Dar es Salaam biashara zinakufa kwa kasi sana

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
Dar es Salaam inachakaa kwa kasi ya ajabu. Mtaa wa Samora, moja ya mitaa ya jiji iliyokuwa kitovu cha biashara ya bidhaa halisi kwa sasa inatia huruma. Biashara ni kama hakuna na zilizobaki hazina wateja. Ule ukijani na marashi ya Mtaa wa Samora sasa ni historia.

Mabenki kama NBC ukienda pale Corporate Branch unakuta wateja kwa idadi ya single digit na tellers wawili tu ndo wako on duty. Dar es Salaam inakufa kwa kasi.

Nenda Mlimani City kuna fremu nyingi tu ziko wazi.

Pita eneo la viwanda Nyerere Road vitega uchumi vya Quality Group sasa hivi ni uwekezaji wa popo na jamii zingine za ndege wa usiku.

Kama nchi nadhani kuna shida mahala.

Rais ajae ana mtihani.
 
Safi sana, na izidi kuchakaa kabisa ili na sisi watanzania tulio mikoa mingine ( mnatuitaga wamikoani ) turudishiwe heshima yetu ambayo ninyi wadarisalama mmeitwaa kinguvu kwa miaka mingi.

It's time to invest in other regions letting their economic growth see off Dar es salaam in the long run.
 
Kinachoendesha sekta ya fedha ni mzunguko wa pesa, sasa benki zitafanya vipi transactions ikiwa shughuli za kibiashara zimedorora kutokana na mzunguko mdogo wa pesa....haya kwa sasa siyo mitano tena, tumlazimishe..
 
Dar es Salaam inachakaa kwa kasi ya ajabu. Mtaa wa Samora, moja ya mitaa ya jiji iliyokuwa kitovu cha biashara ya bidhaa halisi kwa sasa inatia huruma. Biashara ni kama hakuna na zilizobaki hazina wateja. ule ukijani na marashi ya Mtaa wa Samora sasa ni historia...

Ni zamu ya Chattle aisee...! Asante.
 
77 Reactions
Reply
Back
Top Bottom