Dar: Barabara ya Jangwani yafungwa kutokana na mvua zinazoendelea

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,008
9,873
Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 10:15 jioni kutokana na mafuriko kwa mvua inayoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam

Wasafiri wanashauriwa kutumia usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Morocco kwa wale wanaotokea Posta kwenda Kimara. Wakifika Morocco wanaweza kuendelea na usafiri wa DART mpaka Kimara na sehemu nyingine za Jiji

Kwa wasafiri wanaoelekea Posta kutoka Kimara, tunawashauri kuchukua mabasi ya DART mpaka Morocco ambapo wanaweza kuchukua usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Posta, Kariakooo na sehemu nyingine za Jiji

ZINGATIA: Nawa mikono kabla ya kuingia kwenye Basi, Panga foleni ukiwa kituoni kwa kuingia kwenye Basi, Usiingie kwenye Basi kwa kugombania, Subiri Basi linalofuata endapo Basi iliyopo imejaa, Bila kunawa mikono kwa sabuni au dawa, hautaruhusiwa kuingia kwenye Basi
 
Hii sasa imekuwa shida. Wameshindwa. Labda mpaka dr magufuli aseme .watendaji wengine sijui hawaoni kama ni shida!!!!
 
Si Mkuu wa Mkoa alisema anatupia kitu moja hatari sana hapa jangwani, mita 300 kwenda juu
 
hili la jagwani litaondoka na mtu huu mwaka ndio akili zitawarudia..
 
Jangwani ni kuwa watu wameshindwa kuwaza Eneo limejaa sana mchanga mpk utafika juu ya daraja
Ilipaswa kusimamiwa kwa ule mchanga utolewe kila mara.

Kuna wakati hua serikali inakumbusha kuzibua mitaro,ss jangwani sijui kunamuhusu nani
Pia mchana ule ungetumika kujenga kingo,ikimaanisha wataalamu waaweza kutadhimini kama maji yakiongezeka yatafika mahali gani.

Ukiwaza huu mto umetokea wapi na huko upitapo kuna sehemu pana shida kama jangwani

So ukitafuta suluhu utapata kujenga daraja ila kwass kama ukiwekwa mpango wa kupunguza mchanga mpk salenda italeta auheni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkwajuni kwenyewe palifungwa, tumepita na eicher roho kigumu sana. Mwendokasi haupiti, kwa taarifa za pale nasikia kuna gari ndogo imesombwa na maji toka saa 17 leo.
 
Back
Top Bottom