Dar bila Dalali (Wapiga Debe)inawezekana??

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Kuna mjadala unaendelea TBC kama Je Dar es salaam bila dalali inawezekana??(Dalali wa nyumba za Kupanga) kila mtu ana mtazamo wake lakini binafsi mimi naona hawa local Brokers ni tatizo sana.
  • Wanakula kwa mpangaji na mpangishaji(unalipa miezi 13 badala ya 12 na Landlord anapokea kodi ya miezi 11 badala ya 12)
  • Wanapangisha double double kwa tamaa
  • Wanaonyesha nyumba iliyopangishwa tayari(Hawapo tayari siku ipite bila kupata chochote hata kwa ulaghai
  • Wanakuza bei ili maslahi yao yaboreke
  • Si wakweli na ni wasumbufu sana
  • Not Registered.Not Lincesed,Hawalipi kodi,incase of complaints anahama kijiwe na kubadili namba na wenzake wanamlinda...kama wapiga debe wa ubungo tu!
Bora wenye nyumba wapeleke taarifa zao ktk kampuni zinazojulikana
na mpangaji akaziangalie akiridhika na nyumba na terms wawasiliane
Sijui wana JF mna maoni gani hapo??
 
Mimi nadhani serikali iandae utaratibu wasajiliwe kisheria wawe na ofisi kila kitu kiwe wazi.
vinginevyo ningumu sana kuwakwepa hawa jamaa kama unatafuta nyumba maeneo usiyoyajua
 
Nadhani hatuwahitaji hawa watu in any way kwani ukichunguza majority yao ni wababaishaji ambao hawana uhakika na wanachokifanya! After all, wamekuwa gharama kwa wateja wao!
 
Hao watu wanaoitwa madalali nawachukia sana,walimleta mteja wakamwonyesha nyumba yangu kuwa inauzwa,mteja akawapa laki 2,
 
Back
Top Bottom