Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,657
- 22,252
Hivi karibuni watoto wa darasa la saba walimaliza kufanya mtihani wa kuingia kidato cha kwanza, kama kawaida maeneo mengi ya Dar. kila baada ya mtihani harusi za watoto hao huanza, ni mavuno mitaani kwetu. Inaelekea serikali huwa hsiwaandai viongozi wa serikali za mitaa kuhusu kuzuia harusi hizo ambazo huenda baadhi ya watoto hao watafaulu kuingia kidato cha kwanza. Tusimpe kazi Mwanri (najua yuko Tabora) ya kuanza kusukuma ndani wachagua mchele, wapiga ngoma, mashangazi, wajomba, waoaji na wanaoolewa, serikali ianze kuzuia sasa ingawa tayari imechelewa.