Dar es Salaam imekuwa Dampo la biashara

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,734
3,017
Ndugu,

Nina mda cijakanyaga Dar last week nilikuwa huko kwa mishe zangu kiukweli kinachoendelea kinasikitisha sana.

1. Barabara zimegeuka frame za maduka, mbaya zaidi wanafanya biashara mbele ya frame za watu.

2. Ni vurugu hakuna kwa kupita kila kona ya jiji ni uhuni unafanyika.

3. Wanaofanya biashara ni wachafu kupitiliza hawajali kanuni za afya.

Napendekeza kwa Dar machinga walipe 50000/= kwa mwaka ili wapewe kitambulisho cha ujasiliamali.

Pia serikali iangalie utaratibu wa kuzuia mambo ya ajabu yanayoendelea hapo.
 
Anayetuongoza mchafu amezoea kulala na ng’ombe unategemea nini?
 
Watu wameziba mitaro yote ya maji barabarani, mvua ikinyesha inaziba makaravati, maji yanaharibu Kingo za Barabara! Biashara zinafanyika maeneo hatarishi!

Masoko yapo hayatumiki, kwenye biashara zenye leseni TRA hawatetei, waenda kwa miguu hatuna pa kupita! Barabara zimejengwa zinageuzwa masoko foleni inabaki pale pale watu wanapoteza muda mwingi njiani huko!! Rejea kariakoo hakupitiki, Mbagala mwisho hapapitiki, Tegeta kwa ndevu watu wanakesha kwenye foleni kuanzia iptl kisa biashara barabarani, manzese, river side ili uingie kwa flyover unakutana na foleni isiyokuwa ya lazima, Tanroads, jiji, Meya, DC, Nani amewaloga!?

Tunahitaji ustaarabu kidogo kwenye hii miundombinu michache iliyopo!!!
 
Bora nyingi ya hizo bidhaa zingekuwa zinazotoka kwenye viwanda vyetu na sio kwa Wachina. Kifupi imekuwa dampo la bidhaa za mchina.
 
Nchi ni yetu sote! Kwa asiyetaka bughuza anunue kisiwa akae mwenyewe
Upo sawa kabisa ila sidhan nikija kwako nitakuta jiko, kitanda, stoo, na vingine vyote Sebuleni!! Lazima itakuwa umependezesha sebule yako!! Vivyo vivyo kwa majiji yetu kuwe na utaratibu!! Unakuta watu wamezuia njia ya waenda kwa miguu!! Kwa manasi yake hii sio sawa kwa watumiaje wengine!! Fikiria gharama ya hiyo njia na kodi ya huyu muuza mananasi.
 
Hakuna namna waache watu wapambane tu maana hali ni ngumu mtaani ajira akuna ingawaje wanaleta uchafu na usumbufu barabarani
 
Hii ni kwa miji yote siyo Dar peke yake, machinga na vibanda ni kila kona hata pa kupita imekuwa tabu.
 
Back
Top Bottom