walipohamishwa wakazi hawa na baada ya hapo wanarudishwa kwenye nyumba zao.


Kutakuwapo utaratibu wa kuwalipa fidia wenye nyumba wakati wa kuwahamisha, lakini baada ya ujenzi kukamilika waliokuwa wamiliki wa nyumba zilizovunjwa watapewa fursa ya kununua nyumba mpya zilizojengwa kwa bei nusu ya gharama. Nyumba za ziada zinazojengwa katika maeneo hayo zitauzwa kwa bei ya soko na hivyo kufidia gharama zilizotumika.


Katika Jiji la Dar es Salaam, Wilaya ya Temeke nyumba zitakazovunjwa na kujengwa upya chini ya utaratibu huu ni zile zilizopo katika maeneo ya Mtongani, Kichangani, Keko, Chang'ombe na Mbagala.


Kwa Wilaya ya Kinondoni, mradi huu utaanza kwa kuvunja na kujenga nyumba za Magomeni, Kigogo Mbuyuni, Mkwajuni, Mwananyamala, Mburahati, Manzese, Msasani, Kinondoni Shamba na Mwenge.


Mradi huu mkubwa kwa Manispaa ya Ilala nyumba zitakazovunjwa na kujengwa upya ni za Mchikichini (mradi umeishaanza), Vingunguti, Buguruni na Gongolamboto.


Hospitali ya Apollo yaja Dar
Dk. Dau ameliambia Jamhuri kuwa kufikia Februari mwakani, wagonjwa waliokuwa wanapelekwa India kwa uchunguzi wa afya wataweza kupata huduma hiyo hapa nchini.

Amesema kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili, tayari wameingia mkataba na Hospitali ya Apollo ya India, ambayo itafunga mitambo ya kisasa ya kuchunguza afya na kufanya matibabu ya msingi katika Jengo la NSSF Bibi Titi, Dar es Salaam.


"Katika jengo letu hili wamechukua ghorofa tatu za chini na wanafunga vifaa vipya kabisa. Vifaa hivi vitatumiwa kufanya uchunguzi wa afya kuanzia kichwani hadi kwenye kisigino.

Hatutakuwa na sababu tena ya kumpeleka mtu India kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya isipokuwa kwa magonjwa yaliyoshindikana tu," amesema.


Ameongeza kuwa Apollo wamesisitizwa kuwa gharama ya matibabu isiwe kubwa. Kwa mfano yeye aliwahi kupima kipimo cha mwili mzima kinachogharimu dola 200 (Sh 360,000) huko India, hivyo akasema kila mtu anastahili kupata huduma hii kwa gharama nafuu.


Kwa miradi hii iliyotajwa ikikamilika Jiji la Dar es Salaam litabadilika sura na kuwa la kisasa sawa na majiji mengi duniani ya nchi zilizoendelea.
 
Watu wanaoishi MANZESE na VINGUNGUTI wataenda WAPI? Isije Ikatokea kama SLAMs za NAIROBI kwa Wananchi kufukuzwa kwenye VIWANJA halali...

Nani alishakuwa MBUNGE wa KISARAWE???
 
wanaita fao la kujitoa?

naona NSSF imekuwa ndio kimbilio kwa sasa, waache kuchota huko ili miradi kama hii iwe feasible
 
Ukisikia ushe..i wa tabia wa ndio huu, kwanza serikali itetehe hoja ya kusema bandari ya Bagamoyo inayotaka jenga hipo kwa mantiki ya kupunguza msongamano wa mjini na kwa sababu za kupunguza unnecessary traffic at city centre. Hapohapo serikali imejizatiti katika kujenga an economic zone to justify the project at the expense of tax payers money and outside investment.

Halafu anakuja mpuuzi kama huyu anasema anataka jenga reli na kubomoa nyumba za watu (assuming with the government blessings) whilst the same government has promised to reduce the inflow of traffic in the city by building another port.

Sasa basi hiwapo bandari ya bagamoyo itajengwa wouldn't that solve that same traffic problem assuming residential areas are restricted and all other plans are considered and the priority is the inflow of goods.

In short Dr. Dau kaishiwa and apparently he has got too much money on his hands na hajui pa kuzipeleka ndio sababu wengine tunasema kuna watu wengi wapo kwenye position ambazo si haki zao sio kwa sababu ya elimu zao bali they're just not creative enough for the posts they hold.
 
Here is the NSSF pathetic business strategy the area that we seek to demolish has increased in property value from what we can destroy, for that matter either way we are not going to loose in the property development considering the poor are not going to be paid on market value but we will charge on the current market value once we build.

If the government is going to build a port in Bagamoyo no body should allow this fools to do anything it is not on the social interest, rather it is just an exploitation of the poor.

Have morals Dr. Dau
 
Pendekezo: Dr. Ramadhani Dau awe Rais au hilo likishindikana NSSF iwe wizara ya serikali!
Tatizo sio serikali kushikilia hivi vyombo, tatizo ni watu wanaokabidhiwa hivi vyombo kujipendekeza na kutaka kudhulumu. Wakisahau potentials za dhamana walizopewa kwa faida ya jamii na serikali.
 
HUKURU MUNGU, MAMBO KAMA HAYA YANAKUJA SIKU HIZI BAADA YA uJAMAA NA KUJITEGEMEA KUFA. la sivyo ungesikia kuwa NSSF imejenga chuo kipya cha siasa kule songea au kigoma!
 
Hivi Mkurugenzi wa NSSF huteuliwa na rais?

Je, rais ni mwanachama wa NSSF pia?.?

Kama sio mwanachama kwa nini wakurugenzi wanajipendekeza kwake na sio kwa wanachama??
 
Wanaongelea ofisini kwenye makaratasi,
miaka minne siyo mingi aangalie haya maneno yake yasijemfuata nyuma.
 
Tanzania is full of suprises,siamini chochote wanachosema,mpaka nione kwa macho yangu....tatizo viongozi wetu perepeche kibao,,,implementation hakuna.
 
Nampongeza sana Dau. futilia mbali slums za manzese na huko ushenzini watu wanaishi utafikiri sio jiji?

Tukiataka maendeleo, fumba macho, safisha jiji ili pawe pasafi, maadamu watalipwa fidia na kupewa makazi ya muda na kuuziwa nyumba kwa nusu bei. ukifika pale manzese hadi ma.vi yananuka watu wachafuuu, mbona hayo hatuyaoni kimara?

Tuache uswahili. ona slums za Nairobi zilivyogeuzwa kuwa apartments za kisasa kama ulaya, wenzetu wamefumba macho, sisi tukiingiza siasa hapa tutaendelea kuishi kama wanyama pori. congrats Dr. Dau.
 
Hii plan ingekua nzuri kama kusingekua na plan ya kujenga bandari ya bagamoyo lakini ile bandari ya bagamoyo mkataba ushasaniwa unaanza ujenzi sasa hata wakijenga itakua hamna mantiki.

Ushauri kwa dr dau ashirikiane na mwakyembe laiti hizo pesa zipo waboreshe reli hii inayotoka posta hadi ubungo ifike mbezi sasa.kuwe na route posta-mbagala,posta-karikoo-tegeta na maeneo mengine hizi reli zikashajengwa na kuwekwa treni nzuri za usafiri zitasaidia sana kuboreshwa usafiri na kupunguza foleni.

Sasa hivi dar ina watu zaidi ya milioni 8 ina maana zaidi ya watu milion 2 wako mizinguko ya kila siku tuseme lazima waendeshe magari yao,wapande daladala kama tutakua na usafiri mzuri wa treni tunaweza wavutia watu milioni 1 kwa siku wakawa wapanda treni zetu sasa ukiweka kwa bei ya 700 shirika la tra lina uhakika wa milioni 700 kwa siku zile za kazi.

