Dar coach hapa tuwape pongezi jamani

Nimefarijika na kazi za Watanzania wenzangu, vip Sabasaba walienda kuonyesha umma. Good job
 
Ah hii si sawa.. sasa mtu akiamua ashushe tu sound kwa interest zake si italeta shida
They are now coming

Nashauri wafikirie kutengeneza components za kwao badala ya kutumia za kuagiza, sina uhakika kama watakuwa wameweka virekebishio vya ulalo wa viti toka China au Ulaya, wanaweza kuweka vitu visivyodumu halafu tukarudi kuleee tulikokwepa.

Kadhalika nashauri speaker ndani ya basi ziwe na controls ili mteja asiyependa kelele apunguze mwenyewe au kuzima kabisa
 
Mm nikikaa kwenye Eicher tuu napitiliza kituooo,
Nikipanda hilo hakikaa naweza nipitilize mpk mbinguni,
Unashtuka paaaap upo kwa mzee baba anachochea moto pembeni unamuona magu ameshkiwa counter book quire 5 anasomewa mashtaka,
Nitakachoomba ni tender ya kuchochea kuni moto usipunguee.
Ha ha haaa ninyi watu mnatafuta kujiteka kisha ndugu zenu waanze kulalamika wakati marehemu ndiye alikuwa mchokozi
 
Kiuhalisia hawajaunda bali wameunganisha (assembling) siku hizi kila kitu kiko Internet... Ukishakuwa na engine na chassis.. Kinachofuatia unachagua shape ya body unayotaka... Baada ya hapo unachounda ni body frame tuu... Vingine vyote vinavyofuatia unafunga na kupachika.. Vilishatengenezwa... Siku hizi hakuna ubunifu tena
Kwani Yutong, Zhongtong, Higer, Marcopolo, Irzar si wanafanya hikohiko tu wanachukua chasis kwingine na kuunda body. Hebu tupende vya nyumbani, kazi wanayofanya haina tofauti na hao

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom