Dar: Baada ya kudaiwa kuwepo kwa Ugonjwa wa mlipuko wenye dalili kama za Malaria, Serikali yakanusha kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa huo

Mi nilihama dar kwa sababu ni sehemu isiyo salama kuishi mwanadamu. Hata Magufuli ameshtuka kahamia Dodoma. Huo mji ni mchafu sana umejaa maradhi na kila aina ya vihatarishi kwa afya ya binadamu.

Hewa chafu, joto kali, msongamano mkubwa wa watu, miundombinu mibovu, makazi holela sijui watu wanapapendea nn Dar. Asilimia 90 ya Dar ni Slums
Kama huna hela mji unakuchapa vibaya
lkn kama fedha ipo hata foleni huoni
 
Mimi nimepatwa na ugonjwa wenye dalili zote hapo juu, kikohozi, mafua, kichwa kuuma vibaya, na homa. Lakini kwenda kupima ikagundulika nina malaria, na baada ya kumaliza dozi sasa nimepona.
 
nilipata mafua jana ya ghafla, baadae homa ikaanza kugonga hodi, nikanyuka diklopa zikatoweka
 
Mimi sio daktari ila inawezekana kabisa kuna hewa fulani yenye sumu imepita hayo maeneo. Au la kuna sumu fulani imeingia kwenye maji au vyakula hasahasa vyakula vya baharini kama samaki na jamii zake. Uzuri inaonekana madhara sio ya muda mrefu kwahiyo msiwe na wasiwasi.
 
Huu ugonjwa chanzo chake kg niliumwa . Kungekuw na ukaguz wa haya matrain kuna watu wanabeba vimelea
 
Juzi nilikua na dalili za tonsils, jana niliamka nikiwa na joto kufika jioni joto likapanda kiasi mpaka kiti nilichoegemea kikawa kinaabsorb, kisha nikawa natokwa na goosebumps.
Maumivu ya kichwa yakawa makubwa, kizunguzungu nikijaribu kutembea hamu ya kula hakuna, lips kavu (hata baada ya kufululiza kunywa maji).
Anyway, mimi nikahisi ni Malaria, so hiyo usiku nikanunua Malafin na panadol nikatumia, nimeamka joto sina maumivu ya kichwa yamepungua (hayajaisha) nimeweza kula.

Kiukweli hii habari ningeiona nilichokifanya cha kumeza hizo dawa nisingekifanya.
 
Tusali, kufunga na kuomba kwa Mola wetu isije kuwa mabeberu yameshatuletea janga jingine kama lile la AIDS.
 
Huu ugonjwa unatokea kw mabeberuru na kuna watu wanasambaza kuna mtu alibeba mzigo unanuka kwenye train baada ya hapo niliumwa mpaka kulazwa mipaka yetu haipo salama
 
Kabudi na kaka yake wakisikia watasema ni njama za mabeberu kutupiga vita vya kiuchumi baada ya kuona tunanunua ndege kwa mpigo wanasingizia tuna malaria.
Tuunge mkono juhudi!
Pia kuna ukweli katika ilo unajua wamagharibi kuna kitu wanakiita biological weapon yn anatumia siraha za kibaiolojia kukumaliza ss majaribio yao huwa wanafanya uku Afrika mfano Ebola Dengue HIV and the likes of that

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeumwa nashukuru nimepona sikunywa dawa nilikuwa nakunywa maji tu.
 
Kupitia Mitandao ya Kijamii, baadhi ya Watu katika maeneo ya Jiji la Dar wamekuwa wakilalamika kupatwa na ugonjwa ambao dalili zake zinaendana na zile za Malaria.

Baadhi yao wanasema dalili za ugonjwa huo ambao umewapata watu wengi katika maeneo wanayoishi ni pamoja na Kikohozi, Mafua, Maumivu ya Kichwa na Homa Kali.

Baadhi ya maeneo ambayo watu wameonekana kulalamika zaidi kuhusu Ugonjwa huo ni pamoja na Kimara, Sinza, Ubungo, Kigogo jijini Dar es Salaam.

JamiiForums imewasiliana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na ameeleza kuwa Wizara yake kupitia Timu inayofanya Ufuatiliaji wa Magonjwa inafuatialia suala hilo na itatoa ufafanuzi mapema iwezekanavyo.

Inashauriwa unapopata dalili za Malaria uasiende duka la dawa na kununua dawa na kuanza kunywa, nenda hospitali ukafanyiwe vipimo na daktari.
Dah! Ninakama wiki tangia niugue hivi viugonjwa ambavyo vilichukua zaidi ya wiki mbili.
 
Kumbukeni watu wa utabiri wa mamraka ya khari yahewa nchini TMA walisema kutakuwa na mvua ikiwa na kimbunga hii mvua umevutwa na upepo km walivyokuwa wakitoa taarifa, hivyo mvua na upepo vimekuja namaambukizi haya kutokea ukanda wa bahahari. Hivyo mvua zikikatika au upepo namafua kwishe, tumia dawaza pilipili manga nk. Nisiku2 tu unapona
 
Aisee kumbe hata mm imenipata sjatoka siku mbili npo moro . nilianza kuhisi joto baadaye jioni nikaanza kusikia homa mara mafua then kikohozi na general weakness nikaenda kucheki na kukutwa na malaria 7 .mambo ya epidemiology hayo !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hali kweli kama nakubaliana na wewe, nlisafiri kwenda Mtwara hali hii ikanipata huko. Sihitaji kuelezea ila ni exactly kama ulivyoelezea.
Ndg zanguni msiombee hali hii iwakute ni hatari sana,mimi binafsi tatizo hili lilianza Ijumaa hii ya majuzi,kichwa macho kwa ndani vinauma mfano wa jua limewekwa kichwani,huku kifua kukohoa,mafua ya maji maji na mzigo wa homa juu dadeki,kimazoea nikajua hii ni maleria nikajigongea Orodar zangu na panadol,hapo nikazidiwa zaidi,nikajongea bafuni na homa yangu kali nikajaza sink maji top nikajimwaya humo kwa saa limoja nilatoka nikajipumzisha kitandani.nashukuru mungu jumatatu ya leo nimeweza kwenda kazini kama kawaida lakini kichwa bado bado kinani beep beep.Alhamdullilah
n.b.Katika siku zote tatu nilijitahidi sana kula matunda mengi ya aina mbalimbali na maji mengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom