Dar es Salaam: Mji salama zadi kwa kwa wanawake kuliko Nairobi na Kampala

BigBro

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
3,192
9,802
Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania ndilo jiji ambalo wasichana na wanawake wanajihisi wakiwa salama zaidi miongoni mwa miji mikuu ya kibiashara Afrika Mashariki.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti kuhusu usalama wa wanawake na wasichana dhidi ya udhalilishaji katika miji mbalimbali duniani uliofanywa na shirika la Plan International.

Jiji la Kampala linaongoza kwa kuwa hatari zaidi, ambapo wataalamu wanasema wasichana na vijana wa kike wamo katika hatari ya juu zaidi ya kudhalilishwa wa kingono wakiwa katika maeneo ya umma.

Sharon, mama mwenye miaka 19 anayeishi mtaa wa mabanda Kampala, aliambia Plan International kwamba matokeo hayo si ya kushangaza hata kidogo.

"Utekaji nyara hapa ni wa kawaida kuliko mnavyofikiria. Kila wakati unasikia kuhusu watu ambao wameuawa, kubakwa au kutekwa nyara," alisema.

"Hili hunifanya nijihisi kutokuwa salama. Kazi yangu hunilazimu kufanya kazi usiku na nafikiria wakati mmoja huenda nikawa mwathiriwa."

Jiji la Nairobi ndilo linalofuata miongoni mwa miji ya Afrika Mashariki iliyoshirikishwa na Dar es Salaam ni mji wa tatu.

Maana ya udhalilishaji iliyotumiwa ni pamoja na kujisukumiza au kujisongeza kwa wanawake katika maeneo ya umma, kuwagusa maungo bila hiari yao, kuwakejeli au kuwatania, kuwakodolea macho wasichana wanapokuwa wanapita, na pia kuwafuatilia mienendo yao bila hiari yao.

Kando na miji ya Stockholm, Dublin na New York, miji mingine yote iliyoshirikishwa katika utafiti huo ilibainishwa kuwa hatari kwa wasichana katika maeneo yake ya umma.

Utafiti huo uliangazia miji 22 na kuwahusisha wataalamu wa masuala ya haki za watoto na wanawake karibu 400 katika miji hiyo.

Wataalamu walikadiria hatari kwa kueleza miji waliyohisi ina hatari ya juu na hatari ya juu zaidi.

Katika miji ya Bogota na Johannesburg, kulikuwa na maafikiano kwamba si salama hata kidogo.

Kwa jumla, mji wa tatu duniani kwa kutokuwa salama kwa wanawake ni Delhi kisha inafuata Lima kabla ya kufikia Kampala.

Mji wa Kampala hata hivyo unaongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha 'hatari kuwa juu zaidi'.

Jiji kuu la Kenya, Nairobi linaifuata Kampala ingawa kwa kiwango chake cha 'hatari kuwa juu zaidi' ni chini ya asilimia 40.

Baada ya Nairobi, kuna Cairo, Sao Paulo, Dhaka, Jakarta na Paris kabla ya kuifikia Dar es Salaam ambao ni mji wa 12 kwenye orodha ya jumla.

Kwa kuangazia unyanyasaji wa kingono na ubakaji, Johannesburg inaongoza ikifuatwa na Kampala, huku Nairobi ikiwa ya nne na Dar es Salaam ya 13.

Mmoja wa waliochangia kutoka Johannesburg alisema: "Unyanyasaji wa kingono hutokea mara nyingi sana kiasi kwamba tunahisi ni jambo tunalofaa kutafuta njia za kulizoea kuishi nalo na kuendelea na shughuli zetu."

Kwa wizi na uchopozi, Johannesburg inaongoza, Kampala ni ya nne ikifuatwa na Nairobi. Dar es Salaam inapanda juu kidogo ikilinganishwa na visa vingine, ambapo hapa inashikilia nafasi ya 10.

Dar es Salaam pia iko juu kwa hatari ya wasichana kutekwa nyara, ambapo inashikilia nafasi ya tisa, hapa ikiizidi Nairobi ambayo ipo nafasi ya 13. Kampala inaongoza kwa hili, sawa na hatari ya visa vya mauaji ya wanawake maeneo ya umma. Kwa hili, Nairobi ni ya 11 lakini Dar hatari ipo chini sana, ambapo wanashikilia nafasi ya 17, kiwango cha hatari kikiwa chini ya asilimia 10.

Kwa jumla, wanawake katika miji mikuu ya Kenya, Uganda na Tanzania hutengwa katika asasi zinazofanya maamuzi kuhusu usalama mijini.

Hali ni mbaya zaidi Kampala, ikifuatwa na Dar es Salaam ambayo ipo nafasi ya 16 kwa wanawake kutoshirikishwa. Nairobi ni ya pili kutoka mwisho, ishara kwamba wanawake wanashirikishwa zaidi mji huo wa Kenya katika maamuzi.

Lakini kwa kuzingatiwa kwa maoni ya wasichana na vijana wa kike, hali ni afadhali kidogo Dar es Salaam katika nafasi ya 19, kuliko Nairobi nafasi ya 15 na Kampala nafasi ya 10.

Sheria kuhusu usalama wa wasichana na wanawake Afrika Mashariki zinafanikiwa zaidi Dar es Salaam iliyo nafasi ya 18, kuliko Nairobi (14) na Kampala (6).

Inakadiriwa kwamba kutakuwa na wasichana karibu 1 bilioni wa chini ya miaka 18 duniani kufikia mwaka 2025.

Wengi wao watakuwa miongoni mwa watu 5 bilioni duniani watakaokuwa wanaishi mijini kufikia mwaka 2030.

CREDIT; BBC Swahili
 
Dar es Salaam mji wa kujiachia.

Kama huamini panda pantoni weekend uelekee kigamboni ndio utajua Dar es Salaam watoto wa kike wanajua kujiachia aiseeee na wako huru.

Nakubaliana kabisa na hiyo ripoti.
 
Dar es Salaam mji wa kujiachia.

Kama huamini panda pantoni weekend uelekee kigamboni ndio utajua Dar es Salaam watoto wa kike wanajua kujiachia aiseeee na wako huru.

Nakubaliana kabisa na hiyo ripoti.
Usisahau kusema na ma beach boy wanavyowafanya kwny maji chief.
 
Usisahau kusema na ma beach boy wanavyowafanya kwny maji chief.
He he he he
Mkuu na wewe ni miongoni mwa wale wanaowafundisha warembo kuogelea free??

Nimepakumbuka sana Mikadi enzi hizo kijana bado nina nguvu za kutosha
Nilitoa sana hio huduma ya kuwasaidia watoto wazuri kujifunza kuogelea.
 
Back
Top Bottom