Dar coach hapa tuwape pongezi jamani

digalangosha

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
1,554
2,265
Bila kupoteza muda, nimepita kwenye page ya Dar coach (kampuni ya kitanzania ya kuunda bodi za mabasi) aise hawa jamaa wameunda bodi kali sana waliyoiita "tanzanite" ikiwa imevaa chasis ya scania.

Ushauri wekeni bei nzuri hili mlete upinzani kwa basi za kichina zinazozidi kuota mizizi nchini.

Pia jitahidini kufanya marketing kuwashawishi matajiri kama kina shabiby, zuberi, dar lux, sauli, dar express, klm, abood, bm, etc wanunue basi zenu....hao watasaidia kuleta chachu kwenye ushindani.

Tujivunie vya nyumbani....

Source ya picha-dar coach page, tbb
FB_IMG_1562662908117.jpeg
FB_IMG_1562663220800.jpeg
FB_IMG_1562663224138.jpeg
FB_IMG_1562663228185.jpeg
FB_IMG_1562662905353.jpeg
FB_IMG_1562692643789.jpeg
FB_IMG_1562692640707.jpeg


Sent from my SM-J727P using JamiiForums mobile app
 
'siku nzi akiacha ujinga anaweza kutengeneza asali'

kuna kampuni muundaji mzuri wa boti na meli. nadhani linaitwa Songoro kama sikosei. aisee kumbe tunaweza, sema tu ufahamu wetu tumeumbiwa kuthamini vya nje.

heko wazalendo, soon tutaendesha na magari ya kifaru toka lile kampuni letu kama litafufuliwa.

kuna haja mamlaka za ubora, costech kutupia jicho kwa wagunduzi na mafundi wenye nia ili waisogeze Tz katika aina nyingine ya uchumi kwa kupunguza mlolongo wa vikwazo na masharti.

yaani wagunduzi wajengewe uwezo+mitaji na wapewe kila msaada unaohitajika kutimiza ndoto zao kisha kazi (vilivyokamilika) wapewe wengine kuendeleza mchakato wa ubora, leseni, vibali na kusaka masoko. tumepoteza mawazo mengi kwenye ugunduzi wa helikopta, meli, magari, ndege/drones kwa wagunduzi kukosa vigezo vya mamla ikiwemo kubwa la mitaji.

cc. VETA
cc. SIDO
 
They are now coming

Nashauri wafikirie kutengeneza components za kwao badala ya kutumia za kuagiza, sina uhakika kama watakuwa wameweka virekebishio vya ulalo wa viti toka China au Ulaya, wanaweza kuweka vitu visivyodumu halafu tukarudi kuleee tulikokwepa.

Kadhalika nashauri speaker ndani ya basi ziwe na controls ili mteja asiyependa kelele apunguze mwenyewe au kuzima kabisa
 
Back
Top Bottom