Hii ina maanisha kama treni zitakua za kisasa na za speed hata wale wanaotumia magari wataacha nyumbani sasa kama mtu unatoka mbezi to posta kwa dakika 20,huku kwa gari anatumia saa nzima lazima ataanza kutumia usafiri wa treni.

Lakini vile vile tuweza anzisha usafiri wa boat za speed kule ambako maji yanapita mpaka posta mfano kutoka tegeta-posta,mbagala-posta kote kupunguza hizi foleni na kuwahi makazini.

Lakini vilevile dr dau kama anataka kufanikisha plan yake aende mazese pale ananunue zile nyumba za chini ambazo ziko kama slams waingie mkataba na shirika la nyumba wawakopeshe pesa hizo wanazotaka kuchezea wajenge magorofa pale ya kuishi kwa kukodisha kwa watu nyumba za chini pale mazese bei yake ina range milion 150-400.kama mpango utafanikiwa tunajenga ghorofa moja kwa mfano ambalo lina zaidi ya vyumba viwili na choo 30 kwa kila ghofora labda bei ya vyumba viwili na choo ndani ni 100000 watapangisha kwa mwezi wana uhakika wa kupata milioni 3 lakini kwa mwaka wana uwezo wa kukusanya zaidi ya milioni 30 kwa ghorofa.

Lingine litakalo ondoa msongamano bandarini atujengee reli ya kati na matreni ya kisasa hapa amkopeshe hizo hela mwakyembe.tukijenga reli ya kati imara na nzuri leo tutateka soko kubwa la majirani zetu.

Pia msongamano utapungua kuja mjini maroli machache ndo yataingia maana mizigo mingi itabebwa na treni zetu.

Salamu kwako dau na mwakyembe tumieni elimu yenu
 
Ukisikia ushe..i wa tabia wa ndio huu, kwanza serikali itetehe hoja ya kusema bandari ya Bagamoyo inayotaka jenga hipo kwa mantiki ya kupunguza msongamano wa mjini na kwa sababu za kupunguza unnecessary traffic at city centre. Hapohapo serikali imejizatiti katika kujenga an economic zone to justify the project at the expense of tax payers money and outside investment.

Halafu anakuja mpuuzi kama huyu anasema anataka jenga reli na kubomoa nyumba za watu (assuming with the government blessings) whilst the same government has promised to reduce the inflow of traffic in the city by building another port.

Sasa basi hiwapo bandari ya bagamoyo itajengwa wouldn't that solve that same traffic problem assuming residential areas are restricted and all other plans are considered and the priority is the inflow of goods.

In short Dr. Dau kaishiwa and apparently he has got too much money on his hands na hajui pa kuzipeleka ndio sababu wengine tunasema kuna watu wengi wapo kwenye position ambazo si haki zao sio kwa sababu ya elimu zao bali they're just not creative enough for the posts they hold.

Acha kashafa na matusi, Dau unamuita mpuuzi tupe mfano wa mkurugenzi wa Pension fund alie creative zaid ya Dau au pengine hujui maana ya Creativity! Kisarawe ni Bandari ya nchi kavu ya ile ya Dsm we unazungumzia ya b.moyo au unadhani ya b.moyo maana yake ya dsm itafungwa, Huyo unaemuita mpuuzi we mwerevu umemzidi nini zaid ya matusi?
 
walikuwa wapi siku zote 2015 inakaribia ndo wanakuja na mipango mizuri hatudanyiki zamani ilikuwa uchaguzi unapokaribia matinga tinga kila barabara ya vumbi kutibua mavumbi raia hawataki coz wameamka sasa wanakuja na mipango mizuri mi sidanganyiki
 
NSSF iwekeze kwenye teknolojia ya kisasa mtu aweze kupata statement kwa njia ya simu na email tena latest. Wao statement zao ni mwaka mmoja nyuma. Vile vile wapambane na rushwa wakati wa kulipa mafao na usumbufu watu wanaoupata.
 
Wao kila kitu kimepitwa na wakati,mbona CCM imepitwa na wakati hawaibomoi na kuijenga kisasa?.
 
Back
Top Bottom