Dar: Baada ya agizo la Sirro, watu 41 wakamatwa kwa wizi wa pikipiki 21

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Jeshi la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam limeendelea na operesheni kali dhidi ya vikundi mbalimbali vinavyojihusisha na uhalifu ikiwemo wizi wa Pikipiki, Bajaji na magari.

Kutokana na oparesheni hiyo wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 41 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Pikipiki 29 za wizi za zingine zinazotumika kuwafanyia uhalifu zimekamatwa.

Hatua hiyo inakuja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kunukuliwa akisema kuwa kuna msako mkali unaendelea kuhusu wezi wanaotumia pikipiki na vyombo vya moto, kauli aliyoitoa wakati akitembelea vituo kadhaa vya Polisi jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salam, Muliro Jumanne amesema: “Jeshi la Polisi linawaomba Wananchi waendelee kutoa taarifa mbalimbali ili zifanyiwe kazi na vitendo vya kihalifu viweze kupungua.”
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom