Dar es Salaam: Mlipuko wajeruhi Mwanafunzi akifanya maonyesho kuhusiana na Umeme katika sherehe za maadhimisho ya elimu

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
mlipuko.jpg

Mlipuko huo ulitokea mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya elimu kwa mkoa wa Dar es Salaam na kuhusisha wanafunzi wa shule mbalimbali na walimu wao.

Katika mlipuko huo, mwanafunzi Nickson Simon wa kidato cha tatu katika Shule ya Fray Luis Amigo iliyoko Tungi, Kigamboni jijini Dar es Salaam, alijeruhiwa vibaya katika mkono wa kulia.

Baada ya tukio hilo, mwandishi alishuhudia mwanafunzi huyo akipandishwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser VX, lenye namba STK 1664, lililokuwa limemfikisha mgeni rasmi mahali hapo na kisha kumuwahisha majeruhi huyo katika Hospitali ya rufani ya Mkoa ya Temeke.

Mwanafunzi huyo alikuwa jirani na meza ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania ambako ndiko mlipuko ulitokea wakati mgeni rasmi akipewa maelezo kutoka kwa wanafunzi kuhusiana na umeme.

Mgeni rasmi baada ya kutembelea mabanda takribani saba, ndipo alipofika kwenye meza ya wanafunzi wa Azania ambao walikuwa wakimwonyesha majaribio yao mbalimbali kuhusu umeme.

Wakati mgeni rasmi akiendelea kusikiliza maelezeo ya wanafunzi hao, ndipo ulitokea mlipuko huo uliosababisha kishindo kikubwa kiasi cha kusababisha taharuki kwa mamia ya watu waliokuwa kwenye ukumbi huo.

Baada ya hapo, mgeni rasmi ambaye hakuwa amepata madhara aliondolewa eneo la tukio akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, huku pia wanafunzi waliojeruhiwa wakipewa huduma za kwanza na aliyejeruhiwa zaidi akiwahishwa hospitali.

Wanafunzi wengine wawili wa Azania walipata majeraha madogo pia, lakini Nickson ndiye aliyeonekana kuathirika zaidi na ndipo alipopelekwa hospitalini akisindikizwa na maofisa kadhaa wa elimu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo lilisababisha shughuli zilizokuwa zikiendelea kusimama kwa muda hadi hali ilipotulia na mwishowe kuendelea na ratiba.

Nipashe ilifahamishwa baadaye jana kuwa mwanafunzi aliyejeruhiwa alikuwa akiendelea kupata matibabu.“Mlipuko umetokea mbele ya mgeni rasmi na hata mwenyewe alitaharuki, ukumbi ulizizima kwa hofu maana watu hawakutarajia,” alisema mmoja wa mashuhuda waliokuwa eneo hilo.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema hajapata taarifa hizo lakini aliahidi kutoa ufafanuzi pindi zikimfikia.

Chanzo; Nipashe
 
Watu wanaiga iga vitu tuu. Ati viwanda. Wangekufa je. Alafu nilipokuwa nasoma hii habari nimejikuta nacheka tu jinsi ya uandishi huu ni kama comed hivi. Pole kwa majeruhi ila wasifanye fanye michezo.
 
Kuna mdau alisema mfumo wetu wa elimu una dosari nyingi, yawezekana alikuwa sahihi ...kama watoto wanaweza kuwa subjected kwenye mazingira hatari namna hiyo je nani atapenda kusoma science, na je huko tunakokwenda tutafika!!!???
 
Back
Top Bottom