Dar Coach wazidi kushusha bei zao za uundaji body za mabasi

IMG_5997.JPG
IMG_5998.JPG
 
Dar coach wanastahili kupongezwa, bodi zao wanatengeneza bora na zenye mwonekano mzuri kuliko zile za kikenya. huwezi amini kama zinatengenezwa hapa bongo. magari yao yanakimbia balaa na ni imara kuliko ya wachina hayo. kwa wale wa mwanza kahama bukoba watakuwa wanazijua kisbo na kina leina.
 
Kampuni ya utengenezaji wa body za mabasi nchini katika ubora wa hali ya juu ya DAR COACH , sasa inawatangazia wamiliki wa mabasi nchini na nje ya nchi kuwa imeshusha bei ya bus zake.

Ushushwaji wa bei za bus kutoka DAR COACH haupunguzi ubora wake, isipokuwa ubora umeongezwa Mara dufu.

Ushushwaji wa bei ya bus kutoka DAR COACH umesababishwa na kampuni ya SCANIA kuiamini DAR COACH na kuamini ubora wa kazi zake katika chassis za scania hivyo kuamua kutoa PUNGUZO kubwa sana la bei za chassis zake model mpya 95 kwa DAR COACH.

Kwa bei hiyo ya chassis za scania, sasa hakuna haja ya kufuata bus China kwasababu utapata bus yenye sifa zifuatazo
1.full AC
2.fridge
3.luxury seats
4.automatic doors
5.automatic boot doors
6.luxury interior
7. 7 tv's
8.zhongtong body/Crystal body/Diamond body

Kwa bei ya U.S.D $217,000/= tu hapahapa nchini .
Hivi ndio viwanda tunavyovizungumzia
 
Kilimanjaro bus usigope kusema
Awali alikua ana modify youtong akaona ujinga,
Sawaya ndio kichwa cha modify malori na mabasi nchi hii.
BoxBody=dump=bus=tanker=semi=pulling=boxbody kipisi
Hakumodify yutong,ila kipindi kile yutong f11 zinatoka takribani mwaka 2011 alizinunua kama tatu hivi ili kuonja ladha ya mchina,matokeo yake hakuzipenda hivyo akaamua kuzifumua engine na kuweka injini za malori yake
 
Bei ni kubwa kuliko kununua nje kwa sababu vyuma Tanzania ni ghali sana kwa hiyo lazima iwe ghali sana,ukitaka uwe na viwanda lazima chuma kiwepo kwanza na umeme wa kutosha bila hivyo utakwama tu.Mfana cages za kufugia kuku kwa bongo wanatengeneza mafundi wa kawaida tu mitaani lakini bei yake ni ghali kuliko kuchukua kutoka China na tatizo ni bei za vyuma Kwa Tz
Hili mkuu nilishangaaa sana yan cage ya kuku 4800 ni 32m kwa bongo ila china ni 8 to 10m
 
Million zaidi ya 470, hapo bado sijalisajili TRA, SUMATRA.......wakati Yutong au higer au zhongtong kwa pesa hiyo linakua barabarani na coaster 4 mpya nimenunua....

Changamoto bado mnayo tena kibwa aise
 
Hapo kinachofanya bei iwe juu ni chasis na engine ni vya scania F95HB310 ni engine ya kisasa inayotumia mafuta vzr kwa pungufu ya 30% ukilinganisha na zile scania 113 series, na zinadumu kwa muda mrefu ni tofaut na engine za kichina ambazo zikikaa miaka 2-3 lazima ubadilishe uweke mashine, gear box na difu ya scania
Mbona kimbinyiko zina miaka 6 hazijabadilishwa engine wala box
 
Hakumodify yutong,ila kipindi kile yutong f11 zinatoka takribani mwaka 2011 alizinunua kama tatu hivi ili kuonja ladha ya mchina,matokeo yake hakuzipenda hivyo akaamua kuzifumua engine na kuweka injini za malori yake
hehehehe we bwana unahatari:D:D
 
kila mtu na mapenzyake, abiria wanapenda gari za kichina sababu ya uluxury wake ndio maana hata dar coach wameliona hilo
mkuu falcon hivi zile bus zainabu ilikua miaka ya 2000 mwanzoni zilikua aina ya volvo zilipoteleaga wapi??
 
Back
Top Bottom