Dar es Salaam: Gharama za kujifungua ni Tshs 75,000. Uchaguzi huu unakupa nafasi ya kukataa uharamia huu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,562
217,875
Wajawazito wanaojifungulia kwenye Hospitali ya Rufaa ya Temeke , wale wanaojifungua kwa njia ya kawaida inawalazimu kulipia pesa taslimu ya kitanzania shilingi elfu 75 kama gharama ya kuzaa , Wale wanaojifungua kwa njia ya upasuaji wanapaswa kulipa zaidi ya Tsh laki 2 na yaweza hata kufika laki 2 unusu kutegemeana na complications .

Gharama hizi hazijumuishi gharama ya vifaa ambavyo mjamzito anapaswa kuingia navyo chumba cha uzazi ikiwemo pamba na gloves.

Kwahiyo basi uchaguzi huu unakupa nafasi ya kuchagua kuendelea kulipia gharama ya kuzaa au la , wale waliotuaminisha kwamba tuendelee kufyatua watoto kwa vile elimu ni bure ni vema wangeanzia kuondoa hii kodi ya kuzaa ili mambo yawe mepesi zaidi na kuwezesha wananchi kufyatua watoto kwa amani zaidi.
 
Huu ni uongo kabisa. Mwanafamila wangu amejifungulia kaloleni hospitali. Hatukulipa hata senti moja. Ilkua mwezi wa sita, na huduma ilikuwa Safi Sana, usafi wodini, huduma ya mama na mtoto imeimarishwa Sana Tanzania. Hakuna hizo garama kwenye hospitali ya serkali

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Unazo risiti za mama aliyetozwa hizo gharama? Weka hapa ili bandiko lako liwe na mashiko zaidi. Acha uzushi kama wa salon
kuweka risiti hapa ni kumchongea bure mama kichanga , halafu tozo hii siyo siri iko wazi kabisa na ni utaratibu halali kabisa na wala si magendo , tumeweka uzi ili wazaaji waliodanganywa waelewe
 
Acha upoyoyo safari hii magu kawashika kwenye kende hamna kitu chakuzungumzia mmebakiza ni uongo na uzushi tuu kenge nyie.
 
Huu ni uongo kabisa. Mwanafamila wangu amejifungulia kaloleni hospitali. Hatukulipa hata senti moja. Ilkua mwezi wa sita, na huduma ilikuwa Safi Sana, usafi wodini, huduma ya mama na mtoto imeimarishwa Sana Tanzania. Hakuna hizo garama kwenye hospitali ya serkali

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Uzi unazungumzia DSM , hata hivyo tunakushukuru kwa kuchangia
 
Sasa elfu 75 nayo hela ya kulalamika wakati unaenda kupata huduma ya kujifungua?

Unataka kuzaa tu bila kujua gharama za kuzaa?
.
Kama uanalalama 75 elfu ya kuzaa utaweza gharama za malezi kweli wewe?
 
kuweka risiti hapa ni kumchongea bure mama kichanga , halafu tozo hii siyo siri iko wazi kabisa na ni utaratibu halali kabisa na wala si magendo , tumeweka uzi ili wazaaji waliodanganywa waelewe
Juzi waziri mkuu akiwa ukara amewauliza akina mama juu ya hili suala,wamekataa.

Kama ni kweli huwezi kumchongea,maana ni habari ya ukweli,ila wewe ni muongo. Mimi sipendi makamanda waongo.
 
Natolea mfano sehemu nilizopita mkoani kagera mama mjamzito unatibiwa bure clinic bure dsm palestina mtu unajifungua bure.
 
Unazo risiti za mama aliyetozwa hizo gharama? Weka hapa ili bandiko lako liwe na mashiko zaidi. Acha uzushi kama wa salon
Kaka mimi sio mwanasiasa wala huwezi kunikuta nachangia mada za siasa lakini hili la kutoza 75,000 kujifungua kawaida na 200,000 kwa njia ya operation ni kweli kabisa.
Mke wangu alijifungulia Amana hospital baada ya kupewa rufaa nililipa 249,000 ikiwa laki 2 kama gharama ya kujifungua na 49,000 kama gharama ya dawa za maumivu baada ya kujifungua.
 
Mimi nitaamini hii post yako bila kuweka risiti ulizotozwa?
 
kuweka risiti hapa ni kumchongea bure mama kichanga , halafu tozo hii siyo siri iko wazi kabisa na ni utaratibu halali kabisa na wala si magendo , tumeweka uzi ili wazaaji waliodanganywa waelewe
Mkuu upo sahihi kabisa mke wangu alienda kujifungulia Amana hosptal kwa njia ya operation nilishangaa kuambiwa natakiwa kulipia 200,000 kama gharama ya kujifungua na 49,000 ya dawa.

Nilielekezwa dirisha la kulipia na nililipia kihalali kabisa na risiti nikapewa.

Ni wamama wote walifuata utaratibu huu na nilishuhudia mama mmoja akizuiwa kuondoka wodini baada ya ndugu zake kushindwa kulipa gharama hii.
 
swadakta
 
Back
Top Bottom