Dar es Salaam: Ahukumiwa kifungo cha nje na fidia ya 20,000 baada ya kumpiga mkewe kwa mwiko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Dar es Salaam.

Mahakama ya Mwanzo ya Buguruni imemhukumu kifungo cha nje cha miezi minne mkazi wa Tabata Segerea, Baraka Athuman (33) baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mke wake Kuluthum Khamis kwa kutumia mwiko wa ugali kutokana na wivu wa mapenzi.

Pia, mahakama hiyo imemwamuru mshtakiwa amlipe mkewe huyo kiasi cha Sh20,000 kama fidia ya matibabu.

Akitoa hukumu hiyo juzi Hakimu, Gladness Njau alisema ushahidi uliotolewa na mlalamikaji pamoja na mume wake Athumani kukiri mahakamani hapo kumpiga Kuruthum sehemu mbalimbali ya mwili wake, ulitosha kumtia hatiani. Alidaiwa kumpiga kwa mwiko wa ugali baada ya kumfumania akiishi na mwanaume mwingine.

Alisema kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji pamoja na mshtakiwa mwenyewe mahakama hiyo imejiridhisha kuwa ni kweli alimpiga Kuruthum sehemu mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia maumivu makali mahakama hiyo inamtia hatiani.


Mwananchi
 
Huyo hakimu hajui maumivu yake. Mwiko tu hukumu? Daah huu uchumi wa kati tutaona mengi
 
Mi kusema kweli nampa pongezi hakimu. Angekua feminist hapo ungesikia Miaka 5 jela.

Hapo jamaa ampe tu iyo 20,000/= uyo bibie hafu kila mtu acheki pande zote.

Hafu shukrani za pekee pia ziende kwa Baraka kwa kutomuua wala kumkata mapanga uyo m***ya.

Uyo mwanamke walimjaza upepo akajua atalipwa pesa nyingi sasa Elfu 20 sta kijola haitoshi na taraka juu.
 
Hivi mtu akihukumiwa kifungo cha nje kinakuaje yani ? Huwa sielewi hapa !!
Kwa mujibu wa kifungu na 3(2) (a) cha Sheria ya Huduma kwa Jamii ya mwaka 2002 kifungo cha nje ni utaratibu ambao unampa fursa mfungwa kutumikia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli/kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya jamii.
 
Back
Top Bottom