Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
Benki za nje zenye matawi yake Tanzania, huenda "zikafungasha virago" kuondoka nchini kufuatia sheria mpya ya madini.
Uchunguzi umebaini kuwa benki hizo zilikuwa zikitunza na kufanya miamala mikubwa ya kampuni za madini, ambapo sasa sheria mpya ya madini inazuia.
Sheria hiyo ya madini iliyoshadidiwa na kubebewa bango na Rais John Magufuli, inakataza benki za nje, zinazimiliiwa kwa hisa kubwa na watu binafsi au kampuni kutoka nje kutumiwa na kampuni za madini.
Lengo kubwa la sheria hii, ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na mwanya wa kufuatilia mapato halali ya madini na kodi inayolipwa kwa serikali.
Benki zinazoonekana kuathirika zaidi ni pamoja na Barclays, Standard Chartered na FNB.
Sheria hiyo iliyoanza kutumika mwaka huu, ibara ya 49 (2) imaeleza adhabu kwa yeyote atakayebainika kutenda kosa kinyume na sheria hii atatozwa faini Kati ya Shilingi Milioni 100 hadi Milioni 250 au kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja