Dar es Salaam inapanuka sana. We fikiria mwenyewe jambo hili

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Zamani watu walikuwa wanakataa viwanja Ubungo Kibangu, wakawa wanakataa viwanja Kimara, wakawa wanakataa viwanja Mbezi...leo hii watu wanajenga Kibaha wanafanya kazi Dar Posta.

Stand leo hii inajengwa Mbezi Luis ya magari ya mikoani. Miaka kadhaa ijayo utakuta inahamishiwa Chalinze, ukikaaa kaa tena utakuta inaenda jengwa Morogoro, ikikatika tena utakuta inahamishiwa Iringa na Dodoma.

Maisha yanakimbia kwa kasi sana. fikiria mtu anaishi mkoa wa Pwani Kerege ananunua mahitaji yake Dar Bunju, Bocco.

Hii dunia kwa sasa kama unapewa kiwanja Mikumi chukua tu. Usije ukasema porini. Kesho na keshokutwa utakuta unakuja lazimika kununua kiwanja mlima Kitonga na hali ulipewa kwa bei ndogo Mikumi ukakataa. Majuto ni mjukuu usije sema sikukwambia.
 
Swadakta....

Mwaka 1998 Januari Mosi, Siku ya Jumamosi Saa 10 Ya Alasiri na kamanda wa Polisi Dar es salaam akiwa Alfred Gewe na kituo cha TV chenye kuangaliwa kwa wingi kikiwa DTV na nikiwa mtoto wa shule ya msingi nilipata ajali mbaya ya gari pale Tegeta nikitokea Shambani Bunju...

Kipindi hicho Barabara ilikuwa ni ya KOKOTO yenye vumbi tele....

Nikiwa ndani ya gari Binafsi kutokea Shambani Bunju, tuligongwa vibaya na Daladala(kipanya) kilichokuwa kinatoka mjini kuelekea DEGE BEACH...vijana wasiopungua 5 walipoteza maisha yao baada ya gari walilopanda kuanguka pale DARAJANI na kupinduka juu chini...

Alhamdulillah sisi hatukupoteza uhai zaidi ya majeraha.

Nimeanza mbali baada ya juzi kumwambia mdogo Wangu mmoja anayesoma shahada ya kwanza kuwa PINDIPO atakapopata PESA...basi atajenga nyumba MASAKI YA KISARAWE kuelekea MTAMBA KISARAWE...akacheka sana.....

Miaka 22 baadae hali ya BUNJU na TEGETA si ile iliyokuwa 1998....

Miaka 20 baadae hali iliyokuwa CHAMAZI na Mbagala yote si hii ya sasa....

Vipi Goba?
Vipi Majohe?
Vipi Chanika?

Haya Barabara ya Mbagala huelekea KIBITI....
Haya Barabara ya Pugu Kajiungeni ni jirani na Msitu wa KAZIMZUMBWI.....

Wale wanaotaka Kuishi na kujenga mjini watafanya LAND RECLIMATION kule baharini Kigamboni?!!!!

Jombaaa Umeongea BAYANA kuwa MBEZI LUIS ilipo STAND KUU YA MABASI YA MIKOANI Wala si mbali kabisaaaa...

Wakubwa zetu watakueleza kuwa zamani hizi kambi za Jeshi za hapa Dar es salaam zilikuwa mbali mnooo.....leo?!!!

Lugalo hiyo hapo...imezungukwa na makazi ya wanamji....
Ya Mbagala hiyo hapo....Mbele Kizuiani, pembeni Kibondemaji, nyuma KIJICHI kule...
Ya Gongo La Mboto hiyo hapo...mbele Guluka Kwalala....pembeni Pugu, nyuma Songosongo, Kipunguni na Majohe......

USHAURI:

JIJI LINAKUA KWA KASI...hebu kimbilieni kupata maeneo ya kujenga huko nje ya jiji....hata Kama ni KISARAWE ama MKURANGA kwani SERIKALI YA AWAMU YA 5 inajenga miundombinu ya BARABARA BORA NA NZURI juu yake zipite MABASI YA MWENDOKASI kila CHOCHORO....



Maendeleo hayana CHAMA
 
Umeongelea hilo la kambi ya jeshi.

Zamani kuna kipindi nilipokuwa Uingereza niliona kambi ya jeshi (sehemu yaitwa Aborfield) ikihamishwa kwenda sehemu ingine ili kupisha makazi ya watu.

Ile kambi imegeuzwa hadi leo ni makazi ya raia wa kawaida na jeshi limehamia maporini huko kuanzisha kambi mpya.

Muda si mrefu Lugalo italazimu kuihamisha.
 
Umeongelea hilo la kambi ya jeshi.

Zamani kuna kipindi nilipokuwa Uingereza niliona kambi ya jeshi (sehemu yaitwa Aborfield) ikihamishwa kwenda sehemu ingine ili kupisha makazi ya watu.

Ile kambi imegeuzwa hadi leo ni makazi ya raia wa kawaida na jeshi limehamia maporini huko kuanzisha kambi mpya.

Muda si mrefu Lugalo italazimu kuihamisha.
Facts....

Time is not our best Ally, Time will tell ..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom