Dar Coach wazidi kushusha bei zao za uundaji body za mabasi

Hapo kinachofanya bei iwe juu ni chasis na engine ni vya scania F95HB310 ni engine ya kisasa inayotumia mafuta vzr kwa pungufu ya 30% ukilinganisha na zile scania 113 series, na zinadumu kwa muda mrefu ni tofaut na engine za kichina ambazo zikikaa miaka 2-3 lazima ubadilishe uweke mashine, gear box na difu ya scania
Maneno ni mazuri sana, lakini wateja wanapenda zile body za kichina kwa muonekano wake. Wangejitaidi kuboresha muonekano wake bila ivyo ngoma nzito biashara ina ushindani sana.
Tatizo wateja wengi wanapenda youtoung mchina
 
Maneno ni mazuri sana, lakini wateja wanapenda zile body za kichina kwa muonekano wake. Wangejitaidi kuboresha muonekano wake bila ivyo ngoma nzito biashara ina ushindani sana.
Tatizo wateja wengi wanapenda youtoung mchina
Hata dar coach anatengeneza basi kama ya mchina tuu havina tofaut labda teknolojia maana material anachukulia China kwa hiyo ukitaka yenye mwonekano wa kichina eg sitting configuration, air con na automatic door's ni hela yako nenda angalie dar exp zile crystal plate no T*** DBU ni imetengenzwa dar coach ila interior yake kama bus za mchina tuu, alafu watu wanachanganya China wao wanaunda body eg yutong, zhongtong au higer alafu chasis na engines zinatengezwa USA ni za cummins
 
Maneno ni mazuri sana, lakini wateja wanapenda zile body za kichina kwa muonekano wake. Wangejitaidi kuboresha muonekano wake bila ivyo ngoma nzito biashara ina ushindani sana.
Tatizo wateja wengi wanapenda youtoung mchina
Mkuu huo utafiti wako umeufanya lini wa kuonyesha kuwa wateja wengi wanapenda mabasi ya kichina?siyo kweli kwani kwa sasa wateja wanapendelea sana mabasi ya scania japo hilo haliondoi ukweli wa mabasi ya kichina kupata abiria kwani ndiyo mengi yaliyopo sokoni
 
Sio utani Mkuu, ukitaka nenda kachonge la kawaida kwa 120mil
Iyo akichonga atapanda yeye na family yake . Kwanza iyo itakuwa Eicher au UDA. Biashara ya magari sio biashara ya kitoto inataka mitaji na sio bei za kubembelezaa kuna watu wengi wameweka mitaji yao mikubwa katika izo biashara.
Watu wana boresha kulingana na wateja wanataka nn?
 
Kweli watu mpo gizani, hapa hapa Tanzania ubungo hapo kuna bus za milion mia 7 unasema bei hiyo? Hivi unafikiri zile Marcopolo za Abood na Hood walinunua sh ngapi? Milion mia 5 na kitu, ila guarantee yake ni miaka 10.. Msione vyuma vya watu vipo road mkachukulia poa! Unazungumzia faida? Unajua scania r au g mpya ya kwenye makaratasi inauzwa bei zaidi ya hiyo iliyotajwa kwenye haya mabus? Hapo ni horse tu hujagusa trailer? Hiyo ni bei ya kawaida sana Mkuu.
Ndio maana watu wengi wanakwambia ukitaka kuona maajabu ya Tanzania, njoo UBUNGO BUS TERMINAL.
Njoo asubuhi uone matajiri wa Tanzania walivyo na umiliki wa magari, ndio ukitoka apo ukajitathimini kama iyo milioni 480, ni pesa au? Maana mtu ana magari ya milioni 700, kama 20 yote yanaondoka siku iyo iyo
 
Maneno ni mazuri sana, lakini wateja wanapenda zile body za kichina kwa muonekano wake. Wangejitaidi kuboresha muonekano wake bila ivyo ngoma nzito biashara ina ushindani sana.
Tatizo wateja wengi wanapenda youtoung mchina
Wateja wa wapi? Mi naona wateja wa luxury wanapenda Marcopolo mixed na Scania. Useme hao wamiliki wamekalia michina kwahiyo wateja hawana uchaguzi. Unakumbuka Paradiso za scandinavia?
 
Wafanyabiashara wengi hawataki kuwekeza pesa nyingi hivo kwenye scania na kukimbilia za mchina sababu akinunua mchina kabla halijaharibika tayari linakua limezaa lingine,kuliko kutoa 450m kwa bus moja anaona itachelewa kumlipa.

Haujiulizi hata tajiri namba 1 afrika anatumia trucks za Howo?
 
Mkuu engine za kwenye bus nyingi yazo ni 90 series, mpaka sasa wanatoa hizi 95 mpya kama ambazo wamezitangaza kwenye huu uzi, kinachofanyika ni kile kile ingawa wengine wanasemaga mambo ya kubana pump ila kuchanganya haraka ni kwamba ile engine inaweza kubeba tani 15 mpaka 20 hivi, ila likipakia abiria na mizigo yao inakua na kama tani 8 au pungufu, so gari inakua nyepesi sana hata gear hazichukui muda kuchanganya!

Halafu kwenye roli mara nyingi tunafunga fuse ya speed, angalau kwenye 90kph, ikifika hapo inakata, ila kwenye bus wanaitoa hii so dereva anaendesha mpaka anagotesha mshale mwisho.

Halafu bus nyingi zinakua na gear 8au 10 wakati roli nyingi kubwa ukitoa hizo 90 series zinakua na gear 10,12, au 16 kabisa kwahiyo gari yenye gear nyingi hivyo mpaka ichanganye ni tofauti na huyu wa gear chache, hata ukianza kuzivua hizo gear kwenye mlima ni tofauti na dereva wa bus.

Kingine ni udereva tu Mkuu ndo unaleta huo udambwidambwi, mimi nina madereva ambao wanatoka kwenye maroli na kwenda kwenye mabus na wengine wanafanya viceversa, mfano nina madereva nilikua nao kwenye maroli ila saivi wapo Newforce, Hood, Imo na NBS,.. So hapo ni udereva tu.

Dereva wa roli hawezi kuendesha kama bus maana litamuua, kusimama na roli lilikua 100kph na mzigo wa tani 30 mgongoni ni ngumu ukilinganisha na bus la Abiria 55..
Kwanza mbali na yote Hongera kwa kumiliki biashara ya magari na kuwepo katika hii Mitandao ya kijamii, hasa hasa Jamii Forum. Maana wamiliki wengi wa magari wanakuwaga wapo nyuma sana na maswala ya technology na elimu pia. Swali langu je hii changamoto ya biashara upoje ukizungumzia upande wa serikali katika maswala ya kodi. Na vip? Kuhusu wateja wanapendelea mchina au Scania
 
Back
Top Bottom