Dar es Salaam iendelee kubaki kuwa Makao Makuu ya nchi kwa vitendo

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,707
2,000
Kwanza, Dodoma inaweza kuendelea kubaki kuwa makao makuu ya serikali, kisheria na kiutaratibu katika makaratasi ili kuwaridhisha wanaopenda kuganda katika mawazo ya Nyerere na kuona anaendelea kuheshimiwa.

Pili, Dodoma kuwa katikati ya nchi haifanyi shughuli zote za kiofisi kufanywa kwa ufanisi bila kuathiriwa na umbali. Nairobi, Kampala, Washington, London, Beijing n.k haziko katikati ya nchi zao. Ni ushamba kuamini mji mkuu unapaswa kuwa katikati ya nchi.

Tatu, Dar es Salaam na miji mingine pembeni ya bahari ni sehemu salama zaidi kwa ajili ya makazi ya Rais kutokana na jografia zake.Rejea jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 na jinsi Nyerere alivyoweza kiwatoroka waasi.

Nne, serikali kuhamia Dodoma hakujasaidia kupunguza ujazo wa watu Dar es salaam. Ukiacha Maofisi ya serikali tu shughuli nyingine nyingi za kibiashara bado ziko Dar es Salaam.

Tano, hatupaswi kupanua miji kama Dodoma na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kwa kuhamishia makao makuu ya nchi katika hiyo miji. Kama hivyo ndivyo tunavyofanya, tuhamishie makao makuu ya nchi mji gani mwingine baada ya Dodoma ili kuukuza?
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,474
2,000
Kwanza ni ujinga kuingia gharama kujenga mijengo yoote hiyo eti makao makuu yawe Dodoma kwa kigezo kuwa ipo katikati.

Wazo la kuhamia Dodoma kwa kigezo Cha kuwa katikati lilikuwa na mantiki miaka ya 60 na 70. Wakati huo kulikuwa na miundombinu duni sana.

Mwendazake aliamua kujitengenezea ulaji kupitia "Mayanga Construction" iliyokuwa inachukuwa tenda zote za ujenzi wa majengo hapo Dodoma.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,707
2,000
Museveni alitua Dar, Dangote Dar na Masisi atatua Dar
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom