Dar es Salaam - Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia

Yaan inauma sana mtu kama m kafulila moja ya watu aliyefichua sakata la ESCROW anapigwa chini araf waliokutwa na hatia wanapita hv hv yaan tena mtu anakwambia vijisenti vya mboga
WATANZANIA tuna nini vichwani

Eti watu kama kafulila na wenje na mkosamali wanapigwa chini halafu bungeni wanaenda wakina nape na lusinde 😠. Upumbavu na Ujuha wenye kiwango cha PhD
 
Lile babu linafiki sana, ndo maana makonda alilitia mangumi
Umeona mkuu eeeh? Yaani nakwambia hata mimi sasa hivi nalichkia kama nini sijui, hata nikimkuta Makonda analitandika makofi barabarani nitamsaidia kulitandika makofi!!
 
Safiiii arudi udsm akafundishe siasa siyo sehemu ya majaribio

Kiukweli kama isingekua ubinafsi wa wachache...dar karibu yote ingekua ukawa. Majimbo ya segerea na kigamboni tumeyatoa sadaka wenyewe...yalikua yetu kabisa. Hata ilala zungu kaponea chupuchupu. Ila si haba hata kwa hayo tuliyopata...halmashauri za dar ziko chini ya ukawa.
 
Wanagoma kuachilia jimbo kwa ukawa maana miradi yao fake itakwama.
Na wananchi wamekataa ccm kutokana na ulaghai wao wa miradi fake kupitia mgongo wa serikali kumbe ni ya Jordan na timu yake.

jordan ndo nani???? na team yake ni akina nani???
 
Davis Mosha ni kijana mwema sana, alikuwa na mipango mizuri sana na moshi mjini. Alitaka kuijenga Moshi iwe kama Dubai, lakini bahati mbaya wapiga kura hawakumuelewa na wameamua kumuweka pembeni.
Eti alitaka kuijenga moshi iwe kama Dubai.. Nitajie mbunge yoyote tangu uhuru ambaye amewahi kufanya hivyo. Pili ni ipi kazi ya mbunge? Ikiwa Serikali yenye kila kitu imeshindwa kuijenga Dodoma tangia uhuru mpaka leo ndiyo ataweza huyo mgombea ambaye nasikia hata makazi hapo moshi hana?
 
what amazes me is that, huyu mtu alikuwa kwenye mstari akaona watoto wadogo wanapiga kura, kwanini haku report? akilalamika sasa hivi inakuwa shida kufuatilia. Kwanini asi report na kukaa mpaka sasa hivi?

Kuhusu ku support CCM, mimi naona mabadiliko ya kweli yako CCM tu, hata kama speed ni ndogo, huko nje wanataka kujenga ghorofa za udongo wa mfinyanzi. HAITATOKEA wengi wameshashtuka na ndio matokeo haya.

Mkuu vitu vyenye kuhitaji ushahidi havihitaji papara. Ukisikia jirani yako ana mtafuna mamaa wakati ukiwa safarini usikimbilie polisi haraka haraka. Subiri siku umkute juu yake ( Kizibiti / Ushahidi - japo ushahidi mwingine mpaka usubiri umkamate mhusika unaumiza roho kidogo ) ndipo uende kushtaki. Mabadiliko ya kweli yapo kwako na sio kwenye CHAMA.
 
Wadau napenda kutoa pongezi kubwa sana kwa wakazi wa kata ya Goba kwa maamuzi yao ya kuipa CHADEMA kata hiyo kwa wasiofahamu hii Kata tangu tumepata uhuru haijawahi kuwa chini ya wapinzani.

Kata hii ina mitaa karibu 8 ila ni mitaa 2 tu ndiyo ipo chini ya wapinzani.

Hongereni sana kwa huu ushindi.
 
Matokeo yaliyotangzwa rasmi punde na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la kinondoni
Ndugu Abadallah Maulid mtulia CUF ameshinda dhidi ya Idd Azan wa CCM. Ni shangwe zimelipuka maeneo ya kinondoni, mwananyamala magomeni nk

Abdallah Maulid Mtulia CUF kura 70,337
Idd Azan kura CCM 65,964
 
hah hahah hahah yaan ni furaha ya ajabu

HALIMA ana maana nyingi kwetu sisi
1.SI KILA MDADA LAZMA AJIKOMBE KWA WANAUME WALAKU ILI AFANIKIWE
2.HAIITAJI KUWA MILIONEA ILI UWE MMBUNGE HASA KWA MAENEO YA KAWE

3.KUBWA ZAIDI NI KUWA USHINDI WA MDEE INA MAANISHA KUWA NI KUKATALIWA KWA JAJI WARIOBA.
warioba mwanaye kapewa nafasi ya kugombea ubunge kukamfanya ashindwe kujua ni nani hasa anasimamia.MARA KATIBA MPYA...MARA CCM ILEILE....yaan haeleweki

DOWN JAJI WARIOBA....

Makonda Oyeeeee!!
 
Alhamdulilah. Tusingefanya ujinga wa kuweka majina ya CUF au chadema tungechukua Dar nzima.

Bado Temeke na Mbagala....ilala, segerea na kigamboni zilikuwa zetu basi tu makosa ya kijinga yametugharimu...majuto ni mjukuu....
Kama ikitokea by election kwenye hayo majimbo tuwanyoe bila maji
 
Back
Top Bottom